Sitta: Nchi imebaki mifupa

Ingawa binadamu karibia wote ni wanafiki, lakini huyu mzee inawezekana kawapiku wanafiki wenzie wa ccj, hakika anayemuona mzee huyu kuwa anatetea rasilimali na watanzania hakika huyu bado yupo kwenye usingizi wa pono wa kutoweza kupambanua mtu mwema, asiyemwema, na mtu anayejifanya mwema ilihali si mwema
 
 
Mie kwa mtazamo wangu, SS ni mnafiki tu kaona ES anamzidi akaamua kumhujumu kwa 2mia rugu la usispka , sasa bwan sita anatapatapa hana jipy ni vuvuzela 2 la CCJ Hana jipya analo2ambia, yeye ni tatizo cna
 
Wanafiki wa CCJ utawajua tu kwa kauli zao za kujifanya wako against magamba kumbe wanauma na kupulizia
 
Yeye 6 ni sehemu ya matatizo haya,senior kiongozi alikuwa wapi muda wote mpaka nchi imebaki mbavu tu?Si ndio alikuwa anawakaribisha jamaa waje 'watuwekeze' pale TIC majuzi juzi.
 
Huyu mzee ni maiti inayotembea, hata CCM wenyewe tumemshtukia!
Na nyie mnasumbuliwa na unafiki tu, kama amewashinda au mmemstukia kwa nini msimteme??? Tatizo maamuzi yenu yanachukua muda maana yanatoka kwenye makalio.
 
Mnafiki of the highest class!!! Kama si unafiki anashindwa nini kumshauri rais wanapokuwa kwenye BLM, huko kwenye Cabinet ndio angesema kero zake zote. Kwa nafasi aliyo nayo anaweza kuomba kunywa kahawa na mkuu wa kaya na huko akamweleza jinsi anavyoona nchi imebaki mifupa na akatoa maoni na mapendekezo yake ya kuirudishia nchi nyama. Kitendo cha yeye siku zote kuzungumzia matatizo ya serikali yake kama vile yeye si mmoja wapo ni unafiki! kitendo cha kuzungumzia uoza wa serikali yake majukwaani ni udhaifu mkubwa na kudhani watz bado mbumbumbu hawaoni rangi zake. Anakiuka collective responsibilities ambapo ni kielelezo tosha cha mtu mnafiki asiyeweza kuaminiwa na yeyote! Anatafuta umaarufu kwa wananchi na anataka sisi tu sympathize na yeye....apeleke huko huko siasa zake za maji taka!

Atuambie kwanza alivyotumia nafasi yake TIC kujilimbikizia mali na kuingiza wawekezaji fake kama Richmond ambao alikuja kuwageuka?! Aseme ufisadi alioufanya akiwa Spika kwa kujenga ofisi ya Spika Urambo iliyogharimu karibia sh. 500m? kwanini anaishi nyumba ya Masaki ya kupanga kwa mwezi U$ 7,000 ilhali nyumba za serikali zipo? au ni kwa sababu wanagawana nunu kwa nusu na mwenye nyumba? huko si kuitafuna nchi na kuiacha mifupa? Sita aache unafiki!
 
Mbona anawatetea wanyonge wa nchi hii, kwanini kumwita mnafiki?

Si siri kuwa watanzania walio wengi, au watanzania wenye uelewa wa kutosha kuhusu yanayoendelea hapa Tanzania, wameichoka CCM. Hakuna cha zaidi ambacho CCM inaweza ku-offer kwa Tanzania. Ndio maana werevu wanajua kuwa mtaji wa kisiasa wa CCM ni unyonge wa sehemu kubwa ya watanzania, hasa kielimu. Chama kina sera nzuri lakini ukweli ni kwamba sera ziko kwenye ilani tu, hakuna kinachofanyika. Sana sana kinachofanyika ni kinyume na yale yanayosemwa.

Alianza kusema Agustino Lyatonga Mrema, akaonekana kama mwendawazimu, akaja Mtikila akaonekana chizi, akaja Lipumba pia akaonekana hana maana. Sasa ukweli unawekwa wazi kutoka ndani ya CCM, watu wanaanza kumuona Sitta mnafiki. Sitta si mnafiki amefika mahali na yeye amechoka, zamani ndani ya timu minority ndio walikuwa wezi, lakini sasa majority ndio wezi, hicho ndio kinawakasirisha wasafi wachache walio ndani ya CCM.
 
SITTA bana!!! Kinyonga.....

Mbio za 2015, kazi ipo.
 
Mnafiki mkubwa huyu,ahame nyumba ya Spika!
Ofisi ya Spika alojijengea Urambo inatumikaje sasa?
Yeye na mkewe wamenunua nyumba ya serikali wakageuza baa,sasa katika mazingira haya anawatetea wanyonge wepi?
 
tutasikia mengi zaidi subirini tu maana unafiki ndio unawafanya watoane jasho na kushambuliana kwenye majukwaa ya siasa
 
Waziri Stta amenena kweli kwani hata kama ana makosa binafsi akisema lililojema kwa watu sharti apongezwe
 
Katika mambo yanayoendelea sasa hivi ndani na nje ya bunge, ni kielelezo cha wazi kunatatizo katika mfumo mzima wa CCM.
1. Viongozi hawaeshimiani tena,
2. Mwenye fedha anafanya anavyotaka

Hii ni 2011, mpaka ifike 2013 kitaeleweka

Huyu mzee ndie aliyeipotezea ishu ya Richmond: Anafikiri naye kwa kutumia Masaburi. NAchoona CCM watu wote wanadisconnection kwenye vichwa vyao. Tunaongozwa na mataahira. Milembe dizaini.
 
"Inakera kumwona mtu ni waziri lakini inapotokea mikopo ya fedha za maendeleo kwa vijana na yeye anaingiza mkono wake anaweka majina kama 10. Kwa hiyo kama mkopo ni Sh5milioni yeye anazoa Sh50milioni vijana wengine walengwa wanakosa," alisema Sitta.
 
"Mimi ninachoishauri mamlaka husika za dola ni kwamba, iwachukulie hatua kali viongozi watakaobainika kukutwa na fedha nyingi zisizoeleweka na sheria ichukue mkondo wake kwani watu hawa ndiyo wanaifanya nchi na wananchi kwa ujumla kubakia maskini siku hadi siku huku wao wakizidi kufaidika tu," alisema Sitta.
 
"Nchi imebaki mifupa mitupu huku wananchi wake wakiteseka kwa kushindia mlo mmoja na wengine wakiishi kwa kuokota vyakula majalalani, wakati huo baadhi ya watu wachafu wakiwamo viongozi wao wanaendelea kuneemeka bila kujali maisha duni ya mwananchi," alisema mjini hapa katika ufunguzi wa Kongamano Vijana wa Kikristo kutoka nchi za Afrika Mashariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…