Sitta alivyowadanganya watanzania

Sitta alivyowadanganya watanzania

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,016
Katiba iliyokabidhiwa kwa rais ina utata
Kilio cha Katiba Mpya sasa kuanza upya

SHEREHE ZA kumkabidhi Rais "Katiba Inayopendekezwa" zimeingia dosari kutokana na kasoro nyingi, ikiwemo ya kutopatikana kwa theluthi mbili za wajumbe kutoka Zanzibar, MAWIO limeelezwa.

Katika mfululizo wa vitimbi vilivyoleta kasoro

Mjumbe mmoja wa Bunge Maalum la Katiba ambaye anatoka Zanzibar, amefanywa kuwa mjumbe wa Tanzania Bara.

Wajumbe waliokuwa nje ya nchi, inaonyesha wanadaiwa kupiga kura kabla ya siku yenyewe.
Wajumbe waliokataa vipengele kadhaa katika andiko la mwisho la Katiba inayopendekezwa, wamechukuliwa kuwa wamekubali mapendekezo.

Wajumbe waliokuwa Hijja Makkah, nchini Saudi Arabia na mmoja aliyeko nchini India, wanadaiwa kupiga kura tarehe 28 Septemba 2014 wakati siku ya upigaji kura kwa Katiba inayopendekezwa, ilikuwa 29 na 30 Septemba.

Wajumbe wote walioko nje, wanaonekana kupiga kura kwa ibara zote na siyo kwa utaratibu wa uliotumika Dodoma.

Tarehe 28 Septemba, 2014 ambayo ni siku wajumbe waliokuwa nchini Saudi Arabia wanadaiwa kupiga kura, ilikuwa Jumapili.

Taarifa kutoka nchini Saudi Arabia zinasema Ubalozi wa Tanzania nchini humo, ambao ulitajwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Samwel Sitta kuwa ungesimamia zoezi zima la upigaji kura kwa wajumbe waliokuwa huko kwa ibada ya Hijja, ulijivua mapema jukumu hilo.

Barua kutoka ubalozini inasema: "kwa hivyo, kwa mazingira ya Ibada ya Hijja huko Makkah na katika viwanja na sehemu tukufu za Mina, Arafat na Muzdalifa ni vigumu kwa Waheshimiwa Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kuweza kupiga kura wakiwa huko."

Akiandika kwa msisitizo, ofisa wa ubalozi anasema: "Wanaoruhusiwa kufika huko ni mahujaji tu ambao wanakuwa na vitambulisho maalum katika vikundi vyao na kunakuwa na ulinzi wa hali ya juu."

Aidha, ubalozi unasema: "Hijja ya mwaka huu imekuwa na ulinzi mkali kutokana na nchi ya Saudi Arabia kuwa katika vita dhidi ya magaidi wanaojiita wa Himaya ya Kiislamu (ISIS), huko Iraq na Syiria."

"Serikali ya Saudi Arabia imetangaza wazi kuwa mtu yoyote asiyekuwa Hujaji hataingia katika eneo la Haram na kwingineko. Hii ndiyo hali halisi."

Haijafahamika wanaoitwa wajumbe-mahujaji kutoka Tanzania, ambao wanadaiwa kupiga kura, walikuwa wapi wakati wanapiga kura zao, wakati ubalozi umekwishatoa maelezo kuhusu kutoweza kusimamia zoezi hilo katika mazingira ya Hijja.

Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inataka, ili Katiba inayopendekezwa kwa wananchi iweze kupitishwa na "Bunge la Katiba" na kwenda kwa wananchi kwa ajili ya kura ya maoni, sharti ikubaliwe kwa theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar.

Ni hapa ambapo Mjumbe wa Zanzibar alifanywa kuwa mjumbe kutoka Tanzania Bara kwa sababu ambazo hazijaelezwa.

Wachunguzi wa mambo wanasema: "Ilikuwa kupunguza kura ya hapana kutoka Zanzibar kwa kuwa mjumbe huyo alionyesha dalili zote za kukataa mapendekezo."

Mjumbe huyo ni Maulida Komu (Anna Komu), mbunge Viti Maalum, kutoka Chama cha Demekrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Jana, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Rais Kikwete alitarajiwa kukabidhiwa Katiba Mpya Inayotarajiwa. Hatua hii inakuja baada ya Sitta, aliyekuwa mwenyekiti wa Bunge Maalum, kutangaza kuwa mchakato umekamilika.

