Sitta yamemkuta...

Sitta yamemkuta...

Joined
Jan 22, 2014
Posts
28
Reaction score
3
[h=1]Sitta aonja shubiri[/h]
  • Apokewa kwa mabango ya serikali 3 Mwanza
  • Agoma kuendesha harambee ya machinga



MWENYEKITI wa Bunge Maalumu la Katiba, na Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta, jana alipata wakati mgumu baada ya kulakiwa na kundi kubwa la watu, wengi wao wakiwa vijana waliokuwa na mabango yaliyobeba ujumbe wa ‘serikali tatu’.
Hali hiyo ilijitokeza kabla na baada ya kufungua matawi mawili ya CCM katika eneo la Sahara jijini hapa, ambapo idadi kubwa ya watu wanaodaiwa ni wafuasi wa vyama vya upinzani, walipaza sauti zao kila mara wakimwonyesha alama ya vidole vitatu, wakiashiria kutaka muungano wa serikali tatu na wengine wakionyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA.
Awali hali hiyo haikuonekana kumshitua kiongozi huyo, lakini ongezeko la watu wakati wa ufunguzi wa matawi hayo, waliokuwa wakipaza sauti zao kutaka maoni ya wananchi waliotaka serikali tatu yaheshimiwe, kulimtikisa kiasi cha kumfanya akatishe hotuba yake mara kwa mara.
Kila mara makundi ya watu hao, hususan vijana, walikuwa wakikatiza hotuba yake kwa kuimba; “Tunataka serikali tatu, tunataka serikali tatu, CCM kwisha, CCM kwisha.”
Baadhi ya vijana wa UVCCM, walionekana kukerwa na hali hiyo, ambapo nao walianza kupaza sauti zao wakimshangilia Waziri Sitta kwa kumuita “Jembe, jembe, jembe, jembe.”
Waziri Sitta, alikuwa amepiga kambi jijini Mwanza kwa siku mbili kukutana na kuzungumza na makundi mbalimbali ya vijana wajasiriamali, na kufungua matawi hayo mawili na kituo cha Thamani ya Utu kilichopo kwenye kituo cha mafuta cha MOIL Sabasaba, Manispaa ya Ilemela jijini hapa.
Sitta, aligusia kidogo suala la katiba, akitaka izibane idara zote za umma na kuwa rafiki wa wananchi, kuliko ilivyo sasa ambapo viongozi wengi wanaonekana kuvimba vichwa wanapokuwa kwenye ofisi zenye viyoyozi.
Akizungumza mara baada ya kufungua tawi la CCM la wapiga debe stendi ya daladala Sahara, Waziri Sitta alisisitiza umuhimu wa viongozi wa idara zote za serikali wakiwemo maofisa uchumi wa kila halmashauri nchini, kushirikiana na vijana kuwawezesha mbinu na maarifa ya kubuni na kusimamia miradi ya kimaendeleo.
Alisema vijana ndio nguzo muhimu sana katika maendeleo ya taifa, hivyo ni lazima suala hilo litiliwe mkazo kwani Tanzania ilipata uhuru wake kwa ajili ya kuwakomboa wananchi wake kutoka kwenye makucha ya wakoloni, ili wajitawale na kupigania maendeleo yao.
“Nikiwa Waziri wa Afrika Mashariki, nimepanga kuhakikisha vijana wa Mwanza ninawaunganisha na vijana wa Kigali Rwanda, Nairobi Kenya, Kampala Uganda na miji mingine ya Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki, ili waweze kujitanua kimaendeleo kupitia miradi yao.
“Kumbukeni hapa Mwanza ndiyo kitovu cha nchi za Maziwa Makuu, kwa hiyo tunahitaji kuona vijana mnajinasua kutoka kwenye lindi la umasikini. Na leo hapa nayakabidhi mashina haya mawili ya CCM niliyoyafungua sh 500,000 kila moja,” alisema Waziri Sitta huku akishangiliwa.
Alisema ziara yake hiyo ililenga kukamilisha ratiba yake ya mwaka 2013 iliyohusu kukutana na kuzungumza na makundi mbalimbali ya wajasiriamali, na kuonya kuwa taifa lolote linalowapuuza vijana lina matatizo makubwa.

