Sitta: Dola isitumike dhidi ya Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Dola isitumike dhidi ya Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwele, Mar 9, 2011.

 1. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Someni maoni ya Fr. Mapunda, mimi yamenivutia.

  #1 Ffr. Baptiste Mapund 2011-03-09 03:19
  Serikali ya CCM ijiulize kwa nini Chadema waandamane na kuwashawishi wananchi? Hili swali nikubwa sana, si kwa suala la kuwang'oa wana CCm na seriali yao huo i woga wa kunguru. Naye waziri Mkuu amekosea kabisa kusema kwamba" Rais ni mpole, mpole kwa nani, Rais anachagua ni mpole kwa Mafisadi wanaovuruga amani kwa njia ya kuiba mali ya umma. Lakini rais huyo siyo mpole kwa Wapinzani anaogopa nini? Inashangaza kionmgizi wa ngazi ya juu kuogopa chama cha wapinzani ambao hawana jeshi la polisi, Jw, wala usalama wa taifa. Ila wao wanasera bwana zinazokbalika, wao wanatumia akili na kupanga mambo siyo kukurupuka tu kama wanavyofanya CCM ati kwa sababu ni watawala, hakuna kitu kama hicho, siasa zimegeuka wana CCM, jibuni hoja siyo jazba na vitisho vya nguvu ya dola. Mtamaliza risasi zote lakini watu watakuwepo tu, oneni yanayompakata Gaddafi si ya kurufrahisha, sasa miaka 41 anaharibikiwa kwanini hakuacha alipofika miaka 30 ya utawala wake? Shida kubwa ya viongozi wa Afrika ni kujiamini na "ULevi wa madarka". Mara nyingi naongelea ulevi wa pombe, madawa na ngono, lakini kwa CCM mmelewa madaraka, na hamuoni kama mnaweza kufanya makosa, sasa watu wengi wanamacho mengi kuliko wewe mtu mmoja. Haya yote tunasema si kwa sababu tunaichukia CCM la hasha, mimi si mwanasiasa, nikipenda naweza kuwako kwani waliokuwako wanakitu gani cha pekee? Lakini kazi yangu kama kiongozi wa dini inanipa fursa ya kuiongoza, kuiasa, na kuikemea jamii, na wajibhu huu sijapewa na serikali bali Mwenyezi Mungu. hii ndiyo tofauti kati ya mbunge na mimi> Mimi sijachaguliwa kwa vidole na pengine wizi wa kura, la hasha. Kwa hivi ninyi mnaojisumbua kusema ati"tutoe majoho" kwa taarifa yenu hatutaoa, na badla yake mimi nimeongeza majoho sita kwajili ya kuyatumia wakti nikiwa nahubiri habari njema ya wokovu si ya kifo wala ufisadi, wivu na chuki na uchochesi kama mnavyofikiria wengine na kuwaptotosha wananchi juu ya viongozi wa dinji na hasa kanisa katoliki. Daima nimesema na sasa mtasoma katika kitabu changu kipya "Unabii wa padre Mapunda jijini Dar es salaam Miaka 7' kwamba "Siasa bila dini ni wendawazimu". Tusijidanganye, ukisoma maandiko matakatifu utaona kwamba " Zamani manabii waliishi katika ikulu ya wafaleme, lengo likiwa nji kuwaongoza, kuwakemea pale wanapopotoka na kuwashauri." Lakini leo hii viongozi wetu wa chama na serikali hawataki. Wao wameamua kuwa maadui wa madhehebu ya dini, na hili litawamaliza mpaka kiongozi wa mwisho. Kuwatukana na kuwakejeli viongozi wa dini ati kwa sababu wamekukosoa ni kosa kubwa sana. Inashangaza hata wale viongozi wa serikali na chama ambao wana imani na dini zao wameshindwa kuishauri serikali juu ya umuhimu wa dini katika taifa letu. Tutake tusitake, watanzania wengi wana dini zao, wewe unapowadharau, unazidi kujikaanga kwa maaafuta yako, hii ni siri nawaambia viongozi wa serikali na chama. Wewe kumdharau kiongozi wa dini usijidanganye kwamba ndiyo umefika, kumbe umepotea. Hawa wananchi sisi tunakuwa nao saa mbili tu jumapili lakini hatuwaleti kwa magari, hatufanyi kampeni, wala kuwahonga unga, kanga, chumvi, vitambaa cha kichwani, pombe la hasha, bali