Katika mchakato huu, maoni mengi ya wananchi yameachwa, msingi wa katiba umebomolewa na muundo wa serikali tatu ambao ulipendekezwa kuwa bora kwa maendeleo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, umetupiliwa mbali.

Maelezo yaliyomo katika barua ya balozi nchini Saudi Arabia, yanaongeza utata juu ya kinachoitwa mahujaji kupiga kura.

Kwa mfano, akiandika kwa mwenyekiti wa bunge hilo, mjumbe kutoka Zanzibar, Dk Maua Daftari anasema: "Nakiri kukubaliana na vifungu vyote vya Katiba kama tulivyopitisha."

Andishi la Dk Daftari lililoambatanishwa na "fomu ya kupigia kura," liliandaliwa na kutumwa tarehe 28 Septemba. Inaonyesha kuwa Dk Daftari anakubaliana na mapendekezo juu ya ibara zote za katiba.

Hata hivyo, katika andishi lake kwa mwenyekiti wa Bunge Maalum, Hassan Salim Turky, anayedaiwa kupiga kura akiwa hospitalini Chennai, nchini India hakutamka iwapo amepiga kura ya ndiyo au hapana.

Amesema: "Mhe Mwenyekiti kwa heshima kubwa naomba nikupongeze wewe binafsi pamoja na Makamu wako wa mwenyekiti na Kamati ya Uongozi ya Bunge kwa namna mlivyoniwezesha kutumia haki yangu ya kidemokrasia na kuweza kupiga kura yangu nikiwa hapa Chennai, India hospitalini."

Amesema: "Nawapongeza sana na nawatakia kila la kheri waheshimiwa wajumbe wenzangu wa Bunge la Katiba katika kufanikisha kazi hii kubwa inayotukabili hivi sasa."

Hayo yanaandikwa wakati Mjumbe anayedaiwa kutumwa katika nchi hizo, ili kupigisha kura, ametajwa kuwa ni Suleiman Haji Suleiman.

Haijafahamika alifanya nini Saudi Arabia ambako hakukuwa kunaingilika na tayari kulikuwa na msimamo rasmi wa ubalozi wa Tanzania.

Suleiman Haji Suleiman ni mwandani wa kinachoitwa, "mtandao wa urais" wa Shamsi Vuai Nahodha.

Tofauti ya muda kati ya India na Saudia, ni zaidi ya saa nne, tofauti kati ya Tanzania na India, ni saa tano na tofauti kati ya Tanzania na Saudi Arabia, ni saa moja.

Gazeti hili limeshindwa kufahamu iwapo Suleiman alitumia ndege binafsi kusafiri kwenda India kupigisha kura mtu mmoja, na kisha kuondoka siku hiyohiyo na kufika Saudi Arabia kufanya kazi hiyo hiyo (ambayo balozi aliishaeleza kuwa haiwezi kufanyika).

Maulida Komu aliyefanywa mjumbe kutoka Tanzania Bara, ndiye aliyekuwa mgombea mwenza wa Freeman Mbowe katika uchaguzi mkuu mwaka 2005.

Ni katika kipindi hicho, utata juu ya utaifa wake Visiwani, uliibuka na kuhojiwa mahakamani, baada ya Mchungaji Christopher Mtikila kufungua kesi kupinga mwanasiasa huyo kuwa mgombea mwenza kwa kile alichodai, siyo raia kutoka Zanzibar.

Mahakama Kuu ya Zanzibar, baada ya kusikiliza pande zote mbili, iliridhika kuwa Maulida anatoka Zanzibar.

Akizungumzia utata wa kura, Ismail Jussa amesema: "Kura zilizopigwa kupitisha Sura ya Kwanza hadi Sura ya Kumi ya Rasimu ya Katiba…hazikupata theluthi mbili…Hii ni kwa sababu katiba hii haipelekwi vipande vipande kwa wananchi…Inapelekwa yote."

"Siku ya kwanza ya kupiga kura…wajumbe saba (7) waliikataa katiba. Siku ya pili aliongezeka mwanasheria mkuu wa serikali. Jumla yake ni wanane (8). Wajumbe wa UKAWA wamewataja kuwa wako 65; ingawa sisi tunajua wako 66. Mjumbe mmoja hakupiga kura," anasema Jussa na kuongeza:

"Kwa hesabu ya wajumbe 219, theluthi mbili ni wajumbe 146. Wajumbe ambao hawakupiga kura na wale waliokataa vifungu vya katiba jumla yao ni 74. Hivyo katiba ya Sitta na CCM yake imepitishwa na wajumbe 145…badala ya 146 wanaotakiwa kwa mujibu wa sheria."

