Sitta arejea Nec kwa kishindo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta arejea Nec kwa kishindo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Apr 16, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Sitta arejea Nec kwa kishindo Send to a friend Saturday, 16 April 2011 08:41

  Mwandishi Wetu, Dodoma
  NYOTA ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, imeendelea kung’ara baada ya wabunge wa CCM kumchagua kwa kura 104 awawakilishe kwenye Halmashauri Kuu ya chama hicho (Nec).

  Kwa wadhifa aliokuwa nao wa Spika wa Bunge, Sitta alikuwa Mjumbe wa Nec na Kamati Kuu ya CCM lakini aliondoka baada ya chama hicho kumwengua kuwania tena nafasi hiyo.

  Katika uchaguzi huo, baadhi ya wagombea walikuwa wanawatumia wabunge wenzao kuwafanyia kampeni, huku wengine wakikodi wapigadebe kutoka Dar es Salaam. Katiba ya CCM inaruhusu wabunge wa chama hicho kuwachagua wajumbe 10 kuingia Nec kutoka miongoni mwao.

  Mbali na Sitta, wabunge wangine walioshinda ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, , Nimrod Mkono (Musoma Vijijini), , Abbas Mtemvu (Temeke) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Hawa Ghasia.

  Wengine waliochaguliwa ni Wabunge wa Viti Maalumu, Angela Kairuki, Munde Tambwe na Faida Mohamed Bakari, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba.

  Wabunge walioanguka katika uchaguzi huo ni Brigedia Jenerali Mstaafu, Hassan Ngwilizi (Mlalo), Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Dk Athman Mfutakamba, , Dk Charles Tizeba (Buchosa), Christopher Ole Sendeka (Simanjiro).

  Wengine ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, , Dk Faustine Ndungulile (Kigamboni), , Ahmed Salum Ali (Solwa), , Yahya Kassim Issa (Chwaka), Mwanahamisi Kassim Saidi (Viti Maalumu), Martha Mlata (Viti Maalumu) na Saidi Mussa Zubeir (Fuoni).

  Wagombea waliojitoa kabla ya kura kupigwa ni Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, Dk Hamis Kigwangallah (Nzega), Lediana Mg’ong’o (Viti Maalumu), Naibu Spika, Job Ndugai na Mbunge wa Uzini, Muhammed Seif Khatib.

  Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM ni Jenister Mhagama nafasi ambayo inamuingiza moja kwa moja kwenye Kamati Kuu ya CCM. Bunge lililopita, nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Ali Ameir Mohamed, ambaye alistaafu na hakuwania ubunge. Mwenyekiti wa kamati hiyo ya wabunge wa CCM ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Comments
  0 #8 eston 2011-04-16 17:54 hongera sitta ila jaribu kuwa makini na vitu wanavyokutuma kama walivyofanya muswada wa katiba zanzibar ni aibu
  Quote

  0 #7 Mr suggestion 2011-04-16 17:28 Hongera Sitta but next time kataa kwenda kwenye mswada wa katiba kabla hujausoma vizuri na kuuelewa coz kitendo cha jamaa kuuchana mbele yako mswada hule ni dhahili kwamba ulikuwa haufai conguraturation home boy
  Quote

  0 #6 Gamba Beshubeo 2011-04-16 17:22 Sitta endelea na mapambano. Chema chajiuza.
  Quote

  +1 #5 Grace 2011-04-16 16:38 CCM kama mnasoma maoni haya, oneni watu wanaopendwa na wananchi na wapeni nafasi za kukiongoza chama. Vinginevyo mtabaki na labda...!!!
  Quote

  +3 #4 Jabir 2011-04-16 13:51 Sitaaaa,saafi sana ila sisiem si mahala saf kwako,lakin hongera sana
  Quote

  +8 #3 vuvulzela 2011-04-16 13:26 Mh Sita kuwa makini sana, Serikali ya CCM inataka kukuchafua katika kutetea muswada mbovu wa katiba kule Unguja.
  Mh Sita walikuletea zengwe sasa inawaghalimu maana Makinda sio tuu anapwaya bali hafai kabisa ktk Uspika wa Bunge
  Quote

  +5 #2 josh 2011-04-16 13:18 hongera mhe. Sitta
  pamoja na njama za mafisadi kukusambaratish a kisiasa lakini wamefeli
  endeleza kupambana na mafisadi walioko ccm ambao ndio chanzo cha matatizo chungu mbovu ktk nchi yetu na kutusababishia umaskini unaoendelea kushamiri ndani ya nchi yetu. Mungu azidi kuwa nawe sisi wananchi wenye uchungu na nchi hii tuko pamoja nawe kama samaki na maji. big up again
  Quote

  +5 #1 Mkide J. Mkafrend 2011-04-16 10:57 HEKO! HEKO SITTA,

  NYOTA NJEMA NA INAYONG'ARA HAIZIMWI KWA MAWINGU YA KIANGAZI!

  SASA NI WAKATI WA KULONGA.
  Quote  Refresh comments list
   
Loading...