kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
Kaka Sitta ongeza spidi, kidogo kidogo utakuwa hero wa taifa hili.
Kuna tatizo la kiutandeaji katika baraza la mawaziri wa Kikwete. Kuna wengine hawana lengo la kufanya kazi kama timu bali wanahangaikia umaarufu. Wengi katika mawaziri hao, wamekuwa wakiongea mno na vyombo vya habari. Huyu bwana kama haamini kile wanachokifanya wenzie na njia yake ya kukosoa ni kupitia vyombo vya habari, basi ni vyema angeamua kukaa pembeni na kuwa Mbunge wa kawaida nadhani angeheshimika zaidi.KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Waziri katika Baraza la Mawaziri ameamua kumkosoa mwenzake hadharani kutokana na uamuzi alioutangaza hivi karibuni kwa Taifa.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ndiye amepata ujasiri huo kwa kumkosoa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kutokana na kutangaza kuilipa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Sh bilioni 94, hatua ambayo anaona hakustahili
kuitangaza yeye.
Sitta alisema hayo jana, baada ya kumaliza kuongoza mahafali ya Shule ya Sekondari ya Dini ya Maranatha iliyoko Mianzini Kata ya Kaloleni jijini hapa.
Alisisitiza kuwa Dowans ni ya wajanja waliocheza ujanja kwenye karatasi na Serikali kuingia
‘mkenge' kulipa kitu ambacho alikielezea kuwa hakina sababu za msingi.
Waziri huyo alisema Kampuni ya Richmond iligundulika na Kamati ya Uchunguzi ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, kuwa haikuwa halali lakini inasikitisha kuona na kusikia mbia wake, Dowans amehalalishwa, "kitu hicho ni hatari sana kufanywa na jamii itakuja kutuhukumu kwa hilo.
''Mzabuni feki anacheza karata zake na mbia wake Dowans nasi tudiriki kulipa kitu ambacho si halali … kamwe haiwezi kuwa halali katika maisha yote," alisema.
Sitta alitoa mfano wa mtu ambaye hakumtaja jina, kuwa ana kampuni 17 nchini, lakini jina lake halionekani katika kampuni yoyote na ambaye alidai anacheza michezo michafu na kulipwa mamilioni ya fedha.
Alisema watu hao wapo na wanacheza na karatasi na kuhalalisha kujipatia mamilioni ya fedha za walipa kodi wa nchi hii.
Pia Waziri alisikitishwa na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya ‘kunawa mikono' mapema na kukubali kuilipa Dowans, hatua ambayo alisema ilimshitua sana.
Alisema kwa jambo zito kama hilo, ni lazima Serikali ingekaa chini na kuliangalia kwa mapana na hata ingewezekana kuitisha kikao cha Baraza la Mawaziri kujadili suala hilo kwa kina na kulipatia ufumbuzi wa pamoja, lakini Waziri Ngeleja amelisema haraka jambo hilo.
Sitta alisema Sh bilioni 94 zingejenga barabara ya lami ya kilometa 100 yenye ubora wa hali ya juu vilevile kwa kujenga shule za sekondari 300 za kidato cha kwanza hadi cha nne.
''Naweza kusema wajanja wametuzidi akili na wamefaidi kodi za wananchi kujilipa, lakini elimu bila maadili nchi inaweza kwenda mrama,'' alisema.
Waziri Sitta alisema kwa sasa huwezi kufanya lolote juu ya malipo ya Dowans kwani ''unawezaje kufunga zizi la ng'ombe wakati ng'ombe wote wameshaondoka?''
Alisema ataendelea kusema ukweli mwanzo hadi mwisho bila kumwogopa mtu na kamwe hawezi kuwa mwongo na mnafiki kwa jambo lolote.
Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC) iliamua katika hukumu yake Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) iilipe Dowans fidia ya Sh bilioni 94 kutokana na Tanesco kuvunja mkataba nayo.
Uamuzi huo uliridhiwa na Serikali baada ya Mwanasheria wake Mkuu, Frederick Werema kuipitia hukumu hiyo na kujiridhisha kuwa ni halali.
Kaka Sitta ongeza spidi, kidogo kidogo utakuwa hero wa taifa hili.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Waziri katika Baraza la Mawaziri ameamua kumkosoa mwenzake hadharani kutokana na uamuzi alioutangaza hivi karibuni kwa Taifa.

Kuna tatizo la kiutandeaji katika baraza la mawaziri wa Kikwete. Kuna wengine hawana lengo la kufanya kazi kama timu bali wanahangaikia umaarufu. Wengi katika mawaziri hao, wamekuwa wakiongea mno na vyombo vya habari. Huyu bwana kama haamini kile wanachokifanya wenzie na njia yake ya kukosoa ni kupitia vyombo vya habari, basi ni vyema angeamua kukaa pembeni na kuwa Mbunge wa kawaida nadhani angeheshimika zaidi.