UKAWA inaundwa na vyama vya NCCR- Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), National League for Democracy (NLD), Democratic Party (DP) na baadhi ya wajumbe kutoka kundi la 201 la wajumbe walioteuliwa kutoka asasi za kijamii.

Utata wa kura unaongezeka pale mjumbe aliyetumwa kwenda India na Saudia Arabia kuwapigisha kura wajumbe wa Bunge Maalum, kupigisha kura hizo kwa siku moja katika nchi zote mbili.

Kwa mfano: Dk Daftari, Asha Dodoo Mtwangi, Shawana Bukheti Hassan, Salim Turky na Amina Andrew Clement wote wanadaiwa kupiga kura zao tarehe 28 Septemba, 2014.

Wakati Dk Daftari akionyesha kukubaliana na vifungu vyote vya katiba iliyopendekezwa na Turky kutosema lolote, Bukheti alisema: "Sina pingamizi juu ya Ibara yoyote ile kwa yale ambayo yamo kwenye rasimu hiyo."

Kauli kuwa anakubaliana na yote yaliyomo katika "rasimu" inaweza kutafsiriwa kuwa, kile ambacho mjumbe anakubaliana nacho ni "Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba" na siyo rasimu iliyopendekezwa na bunge maalum."

Rasimu ya Jaji Warioba, ilipendekeza kuwapo Nchi Moja yenye Shirikisho la Serikali Tatu – Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Jamhuri za Muungano.

Muundo wa Muungano wa serikali mbili, uliosheheni malalamiko ya miaka 50 ya "Tanganyika kuvaa koti la Muungano" na Zanzibar kugeuka "koloni la Tanganyika" umekuwa uking'ang'anizwa na CCM, na ndio Sitta amefanikisha katika hatua ya mwisho.

Aidha, Katiba inayopendekezwa, imepatikana chini ya vitisho, matusi, kejeli na ghiliba za viongozi wa CCM na serikali.

Hata mwanasheria mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, aliyekataa vifungu vingi katika andishi la mwisho, tayari amefukuzwa kazi na Rais Mohamed Shein.

"Huu ndio wakati mwafaka kwa wananchi kuanza kufikira kuwa na Katiba Mpya…Hili ni bomu," ameeleza Tundu Lissu, mwanasheria wa Chadema huku akiahidi kuzunguka nchi nzima kuelimisha wananchi jinsi ya kukataa hatari iliyoandaliwa na Sitta..

Chanzo:
Mawio
 
Gazeti la Mawio ambalo mmiliki wake Saed Kubenea alienda Mahakama Kuu, Dar kutaka bunge Maalum livunjwe.

Sasa kwa mantiki hii, unategemea litaleta habari gani chana kuhusiana na Bunge Maalum.

Hoja kuhusu Katiba inayopendekezwa imeishafungwa kisheria kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyotaka.

Hoja iliyopo mezani kwa sasa ni Mchakato wa kura ya maoni.

Taifa endelevu haliwezi kujengeka katika reactive politics kwa kutafuta sindano kwenye mchanga wa bahari.
 
Sawa kwa habari nyengine zaidi nenda katika mada ya afisa wa ubalozi wa Tz Saudi Arabia arudishwa tanzania.
Ni kutokana na barua yake alio Andika juu ya upigaji kura ya wajumbe walioko hija.
 
jk alisema kila jambo lina wakati wake, jaji warioba aliona sasa ni wakati kwa watanzania kupata katiba bora na yenye lengo la kuinufaisha nchi na watu wake lakini sita na wenzake wakaamua kupindisha kwa makusudi ili walinde masilahi ya wakubwa zao na hili limejizihirisha. sasa niwakati kwa watanzania kuamka na kuchukua hatu. No katiba mpya
 
Nyie CCM ni watu wa ajabu sana !

Hivi kweli mnafikiri kitendo chenu cha kupora kura hadharani kitaachwa hivi hivi, kwa hoja nyepesi kwamba eti hilo suala limeishafungwa !. Nani kalifunga ?

