Lakini cha kushangaza, ni hatua ya leo ya Spika Sitta kuamua kujibu mapigo bungeni kwa kutetea masuala ambayo yanaonyesha dhahiri kuwa Bunge linataka lisikosolewe. Sisi tungefarijika sana kuona Spika Sitta anakubali ushauri wa Jaji Mkuu wa kukutana kwa wakuu wa mihimili hiyo mitatu na kuzungumza kuona kama kuna tofauti na jinsi ya kuzitatua, lakini siyo kwa kuendeleza malumbano.
malumbano baina ya taasisi hizi kuu tatu ni muhimu ili kuweza kuweka accountability bora zaidi.
Naamini Samwel Sitta as a good lawyer knows whta he is doing.
Am just looking forward to hearing what they have to say!
Katika hii mihimili mitatu, "unaoongoza kwa ufisadi na watendaji wake kuona mali za wananchi hazina mwenyewe na kuzifuja kama mchwa" ni Serikali(Executive branch), "unaoongoza kwa Rushwa za kubaka haki za raia" ni Mahakama na "Unaoongoza kwa uzembe na ubendera fuata upepo bora liende sisi tupate posho" ni Bunge
Sasa hapa ni kwamba mihimili yote au system nzima ni uozo yaani mfu hawezi kulala tanga la mfu mwenzake.
- Very sad, yaani haya ni maoni ya mhariri wa gazeti maarufu sana kwa taifa, masikini ya Mungu haelewi kwamba ili kupata demokrasia ya kweli kinachotakwia ni malumbano kati ya hivi vyombo vitatu vikuu vya taifa, yaaani Executive, Judicial, na Parliament.- Kwamba ni katika kulumbana kwa vyombo hivi vitatu kisheria ndio unapata ukweli wa kisheria ambao unatakiwa kuongoza siasa ya taifa, masikini jaji mkuu wala hajui power aliyonayo kisheria, kwamba anatakiwa kusubiri mashitaka dhidi ya serikali na kuifundisha adabu kisheria, hajui kuwa bunge likikosa anatakiwa kulisubiri kwenye sheria na kulipa aadhabu kisheria,
- Matokeo yake ndio haya, Jaji Mkuu badala ya kulumbana rasmi kisheria, yeye anaenda kulalamikia kwenye sherehe, badala ya kuwatuma wanasheria wake kuishitaki bunge kwa kuingilia kesi ya Mengi Vs Malima, yeye anakwenda kulia kwa wananchi wasioelewa hata anachosema ni nini kisheria, na kwa bahati mbaya sana ya kutokuelewa kinachotakiwa baadhi yetu tunamuona huyu jaji kuwa ni shujaaa, na Spika naye knowing kwamba huyu Jaji ni nothing but a coward naye anaigeuza ishu ya kisheria kua politics kwa makusudi mazima, na masikini media yetu na sisi wananchi masikini wa habari muhimu za taifa letu, tunakubali na ku-take sides hata bila kuuliza exactly kinachosemwa ni nini?
Mungu Aibariki Tanzania.
Malumbano ya Mahakama, Bunge ya nini?
Mhariri
Daily News; Monday,February 09, 2009 @19:58
Leo, Spika wa Bunge Samuel Sitta aliamua kuanzisha mjadala ambao kwetu sisi tunauona hauna maslahi, tija wala manufaa kwa Watanzania ambao kuna mambo mengi ya msingi ambayo si Bunge tu, bali viongozi wanapaswa kuyafanyia kazi.
Spika Sitta aliamua kujibu, tena kwa maneno ya kejeli ya ‘Potelea mbali', hatua ya mhimili mwingine wa Dola, Mahakama, kulalamikia hatua ya mhimili huo wa Bunge unaoongozwa na Sitta, kuingilia kazi za Mahakama.
"Hapa watasema pia naingilia mahakama…potelea mbali," alisema Sitta bungeni Dodoma leo. Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Bunge, tamko la Bunge litatolewa leo baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Hapa Mh. Spika tayari amekwisha pre-empty tamko la bunge, maana amelisemea msimamo bunge kabla halijatoa tamko, kazi ipo!
Mimi nadhani alieanzisha malumbano ni Jaji Mkuu. Yeye kama alitaka kukutana kwa mihimili hiyo mitatu kujadili utendaji na mipaka ya kazi zao, angefanya hivyo kwa kuzingatia kanuni na taratibu za kiutendaji ambazo zipo bayana. Hakuwa na haja ya kutangazia umma kupitia kwenye sherehe yao ya siku ya Sheria. Spika Sitta alichofanya ni kuelezea anavyoona mambo yakitendeka katika maamuzi ya Mahakama na kutoa maoni kuwa hali hiyo sio sawa. Spika angedharau suala hilo na kuliachia lielee kama baadhi ya wachangiaji hapa wanavyotaka, asingekuwa tu anadhalilisha chombo hicho cha utungeji wa sheria anachokiongoza, bali pia angekuwa ameshindwa kukitetea, kukilinda na kukiongoza.
Wakuu, Katiba ya nchi hairuhusu kauli yoyote ya Mbunge (iliyotolewa Bungeni) kufunguliwa mashitaka mahakamani. Kwahiyo sulala la Mahakama kuishitaki Bunge haipo.
Mahakama ndicho chombo pekee katika mihimili hii mitatu ambacho hakina control yoyote. Hakuna mahali katika Katiba yetu inapoelezea hatua zozote zinazoweza kuchukuliwa endapo Mahakama itakosea, kama Taasisi. Hivyo nadhani ni jukumu la Bunge ambalo hutunga sheria zitumikazo mahakamani kutetea sheria hizo. Endapo Bunge halitafanya hivyo, ni dhahiri kuwa wananchi wataendelea kununua haki kila wakati. Mahakama ni chombo muhimu sana. Hakiwezi kuachiwa kutenda bila mtu yeyote kuelezea maoni yake, au kukikosoa. Utaratibu huo ndio unaofifisha haki hapa nchini. Bila control, hakuna system inayoweza kufanya kazi.
Bunge pia, inabidi kutenda haki kwa Serikali na Mahakama. Serikali na Bunge vinatakiwa kuzingatia mipaka yao kiutendaji ili kuepusha muingiliano usio wa lazima. Hatua inayoendelea sasa, ni matokeo ya kushindwa kuvumiliana yaliyoanza muda mrefu sana. Sasa umefika wakati wa kusema yote kwa manufaa ya Taifa letu.
Kama Bunge lisiposema, nani atakaesema? Walau wao wana kinga wanapokuwa ndani ya BUNGE.