CHANZO; TANZANIA DAIMA YA LEO
 
Sitta nilikuwa namtegemea kuwa akipitishwa na magamba ataleta upinzani,ila alivyoendesha bunge la katiba AMESHUKA VIWANGO.
 
UKAWA, ongezeni nguvu, tunataka kila mwanainterahamwe anayekwenda mikoani apokelewe na hoja ya serikali 3, na kukemea uchakachuaji unaofanyika kwenye mkutano mkuu wa ccm almaarufu kama bunge la katiba kwa posho ya uchakachuaji ya laki 3 kwa siku!
 
Nafikiri we jamaa utakuwa unaongoza kwa kutoka povu humu jamvin utaoa povu kila mara tena bora hata ungekuwa una hoja basi!

Achana na huyu ni
~Mwl hasiefundisha anazulula tu
~Kasoma Duce
~Kauza ubunge wake 2010
~Alifukuzwa chama makini
~Sasa ni kipaza saut za wahuni wa karibu na chuo cha A3.
~Nimfasi wa ACT kwa mbali na karibu
~Jinsi yake haifamiki kwan hajawai kugongaaaaa mlango kabisa!

Me waga na mpuuza na yupo hapa kwa kazi maalumu ya kuaribuaribu mada n.k. kwa upuuziupuuzi tuuuuuuuu

Achana naye!!!
 
Si wanabeza maoni ya wananchi wanasema kuwa ni maoni ya Waryoba ngoja waendelee kuvuna wanachokipanda.
 
Hadi sasa najaribu kujiuliza kwa nini Sita alipambana sana kuhakikisha anapata uwenyekiti wa baraza la Katiba lakini sijapata jibu!

Haielekei kabisa kama yuko pale kwa maslahi ya wananchi walio wengi!
 
Lowasa akifanya hivyo mnasema anataka urais na huyu jee?Kinana lini amekua mtanzania?

Kinana ni Tansoma,wazee wake walihamia so yeye ni Mtz kbs kwa vile ni wa hapa,tusibaguane!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mroho wa madaraka,mnafiki anachosema hafanyi hafai huyo mccj
 
Hivi hadi leo Samwel Sitta ametia kibindoni bilioni ngapi tangu awe Mwenyekiti wa Bunge Maalum La Katiba akiongoza vikao vya Interahamwe? Ulafi wa hawa jamaa hakika unatisha! Yaani kulia kote hadi kuanzisha CCJ, alikuwa anatetea tu tumbo lake! Ulafi na unafiki wa watu ndani ya CCM ndio tishio kubwa la amani nchini.
 
Huyu mzee ni mnafiki sana, hao waliomzomea ni wapole sana, huyu alitakiwa kupigwa mawe,hana faida yoyote kwenye jamii.
 
Huyu mzee ni mnafiki sana, hao waliomzomea ni wapole sana, huyu alitakiwa kupigwa mawe,hana faida yoyote kwenye jamii.

Pamoja sana Mkuu, Huyu Mzee ni mnafiki mwenye husda na roho mbaya kuliko muuza baruti! ... Huyu Mzee huwa anaringia kukaa muda mrefu serikalini lakini ukimuuliza amedeliver nini hawezi kukuambia hata siku moja! Muda si mrefu tutatoa ile clip ya yeye kufumaniwa akiwa na mke wa Mjeda wakati ule akiwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa... Namchukia Kwadhaati Maana alikuwa anajua Uongo wote wa Kumgombanisha JK na Edo na alijua mchezo wote aliyokuwa anacheza Joka la Mdimu lakini yeye situ alikaa kimya bali aliubariki na sasa Woga na Aibu haimuishii...
 
Aibu itaendelea kuwaumbua kwa ubaguzi wao wakifikiri nchi hii ni ya ccm pekee. COME BACK TANGANYIKA:israel:
 
Back
Top Bottom