Kwa upande wetu, tunaopinga hiyo katiba yenu, wizi huo wa kura za wajumbe wa Zanzibar itakuwa ni part na parcel ya campaign yetu ya HAPANA whether mnataka au hamtaki !. Kitu cha wizi ni cha wizi tu na ni haram na hakikubaliki ?!

Leo mtu akiniletea bidhaa nzuri na ya gharama na hata akawa anaiuza kwa bei nafuu.....nitakapogundua ni ya wizi, sitainunua. Nitaikataa.....

Katiba yenu ya wizi, hatutaikubali na tutawashiwishi na waTz wengine waikatae !

Gazeti la Mawio ambalo mmiliki wake Saed Kubenea alienda Mahakama Kuu, Dar kutaka bunge Maalum livunjwe.

Sasa kwa mantiki hii, unategemea litaleta habari gani chana kuhusiana na Bunge Maalum.

Hoja kuhusu Katiba inayopendekezwa imeishafungwa kisheria kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyotaka.

Hoja iliyopo mezani kwa sasa ni Mchakato wa kura ya maoni.

Taifa endelevu haliwezi kujengeka katika reactive politics kwa kutafuta sindano kwenye mchanga wa bahari.
 
Hili suala la hizi namba za kura ninavyoona lina utata ulio wazi, na hata mtu akienda mahakamani zetu hukumu bado zitakuwa zile zile. Lakini wenye akili wanajua na muda sio mrefu litapata majibu sahihi na sio ajabu ukamsikia Sitta akitafuta huruma ya Watanzania kwa kisingizio cha 'kutekeleza maamuzi ya kichama'. Huyu mtu haaminiki sana na ndio maana alisimama sana majukwaani kuipinga serikali ya ccm ambamo naye ni mwanachama lakini baada ya 'kuzawadiwa' uwaziri ametugeuka!
 
kumbe chanzo mawio ndomaana
ebu tutolee uchafu wako huu
 
Hili suala la hizi namba za kura ninavyoona lina utata ulio wazi, na hata mtu akienda mahakamani zetu hukumu bado zitakuwa zile zile. Lakini wenye akili wanajua na muda sio mrefu litapata majibu sahihi na sio ajabu ukamsikia Sitta akitafuta huruma ya Watanzania kwa kisingizio cha 'kutekeleza maamuzi ya kichama'. Huyu mtu haaminiki sana na ndio maana alisimama sana majukwaani kuipinga serikali ya ccm ambamo naye ni mwanachama lakini baada ya 'kuzawadiwa' uwaziri ametugeuka!
shukurani ya punda ni mateke.nae siku zake zinahesabika
 
Gazeti la Mawio ambalo mmiliki wake Saed Kubenea alienda Mahakama Kuu, Dar kutaka bunge Maalum livunjwe.

Sasa kwa mantiki hii, unategemea litaleta habari gani chana kuhusiana na Bunge Maalum.

Hoja kuhusu Katiba inayopendekezwa imeishafungwa kisheria kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyotaka.

Hoja iliyopo mezani kwa sasa ni Mchakato wa kura ya maoni.

Taifa endelevu haliwezi kujengeka katika reactive politics kwa kutafuta sindano kwenye mchanga wa bahari.
Jibu hoja acha kucheka baada ya kujitekenya, Subiri wanaume wakutekenye ndipo ucheke vizuri.
 
Kwa wale waliokwenda kutubu kwa Mwenyezi Mungu huko Makka wanaweza wakaulizwa kuhusu upigaji wao wa kura ulikuwaje, na hatutegemei kupata majibu yaliyokua si ya kuaminika hawa watu wanatoka Hijja ukweli kwao kwa sasa tunaupa kipaumbele
 
Duh tutasikia na yataibuka mengi sana from now onwards
 
sita kwakua ni nikibaraka wa ccm anadiriki kupindua mawazo ya wananchi hakika huyu hatufai niaheri kama angekua mh. pandu amiri kificho angefanya mabadiliko yakweri kwakutupatia katiba mpya ya wananchi kwan uwezo wake tumeuona wakati akiwa mwenyekiti wa muda BMK hakika angeendelea mh. huyu naamini hata neno UKAWA lisingekuwepo nakama ingetokea mm nkashika nchi sitta angekuwa wakwanza kuhukumiwa kwa kosa la kupotosha mawazo ya wananchi kupitia mh.jaji WARIOBA sijui nani ataibuka kutetea maoni sahihi wananchi hakika watanzania tuamke ccm wanatumaliza bila uoga.
 
