Sitta amvutia pumzi Mgeja.................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta amvutia pumzi Mgeja....................

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 27, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Mwananchi linatutaarifu ya kuwa Spika Mstaafu Mheshimiwa Samweli Sitta anamvutia pumzi kada wa CCM Bw. John Mgeja ambaye ameahidi kwenda kwenye NEC ya CCM na kujenga hoja binafsi ya kumvua uanachama Mzee wetu Sitta kwa matamshi yake ya kuhoji maamuzi ya vikao vya CCM hususani Kamati Kuu ya CCM ambayo yalimnyima nafasi ya kuugombea tena Uspika........kwa madai yaliyoshamiri ubaguzi wa kijinsia kuwa sasa ni nafasi ya akina mama..............................


  Sitta amvutia pumzi Mgeja Monday, 27 December 2010 08:50

  Sadick Mtulya na Boniface Meena


  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema amasubiri kwa hamu hoja binafsi iliyoahidiwa kuwasilishwa Halmashauri Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja,.
  Alhamisi iliyopita, Mgeja alimtuhumu Sitta kuwa anaendeleza mgawanyiko ndani ya CCM na kumtaka afute kauli yake kuwa aliondolewa uspika kwa mizengwe, la sivyo atawasilisha hoja binafsi Nec kumtaka athibitishe. 
"Sitta anapaswa kufuta kauli yake kuwa, aliondolewa kwa hila…kikao kilichofanya uamuzi kuhusu nafasi ya uspika ni Kamati Kuu ya CCM. Kwa hiyo anamaanisha wajumbe wa kikao hicho wana hila naye.
  Kusema hivyo kutasababisha baadhi ya wanachama kukosa imani na kikao hicho," alisema Mgeja. 
Akizungumza na gazeti hili juzi, Sitta alisema ingawa hajapata taarifa rasmi kuhusu hoja za Mgeja, anaisubiri kwa hamu.
  "Siwezi kuzungumzia kwa kina taarifa ya Mgeja kwa kuwa sijaipata vizuri, lakini ninaisubiri kwa hamu hoja yake hiyo,'' alisema Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa.
  Wakati Sitta akisita kujibu hoja ya Mgeja, Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango, amemshangaa Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Shinyanga, akisema alichosema hakiwezekani.
  Pia, Kilango alipuuza msimamo wa Mgeja akisema hauna mashiko: "Hoja binafsi zinapelekwa bungeni tu, sio kwenye vikao vya chama. Vikaoni zinaletwa ajenda, sasa huoni haya ni maajabu?"
  "Huyu mwenyekiti asituvuruge, tunatakiwa kujua chama kinaelekea wapi na tumefikaje hapa," alisema Kilango na kueleza kuwa anaamini Mgeja katumwa, huku akiongeza:
  "Ni bora pia atwambie (Mgeja) ametumwa na nani kwa kuwa anachozungumza ni kudanganya umma."
  Kilango ambaye alikuwa akizungumza kwenye mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana, alisema anamshangaa mwenyekiti huyo kumwandama Sitta, badala ya kutafakari jinsi alivyopoteza majimbo manne ya ubunge mkoani Shinyanga.
  "Huyu anataka tumkate panya mkia halafu aendelee kuishi badala ya kumkata kichwa ili kumaliza tatizo," alisema Kilango akimaanisha kuwa Mgeja anataka kukwepa hoja ya msingi kwa kuanza kuzungumzia mambo yasiyomhusu.
  "Namsihi Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, asikubali kuwa na viongozi ndani ya chama ambao wanataka kumkata panya mkia badala ya kumkata shingo ili afe," alisema Kilango.
  Alisema hivi sasa CCM inatakiwa kuokoa chama kwa kufanya tathmini kujua chanzo cha wananchi kuwakataa, lakini sio kuzungumzia mambo yasiyo na msingi.
  Desemba 19, mwaka huu, Sitta alitoa kauli nyingine inayoweza kutikisa CCM baada ya kueleza kuwa, aliondolewa kwenye kinyang'anyiro cha Spika wa Bunge kutokana na hila za viongozi, ambao walishindwa kuhimili kasi ya utendaji wake kwenye chombo cha kutunga sheria.
  Mbunge huyo wa Urambo Mashariki, alijikuta akianguka kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya CCM kwa kile kilichoelezwa kuwapa wanawake nafasi ya kuongoza moja ya mihimili ya nchi.
   
 2. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni walewale 2wrongs does not make one ok!
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Kwa busara za 6....nashaurii aachane na Mgeja....namuona anajipendekeza anataka kutumia weakness za JK na Makamba ya kuogopana....ili yeye aonekana anayaweza....si kwelii angetuliaa aimarishe chama azibe ufa na mashimo shy alipokimbizwa na wapinzani uchaguzii.....mambo ya 6 hayawezii .....
   
 4. semango

  semango JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  wanajuana hao
   
 5. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Wacha mwamalizane kwanza wenyewe kwa wenyewe, halafu sisi kazi yetu itakuwa kama kumsukuma mlevi vile, na safari hii kuna kazi CCM makundi ya TZ bara ni mengi yanayotaka kumtoa raisi, zenji nako wanataka kumtoa pia.
   
 6. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,654
  Trophy Points: 280
  Kumbe ana ya kujibu kwenye chama kwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa CCM Shinyanga na amepoteza majimbo Manne(4) anatakiwa akieleze chama ni kwa nini kapoteza, sasa anataka kupindisha mada kwa kudandia hoja isiyomuhusu.
   
 7. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Hamis Mgela ni wa Kupuuuuuza tu,

  Hana Lolote anabeba beba wageni, Mkoa umedumaa kwa sababu ya siasa zisizo na Tija na Mkoa.

  Kama mna Akili Fukuzeni Mgeja,

  Ni Kimeo kilichoshindwa hata DArasa la SAba
   
Loading...