Sitta alivyowadanganya watanzania

Sitta alivyowadanganya watanzania

Gazeti la Mawio ambalo mmiliki wake Saed Kubenea alienda Mahakama Kuu, Dar kutaka bunge Maalum livunjwe.

Sasa kwa mantiki hii, unategemea litaleta habari gani chana kuhusiana na Bunge Maalum.

Hoja kuhusu Katiba inayopendekezwa imeishafungwa kisheria kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyotaka.

Hoja iliyopo mezani kwa sasa ni Mchakato wa kura ya maoni.

Taifa endelevu haliwezi kujengeka katika reactive politics kwa kutafuta sindano kwenye mchanga wa bahari.

samahani mkuu nilitegemea ungekuja na hoja ya kupangua shutuma zinazoikabili katiba ya chama chenu kuliko kuja na ushabiki wa kubwabwaja bwabwaja.hata kama mtu umeshikwa kama msukule,muwe mnabakiza hata kijiakili kidogo cha kufikiri na kuangalia upande wa pili wa shilingi.kusema tu katiba imepita,hata vyama vya saccos,vyama vya kufa na kuzikana navyo huwa vina katiba na vinapitisha pia lakini siyo kama hiyo ya chama chenu.hivi unadhani mataifa mengine yenye migogoro yalifika hapo yalipo kwa staili gani?au unadhani tanzania inatoka planet mars?uwe unabakiza kijiakili kidogo cha kujiongoza sio unajiendea endea kama bata mjamzito
 
Katika pitapita yangu nimekutana na tangazo hili , " KARIBU TANZANIA , NCHI AMBAYO DEREVA WA SERIKALI NI LAZIMA AWE NA ANGALAU ELIMU YA KIDATO CHA 4 BILA KUSAHAU CHETI CHA VETA , ILA KIONGOZI WA SERIKALI ANATAKIWA KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA TU ! " mwisho wa kunukuu .

mkuu ishia hapo hapo,mingine ni misukule haita kaa ielewe
 
Gazeti la Mawio ambalo mmiliki wake Saed Kubenea alienda Mahakama Kuu, Dar kutaka bunge Maalum livunjwe.

Sasa kwa mantiki hii, unategemea litaleta habari gani chana kuhusiana na Bunge Maalum.

Hoja kuhusu Katiba inayopendekezwa imeishafungwa kisheria kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyotaka.

Hoja iliyopo mezani kwa sasa ni Mchakato wa kura ya maoni.

Taifa endelevu haliwezi kujengeka katika reactive politics kwa kutafuta sindano kwenye mchanga wa bahari.

lakini je,hiyo hoja ni ya uongo?kwa mantiki hiyo,hiyo katiba si halali kwakuwa haikupita kihalali,lazima tuseme ukweli hata kama mnatulazimisha tuamini ushenzi wenu.ccm wote nitawachukia milele.
 
Sijui una miaka mingapi, but nakuhakikishia, hii nchi itaendelea kuwa maskini hadi utakapokufa na hata vitukuu vyako, sababu, haioneshi kuwa na maendeleo yoyote katika Taifa. Mtaendelea kuwahudumia viongozi tu hadi watapokufa bila kuwahudumia wananchi. Huu ndo ukweli kaka. Tujifunzeni nchi zingine zinazoendelea kwa kasi, katiba zao zikoje? Unatunga katiba ya kumlinda kiongozi, unategemea nini, waTZ wengi wajinga sana.
sawa lakin neno wajinga futa katika akili yako hiliyo ganda kama mafuta ya baby care
 
Gazeti la Mawio ambalo mmiliki wake Saed Kubenea alienda Mahakama Kuu, Dar kutaka bunge Maalum livunjwe.

Sasa kwa mantiki hii, unategemea litaleta habari gani chana kuhusiana na Bunge Maalum.

Hoja kuhusu Katiba inayopendekezwa imeishafungwa kisheria kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyotaka.

Hoja iliyopo mezani kwa sasa ni Mchakato wa kura ya maoni.

Taifa endelevu haliwezi kujengeka katika reactive politics kwa kutafuta sindano kwenye mchanga wa bahari.
Ni vyema pia kuangalia mchakato mzima ikiwa kweli umetupa kilicho bora. Ikiwa kulikuwa na ghiriba dhahiri tunapaswa kuzisahihisha. Nimeona kwenye taarifa ya habari usiku huu mjumbe kutoka zanzibar akikanusha kupiga kura lakini yuko kwenye orodha ya waliopiga kura. Je hili nalo liachwe?
 
Breaking News: Afisa Balozi ambae ni Mzanzibari afukuzwa kazi !
AFISA WA UBALOZI WA TZ SAUDI ARABIA ARUDISHWA TANZANIA
Na Jabir Idrissa, Zanzibar
HATIMAYE Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman, amefutwa kazi. Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein ametangaza kumfuta kazi Othman; na nafasi yake tayari imechukuliwa na naibu wake, Said Hassan Said, imeeleza taarifa ya serikali.