Kura ya hapana inarudiwa kesho yake ili iwe ya ndiyooooo, kweli mi-ccm haina aibu kabisaa, Aloooo haya kama si masihara ni nini?
 
Gazeti la Mawio ambalo mmiliki wake Saed Kubenea alienda Mahakama Kuu, Dar kutaka bunge Maalum livunjwe.

Sasa kwa mantiki hii, unategemea litaleta habari gani chana kuhusiana na Bunge Maalum.

Hoja kuhusu Katiba inayopendekezwa imeishafungwa kisheria kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyotaka.

Hoja iliyopo mezani kwa sasa ni Mchakato wa kura ya maoni.

Taifa endelevu haliwezi kujengeka katika reactive politics kwa kutafuta sindano kwenye mchanga wa bahari.

Jifunze kuangalia hoja iliyo mezani kisha uipime, sio kuangalia mtu. Huo ndio utaratibu wa mijadala.
Ova
 
Gazeti la Mawio ambalo mmiliki wake Saed Kubenea alienda Mahakama Kuu, Dar kutaka bunge Maalum livunjwe.

Sasa kwa mantiki hii, unategemea litaleta habari gani chana kuhusiana na Bunge Maalum.

Hoja kuhusu Katiba inayopendekezwa imeishafungwa kisheria kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyotaka.

Hoja iliyopo mezani kwa sasa ni Mchakato wa kura ya maoni.

Taifa endelevu haliwezi kujengeka katika reactive politics kwa kutafuta sindano kwenye mchanga wa bahari.

Sijui una miaka mingapi, but nakuhakikishia, hii nchi itaendelea kuwa maskini hadi utakapokufa na hata vitukuu vyako, sababu, haioneshi kuwa na maendeleo yoyote katika Taifa. Mtaendelea kuwahudumia viongozi tu hadi watapokufa bila kuwahudumia wananchi. Huu ndo ukweli kaka. Tujifunzeni nchi zingine zinazoendelea kwa kasi, katiba zao zikoje? Unatunga katiba ya kumlinda kiongozi, unategemea nini, waTZ wengi wajinga sana.
 
We kilaza kweli,kama hoja kuhusu katiba inayopendekezwa imeishafungwa sasa kura ya maoni tutapigia nini.Halafu jifunze kujibu hoja na si kuleta mipasho humu.
 
Gazeti la Mawio ambalo mmiliki wake Saed Kubenea alienda Mahakama Kuu, Dar kutaka bunge Maalum livunjwe.

Sasa kwa mantiki hii, unategemea litaleta habari gani chana kuhusiana na Bunge Maalum.

Hoja kuhusu Katiba inayopendekezwa imeishafungwa kisheria kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyotaka.

Hoja iliyopo mezani kwa sasa ni Mchakato wa kura ya maoni.

Taifa endelevu haliwezi kujengeka katika reactive politics kwa kutafuta sindano kwenye mchanga wa bahari.
Katika pitapita yangu nimekutana na tangazo hili , " KARIBU TANZANIA , NCHI AMBAYO DEREVA WA SERIKALI NI LAZIMA AWE NA ANGALAU ELIMU YA KIDATO CHA 4 BILA KUSAHAU CHETI CHA VETA , ILA KIONGOZI WA SERIKALI ANATAKIWA KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA TU ! " mwisho wa kunukuu .
 
Sijui una miaka mingapi, but nakuhakikishia, hii nchi itaendelea kuwa maskini hadi utakapokufa na hata vitukuu vyako, sababu, haioneshi kuwa na maendeleo yoyote katika Taifa. Mtaendelea kuwahudumia viongozi tu hadi watapokufa bila kuwahudumia wananchi. Huu ndo ukweli kaka. Tujifunzeni nchi zingine zinazoendelea kwa kasi, katiba zao zikoje? Unatunga katiba ya kumlinda kiongozi, unategemea nini, waTZ wengi wajinga sana.
Mkuu umeandika kizalendo sana ! Lakini ubaya wa bahati ni kwamba huyo unayem quote ni mnufaikaji wa juu kabisa wa huu mfumo mbovu ! Huyu ni kati ya vijana watakaokufa njaa wiki chache sana baada ya ccm kufa .
 
Back
Top Bottom