Sitta:Upigaji kura utaanza September 26

Sitta:Upigaji kura utaanza September 26

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,692
Reaction score
164,963
Katika kuonyesha kuwa wamedhamiria kuendelea na mchakato huo wa katiba,mh.Sitta amesema wajumbe wataanza kupiga kura kupitisha ibara za rasimu ya katiba kuanzia tarehe 26 na kwa wale wajumbe watakaokuwa nje ya nchi utaratibu unafanywa kwa kuwasiliana na balozi husika ili kuwawezesha wajumbe hao wapige kura hata kama watakuwa nje ya nchi.Na hapa aliwalenga wanaokwenda kuhiji na walioko India kwa matibabu.

Ninachojiuliza ni je sheria za bunge hilo zinaruhusu upigaji kura wa aina hiyo?Na kama ndio, mabadiliko hayo ya sheria na kanuni hizo yalifanywa lini?
 
Sitta anachezea katiba, yaani katiba ya Tanzania ikapigiwe kura India???

Hii ni zaidi ya dharau kwa watanzania.
 
Uraia pacha ndio umeenza!

Nafikiri hii ni hatua ya majaribio tu.
 
Sitta ni sikio la kufa!!!!!!!! Na mishipa yake ya aibu imekufa!!!!
 
Sitta anastahili kuplmwa akili, kumbe nchi hii ina viongozi wengi ambao wakiwa katika madaraka ya chini wanaonekana makini na waliojaa busara, kumbe kadri wanavyosogelea madaraka makubwa wanadhihirisha uwendawazimu kuliko wa Idd Amin, ahasante Mungu kwa kutuanikia hadharani Sitta halisi na jinsi alivyo na mrengo wa kifashst
 
Anatafuta namna ya kuchakachua ili akidi itimie na 2/3 ipatikane kwa pande zote. Kama inawezekana mjumbe akapiga kura akiwa nje nchi kumbe UKAWA watapelekewa sanduku la kupigia kura wakiwa nje ya Bunge!

Bora wajumbe wote wa BMK waende makwao watapigia kura hukohuko! Kuna ulazima gani ya kubaki ukumbini, waende wakapige kura ya wazi mbele ya walio wachagua.
 
watu wakitaka kujichosha waacheni - sisi tuendelee na yetu!!
 
Maajabu. Haraka yote ya nini, hata walipiga kura na kutoai 'Rasimu' au Katiba inayopendekezwa, kwangu mimi ni kupoteza fedha kwani haitakuja kukamilishwa kama ilivyo. Let us come back to our senses tupumue kwanza na kisha tukienda tutakuwa na mawazo mazuri zaidi; tupate muda wa kuheal.
 
Six anajaribu kutengeneza mnazingira ya kuendelea kuwa m/kiti kwa bunge litaloteuliwa na Rais Eduardo Lowassa come 2016
 
Katika kuonyesha kuwa wamedhamiria kuendelea na mchakato huo wa katiba,mh.Sitta amesema wajumbe wataanza kupiga kura kupitisha ibara za rasimu ya katiba kuanzia tarehe 26 na kwa wale wajumbe watakaokuwa nje ya nchi utaratibu unafanywa kwa kuwasiliana na balozi husika ili kuwawezesha wajumbe hao wapige kura hata kama watakuwa nje ya nchi.Na hapa aliwalenga wanaokwenda kuhiji na walioko India kwa matibabu.

Ninachojiuliza ni je sheria za bunge hilo zinaruhusu upigaji kura wa aina hiyo?Na kama ndio, mabadiliko hayo ya sheria na kanuni hizo yalifanywa lini?

yaani wakati mwingine naifananisha nchi yangu.kama gari lililo kosa dereva linaenda endatu kwa kuendeshwa na madeiwaka. maskini tanzania yangu naikumbuka sana tanzania ya uongozi wa mwalim nyerere. tuliishi kwa matumaini na uzalendo mkubwa chini ya jemedari.sokoine na kumbuka enzizile ilikua ni muujiza kuwa na kadi ya ccm watu tulitamani chama na kuitafuta kadi kwa nguvu zote.kutokana na uzalendo ulioonyeshwa na viongozi hawa mwalim vs sokoine.nakumbuka tuliitana ndugu. maskini leo kila mtu ni kambale? nchi inaenda endatu matamko ya rais haya heshimiwi hata na viongozi wenzake?
 