wanafika wenyewe kwa hiari yao. Sasa pima hiyo, wewe unapowadanganya huko kwenye kampeni, ujue wanapohitaji amani, faraja, utulivu wanakimbilia kwa viongozi wa dini. kwa hivi usikisema kwamba sisi ni wadini huu ni uwongio mkavu na utawarudia nyie wenyewe. Kama kanisa katoliki lingependa kumipoigia kampeni Dr. Slaa kwanza lingeshindwa? Lingeweza, kuna waumini wangapi katika idara mbali mbali, na mapadre wapo wangapi Tanzania na sisi tulio nje tupio wangapi, je tusingeweza mona hii ni kazi ya dakika tatu tu unamaliza ukiunganisha na elimu tuliyokuwa nayo ya kuwashawishi waumini hii mbona tunageuza nchi dakika tano tu. Kwaq hivi mimi naonya msitu[NENO BAYA]ze kabisa, sisi ni waungwan tumeamua kufuata misingi ya demokrasia ya nchi yetu, kama kuna watu wanafanya kampeni basi ni swala la mtu binafsi lakini siyo msimamo wa kanisa. Na hivi propaganda za mwaka l974 wala hazifai kabisa kwa sabau watz wamebadilika kabisa. Jamani tanznia ni yetu sote, hakuna sababu ya mtu au kiongozxi kujifanya yeye anashika watu na ana watu, hata mimi nina watu je nani hana watu lakini shida ni kwamba unawatumia hawa watu kwa malengo gani? naomba sana viongoxi wa chama na serikali wakati huu muangalie matamsi yenu, si kwa sababu ni viongozi mtaaminika la hasha. Tanzania ya leo n a sasa inahitaji kiberiti tu kuwasha moto katika nyasi kavu, kwa hivi wa kwanza ambao napenda wasikie ushauri wangu ni viongozi wa serikali na chama cha Mapinduzi, najua wengine mtasema Fr,. mapunda anachuki binafsi, laini unajua moyo na mawazo yangu, hii ndiyo shida ya watanzania. Kuikosoa serikali siyo kuwa adui, lakini wrngne tumezoea kusema ukweli, na ukweli unauma kweli kweli, lakini ndiyo dawa. Yesu alisema ' UKWELI UTAWAWEKA HURU" (John 8: 30). naonma kule Mbinga- Ruvuma nyumbani kwetu wananchi bado wamelala usingizi tu, hawana habari wangoja kanga, pombne, vitambaa mwaka 2015, poleni sana akeni ndugu, na wajibikeni kwa maendeleo yenu. Acheni tabia ya kusubiri sewrikali ndiyo kwa maana mnadanganywa kila miaka mitano. Wabunge wa Mbinga mpo? Msihofu na kufadhaika nikiuliza hivyo, ila watu wetu wanapigika kweli na uchakachuaji wa kura katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa halmshauri Mbinga ni kitendawili, je Mwenyekiti wa CCM ametoa jiu kwa wanaMbinga? Walikuwa wanamngojea huko mwezi desemba baaday ya mwananchi mwenye mapenzi mema kupeleka ripoti kwa Mkurugenzi wa Takukuru, Rais na vyombo vingine, ningependa kusikia suala hilolimeshughul ikiwa vipi? Jamani msishangae mtu kwao, mbona methali hii inafahamika sana, tunatka maendeleo ya bra bara Songea- Mbambayay, shule zenye walimu bora, kahawa yetu itusaidie inakufa, na maendeleo katika nyanja zingine. Watanzania amkeni usingizini. naipenda nchi yangu Tanzania ndiyo kwa maana inaniuma sana kuona inayumba.

  Nawasilisha!!!
   
 2. m

  mtimbwafs Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuko pamoja Fr. Mapunda kwa hili ulilolisema hapo juu na kwa kuwaasa viongozi wa serikali na chama chao waacha uchochezi kwa kuwa sisi Watanzania wa sasa tunajua ni nini tunachofanya na tunachotaka. Kwa kweli tumechoka kudanganywa kila baada ya miaka mitano na maendeleo hatuyaoni.

  CHADEMA kinaonyesha njia sahihi ya kupita na kazi ya ccm imekuwa ni kuvikandamiza vyama vya upinzani ili wao watawale milele lakini CDM ni chama imara kilichojipanga sawasawa hivyo hakitachakachuliwa kirahisi kwa propaganda za kitoto namna hii.

  HAKI KWANZA WAJIBU BAADAE.
   
Loading...