Fundi Mchundo,
Hapa kuna kitu kimoja kinalalamikiwa na kwa kweli nimesoma maelezo ya walio upande wa Spika na walio upande wa Jaji hiki hata mimi kinanichanganya. Hili linahusu hili swala la EWURA. EWURA wamekamata vituo vya mafuta ambavyo vinauza mafuta machafu. Kisheria walizopewa, ni kuwa wanaruhusiwa kuvifungia. Ni sawa na bwana Afya akikuta mtu anahoteli chafu basi anaruhusiwa kuifungia palepale na si kuipeleka mahakamani. Polisi akikuta wewe mhalifu basi anakubeba palepale na si kwenda mahakamani kuomba ruhusa. Sasa Mahakama inapokuja na kusema "vituo vya mafuta endeleeni kuuza mafuta machafu..." hapa hata mie nashindwa kuelewa. Walipokamata bidhaa mbovu za China, walizibeba palepale na baadaye zikachomwa moto. Sasa wenye mali wangelienda mahakamani na kudai warudishiwe mali zao na waendelee kuziuza, na mahakama inakubali hivyo, mie hapa ndipo nachanganyikiwa.
Ila kuna hilo umeandika hapo juu kuhusu mtu kugombea na wanamkatalia kwa gia hajatoka chama cha upinzani. Kwa kweli katika haki za binadamu, hii imekaa ovyo ka maana nyingine Mahakama inatumia uwezo wake KUVUNJA KATIBA BOVU linalotumika hadi leo Tanzania. Hili hata mie niko nao kwa sana. Ila nafikiri Mahakama ilitakiwa kuwatolea UVIVU wabunge na Serikali kwa kuendeleza katiba iliyozeeka na imepitwa na wakati.
Ni sahihi kabisa Mkuu FM. Kipengele kinachozua mgombea kushiriki uchaguzi kama kibinafsi, kinamnyima mwananchi haki ya msingi. Ila tujue kuwa kipengele hicho kipo na ni sehemu ya Katiba hiyo hiyo. Kipengele kinachoruhusu mtu yeyote kuchaguliwa kikiungana na kipengele kinachotaka mtu huyo awe ametoka katika chama fulani cha siasa chenye usajili wa kisheria, kinafanya vipengele vyote viwe sahihi na kamilifu. Ila, usawa wa wananchi wote kuchaguliwa bila mipaka unapungua kwa kipengele hicho cha pili (mgombea kutoka chama cha siasa).
Katiba ndio sheria kuu kuliko zote hapa nchini. Mahakama, Bunge, Serikali, Taasisi zote na hata wananchi wa kawaida wanatakiwa kuishi Tanzania kikatiba. Hivyo hakuna chombo chochote kilicho juu ya Katiba. Kumbuka, kuna sheria fulani fulani ambazo hutungwa/hurekebishwa na mahakama. Ila sheria hizo zinatakiwa zitungwe/zirekebishwe kwa kuzingatia Katiba ya nchi (Hii ndio sababu Jaji Mkuu wa JMT hana mamlaka katika mahakama za Zanzibar. Kwakuwa wao pia wana Katiba yao).
Endapo itathibitika kuwa sheria zilizotungwa/kurekebishwa na mahakama zinapingana na Katiba, sheria hizo huwa batili mara moja. Mahakama kote duniani (ambapo Katiba hueshimiwa), hufanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba. Katiba ndio iliyounda Mahakama, hivyo ni lazima Mahakama pia ziheshimu Katiba.
............Sasa serikali ikimcharukia jaji mkuu ikisema uamuzi huo wa mahakama uliotolewa na huyo jaji wa kuruhusu wagombea binafsi ulikuwa wa ajabu ajabu kwa kuwa ulikiuka katiba inayotaka watu wagombee kupitia vyama itakuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama?.........
Hapa tunatofautiana. Pale ambapo Katiba inajichanganya ni wajibu wa Mahakama kutoa TAFSIRI ya kipi kina uzito zaidi. Tofauti na tunavyofikiri, Katiba sio sacrosant. Inarekebishika pale inapoonekana ina mapungufu. Mahakama kwa kusema walichosema imeweka wazi hiyo contradiction ili wahusika wairekebishe!
Amandla.......
Wwanaompinga sita ni walarushwa.mahakama zetu hadi mahakama kuu rushwa tupu ndio maana ukihoji kidogo kuhusu hukumu fulani mahakama zinachachamaa eti kuingilia uhuru wa mahakama.kunahaja kuwepo na chombo cha kudhibiti mahakama zet hasa za nchi za kiafrika ambapo mahakimu na majaji njaa tupuKatika Mahakama zetu kuna rushwa za kutisha na ni vyema Bunge likajadili mambo haya ili umma uweze kutambua mapungufu katika waangalizi wa sheria.
Mahakimu , Majai na hata wafanyakazi wa Mahakama wamejiteua kuwa miungu watu, na hata pale ambapo kesi zimeamuliwa bado kupata nakala za hukumu ni shida sana na ni kwa rushwa.Mifano hai ipo.
Wale wasio penda suala hili lijadiliwe wanawalakini katika kuelewa mtiririko wa utekelezaji wa sheria.
Hivyo basi nampongeza sana Spika kwa Ujasiri wa kumshika mbogo huyu wa sheria kwa mapembe yake, tukumbuke Spika Sitta ni mwanasheria.