Sita, heshima yako itapanda kama utasema:
1. Wamiliki wa Dowans ni (a)......, (b)......, (c).........
2. Mwenye kampuni 17, na akiwa ametumia majina tofauti tofauti ni..................................
mzee umenena!Tatizo hapa ni ushahidi wa hao wamiliki wa makampuni 17 ambao majina yao hayaonekani anywhere! Hapa ndio IGP Mwema alitakiwa kutupa taarifa za kiintelijensia kuliko kukimbilia kuua watu ovyo wasio na hatia!
Hakuna hukumu hapo juu mali ni mawazo. Well nani alimuuliza kwamba baraza la mawaziri limesema? Yeye Sitta naye ni Serikali. Kama haiamini Serikali kwanini asikae pembeni abaki kuwa muhimili mwingine peke yake? Kwani yeye ndiye msemaji wa Baraza la Mawaziri juu ya agenda zake? Kama hawaamini wenzie na kuhakikisha kuwa wanaonekana wa hovyo, anasababu gani ya kufanya nao kazi? Huyu bwana amekuwa na hasira zaidi baada ya kuukosa Uspika. Angeweza kufanya vyema katika wizara aliyopo na akaheshimika zaidi. Aangalie mifano ya kina Magufuli hata leo hii ukianzisha wizara ya kuchimba mitaro ukampa magufuli, utajua kule kuna mtu anafanya kazi. Sio yeye ambaye amejiegeuza msemaji wa kila kitu. Ni bora kuchagua kuwa mbunge au kukaa pembeni kabisa na kwenda kwenye chama kingine. Kwa kumalizia ni vyema nikamtolea mfano Mbunge Zitto. Yeye amekuwa akipingana na wenzie katika chama, na hapa jamii forum wengi saana wamekuwa wakimuhukum. Kuna tofauti ipi na Sitta?Sasa kama Baraza la Mawaziri halijaitishwa angeenda kusemea wapi? Hukumuni kwa haki sio kwa jazba na makengeza ya akili!
Sita, heshima yako itapanda kama utasema:
1. Wamiliki wa Dowans ni (a)......, (b)......, (c).........
2. Mwenye kampuni 17, na akiwa ametumia majina tofauti tofauti ni..................................
Hakuna hukumu hapo juu mali ni mawazo. Well nani alimuuliza kwamba baraza la mawaziri limesema? Yeye Sitta naye ni Serikali. Kama haiamini Serikali kwanini asikae pembeni abaki kuwa muhimili mwingine peke yake? Kwani yeye ndiye msemaji wa Baraza la Mawaziri juu ya agenda zake? Kama hawaamini wenzie na kuhakikisha kuwa wanaonekana wa hovyo, anasababu gani ya kufanya nao kazi? Huyu bwana amekuwa na hasira zaidi baada ya kuukosa Uspika. Angeweza kufanya vyema katika wizara aliyopo na akaheshimika zaidi. Aangalie mifano ya kina Magufuli hata leo hii ukianzisha wizara ya kuchimba mitaro ukampa magufuli, utajua kule kuna mtu anafanya kazi. Sio yeye ambaye amejiegeuza msemaji wa kila kitu. Ni bora kuchagua kuwa mbunge au kukaa pembeni kabisa na kwenda kwenye chama kingine. Kwa kumalizia ni vyema nikamtolea mfano Mbunge Zitto. Yeye amekuwa akipingana na wenzie katika chama, na hapa jamii forum wengi saana wamekuwa wakimuhukum. Kuna tofauti ipi na Sitta?
Kwanza la Kombani na la Sitta linautofauti mkubwa hasa! Kombani na mwenzake Werema walikuwa wanaongelea ishu zilizo chini ya mamlaka yao na si za waziri mwingine. Pia hawa watu wawili hawakuhusisha matamshi yao na baraza la mawaziri. Tatu two wrongs........Sasa kama mwenye nchi amekaa kimya kama kamwagiwa maji ya baridi kuhusu malipo haramu ya DOWANS watu wakae kimya? Huu utaratibu wa kuongea kila mtu kivyake katika Serikali ya JK ni wa kawaida kabisa! Kombani kadai Serikali haina fedha kugharamia mchakato wa Katiba mpya, AG akadai kuwa Katiba mpya "hapana" ila viraka "yes!" JK akaja mwishoni kudai kuwa ataanzisha mchakato wa Katiba mpya, sijui sasa atatoa wapi fedha! Sasa sioni kwa nini unashangaa nini kuhusu mzee wa watu Sita kukemea uporaji huu wa mchana kweupe? Au mwenzetu umeahidiwa mgao?