Alivyokuwa kwenye mkutano huko kanda ya Ziwa alisikitika sana kuona kwenye rasimu mpya ya katiba imeruhusu serikali tatu naye kwa kukurupuka akasema sasa nini maana ya serikali tatu yaani nchi moja itakuwa na marais watatu?Lol hapa kaniacha hoi kabisa huyu ndio Waziri na aliyekuwa Speaker wa Bunge before.
Kasema kwenye Ilani ya CCm hakuna serikali tatu,kasema sie kama CCM ilani yetu inatambua serikali mbili ambazo ni ya Zanzibar na ile ya Muungano sasa basi kama kweli yeye kama waziri na mtu mzima mwenye akili timamu je hiyo nchi nyingine ambayo iliunganika na Zanzibar na kuform serikali ya Muungano iko wapi?
Bora angesema hii rasimu ni nzuri kwa kuwa sasa hata watoto wadogo watafahamu ni nchi gani ziliunda serikali ya Muungano na sio kusema ati ilani ya Ccm inasema serikali mbili,Binafsi nataka kumwambia Huyu mzee Samuel Sitta kwamba katiba inayokusudiwa sio ya CCM kama yeye anavyofikiria wajua unaweza kumuona mtu mzima kavaa suti na mvi kibao ukasema huyu ana busara lakini kumbe ni kopo yupo yupo tu kwa maslahi yake binafsi.
Katiba si mali ya CCm,Chadema,Liberal Cuf,NCCR na vyama vingine katiba ni ya wote walio na chama na wasio kuwa na vyama,ni ya wazee,watoto,wamama,wadada,wakaka,wagonjwa wa akili,nk.
Tunasema Muungano ulipatikana na nchi mbili ambazo ni Tanganyika na Zanzibar so now what we need ni kuona serikali ya Tanganyika ikirudi so moja kwa moja hata mtu wa kutoka Marekani au Ulaya anafahamu kuna Tanganyika na Zanzibar the waliunganika na kuwa na serikali ya Umoja na kuna mambo ambayo hayahusu Muungano so kila upande unajiamulia nini ufanye lakini likija swala la muungano basi linashughulikiwa na Muungano.We need to see Tanganyika.
Hakuna kulala tutakomaa hadi kieleweke Wazanzibar wenzangu this is the time hakuna kurudi nyuma.