Katika kuonyesha kuwa wamedhamiria kuendelea na mchakato huo wa katiba,mh.Sitta amesema wajumbe wataanza kupiga kura kupitisha ibara za rasimu ya katiba kuanzia tarehe 26 na kwa wale wajumbe watakaokuwa nje ya nchi utaratibu unafanywa kwa kuwasiliana na balozi husika ili kuwawezesha wajumbe hao wapige kura hata kama watakuwa nje ya nchi.Na hapa aliwalenga wanaokwenda kuhiji na walioko India kwa matibabu.

Ninachojiuliza ni je sheria za bunge hilo zinaruhusu upigaji kura wa aina hiyo?Na kama ndio, mabadiliko hayo ya sheria na kanuni hizo yalifanywa lini?
Kwani kuna Sheria gani iliyounda kile kikundi kinachojiita UKAWA? Pia ni Sheria gani iliyowafanya UKAWA wasusie Bunge Maalum la Katiba?
 
Swali lako laashiria huzijui kanuni za Bunge na sheria zinazodhibiti uhalali wa maamuzi yake. Hukawii kuuliza vipi wajumbe wasiendelee na bunge bila ukomo mpaka katiba ipatikane!
 
Katika kuonyesha kuwa wamedhamiria kuendelea na mchakato huo wa katiba,mh.Sitta amesema wajumbe wataanza kupiga kura kupitisha ibara za rasimu ya katiba kuanzia tarehe 26 na kwa wale wajumbe watakaokuwa nje ya nchi utaratibu unafanywa kwa kuwasiliana na balozi husika ili kuwawezesha wajumbe hao wapige kura hata kama watakuwa nje ya nchi.Na hapa aliwalenga wanaokwenda kuhiji na walioko India kwa matibabu.

Ninachojiuliza ni je sheria za bunge hilo zinaruhusu upigaji kura wa aina hiyo?Na kama ndio, mabadiliko hayo ya sheria na kanuni hizo yalifanywa lini?

Haya sasa Mzee mzima anaweweseka na limechwea.
JK noma na anaelewa michezo ya kisiasa.Mwamemweka sawa mzee wa watu akidhani kapata pakutengenezea CV ya Uraisi 2015 kumbe wenzake wametega na akaingia kingi.

Na ili adhalilike sawa sawa wataacha hili Bunge liishe kifo cha kawaida;siku zitaisha na akidi haitafikiwa na mwisho ni fault ya Kisheria.

Lawama kwa nani kama si Mwenyekiti aliyekosa Busara!
 
Katika kuonyesha kuwa wamedhamiria kuendelea na mchakato huo wa katiba,mh.Sitta amesema wajumbe wataanza kupiga kura kupitisha ibara za rasimu ya katiba kuanzia tarehe 26 na kwa wale wajumbe watakaokuwa nje ya nchi utaratibu unafanywa kwa kuwasiliana na balozi husika ili kuwawezesha wajumbe hao wapige kura hata kama watakuwa nje ya nchi.Na hapa aliwalenga wanaokwenda kuhiji na walioko India kwa matibabu.

Ninachojiuliza ni je sheria za bunge hilo zinaruhusu upigaji kura wa aina hiyo?Na kama ndio, mabadiliko hayo ya sheria na kanuni hizo yalifanywa lini?

Na ijulikane na watu wote kuwa kuna mwendawazimu asiyejua mipaka ya kazi yake. Alianza kukusanya maoni kinyume na sheria sasa anatunga utaratibu wa kupiga kura nje ya bunge. Ama kweli wendawazimu utawatambua kwa matendo yao na wala siyo nafasi yao katika jamii.
 
Back
Top Bottom