Taarifa hiyo iliyosomwa kwa vyombo vya habari juzi inasema, Othman amefutwa kazi kwa mujibu wa vifungu vya 53, 54(1) na 55(3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 2 ya 2011.
Taarifa za kufutwa kazi kwa Othman zilisambaa jioni ya juzi kupitia vituo vya televisheni, ambavyo vilieleza kuwa Dk. Shein alimfuta kazi mwanasheria huyo. Hakutaja sababu isipokuwa vifungu vya sheria.
Othman alikuwa miongoni mwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba waliopiga kura ya HAPANA kwa katiba inayopendekezwa.
Mwanataaluma huyo ambaye awali aliondoka bungeni, alirejea siku ya mwisho ya upigaji kura; ambapo alikataa karibu theluthi mbili za ibara zote za katiba iliyopendekezwa. Katiba hiyo ina Sura 71 na Ibara 289.
Wakati Othman akifutwa kazi, ofisa mwingine wa ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, anadaiwa kuagizwa kurejea nchini.
Ofisa aliyeagizwa kurejea nchini amefahamika kwa jina moja la Masoud. Ni mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa anayetokea Zanzibar.
Mfanyakazi huyo ambaye ni afisa wa ngazi ya juu, ndiye aliandika barua akionesha kuwa mazingira yaliyoko maeneo ya Makkah, Saudia, hayangeruhusu wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kupiga kura.
MAWIO limefahamishwa kuwa barua hiyo iliyosainiwa kwa niaba ya Balozi, ikiwa ni majibu ya barua ya awali iliyotoka Ofisi ya Bunge Maalum, mjini Dodoma, ilieleza kwa ufasaha katika aya ya mwisho, kwamba “haitawezekana wajumbe wa Bunge Maalum kupiga kura.”

Taarifa kutoka Saudi Arabia na mjini Dodoma zinasema, barua hiyo tayari imeleta mgogoro ndani ya serikali, baada ya kufichuka kwa siri juu ya kinachoitwa “theluthi mbili ya kura kutoka Zanzibar.”
Masoud, kwa wadhifa wake ubalozini, ni miongoni mwa maofisa walioidhinishwa kusaini barua kwa niaba ya balozi.
“Ni kweli wametaka arejee nchini haraka. Hivi ninavyokwambia Masoud tayari ameondoka Riyadh kurejea huko (Tanzania). Lakini hapa ubalozini, msimamo uko wazi, kwamba hakuna kosa alilolitenda,” anaeleza mtoa taarifa ndani ya ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia.

Amesema, “Sasa Masoud ni mmoja wa maofisa wachache walioidhinishwa kulingana na nyadhifa walizonazo, kusaini barua yoyote kwa niaba ya balozi, kwa hivo hajatenda kosa lolote la kinidhamu.”
Taarifa zinasema, balozi amekuwa zaidi katika maeneo ya Makkah kusimamia usalama wa mahujaji wa Tanzania wakiwemo wake wa viongozi kadhaa wa kitaifa; jambo ambalo lilimlazimisha Masoud kufanya kazi hiyo kwa niaba yake.
Barua iliyosainiwa na Masoud, tayari imevuja katika mitandao ya kijamii.
“Unajua Balozi amekuwa hayupo hapa Riyadh muda mwingi. Yeye anashughulikia masuala ya usalama wa mahujaji Makkah; kwa hivyo tuliopo Riyadh ndio tunatekeleza kazi tunazotakiwa kuzifanya,” alisema mtumishi mwingine.

Taarifa zaidi kutoka ndani ya Bunge Maalum zinasema mazingira yaliyokuwepo Makkah, wakati wa ibada ya Hijja, hayakuwezesha wajumbe wa bunge hilo walioko katika ibada hiyo, kupiga kura kama ilivyotarajiwa.
Katika hatua nyingine, watu mbalimbali waliozungumza na gazeti hili wanasema kilichotokea Dodoma katika kupiga na kuhesabu kura, kitakuwa “kitendawili kikubwa.”
“Kila nikipima nakuta ninaumizwa na utamaduni wa kikulacho kinguoni mwako. Kwamba wapo wenzetu hawajali maslahi ya nchi isipokuwa matumbo yao,” ameeleza Omar Said wa Michenzani.
Naye Rashid Sultani anayeishi Mkunazini, Unguja amesema, itamchukua muda mrefu kuamini kuwa theluthi mbili ya kura za wajumbe wa Zanzibar ilifikiwa.

Suala la kufutwa kazi Othman, kuitwa nyumbani kwa ofisa wa ubalozi na mjadala juu ya theluthi mbili ya kura kutoka Zanzibar, ni miongoni mwa mambo ambayo yanatarajiwa kuchukua nafasi kubwa katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Chama cha Wananchi (CUF), Jumapili hii mjini Zanzibar.
Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ya Umma ya CUF imesema Katibu Mkuu wa Chama na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, ndiye atakakuwa msemaji mkuu.
Chanzo: Mawio
 
Kwani hakuna namna ya kwenda kuyapinga Mahakamani,au Mahakama itasema tena ni Swala la kisiasa na si kisheria.
 
sisi tunajiandaa kuandika katiba yetu na raisi wetu mwingine 2016
 
Utata mwingine ni huu wa kuhesabu kura ya Marehemu mama yake Zitto kuwa naye alipiga kura ya NDIO...yaani mainterahamwe hata hayaheshimu Marehemu..
 
Sijui una miaka mingapi, but nakuhakikishia, hii nchi itaendelea kuwa maskini hadi utakapokufa na hata vitukuu vyako, sababu, haioneshi kuwa na maendeleo yoyote katika Taifa. Mtaendelea kuwahudumia viongozi tu hadi watapokufa bila kuwahudumia wananchi. Huu ndo ukweli kaka. Tujifunzeni nchi zingine zinazoendelea kwa kasi, katiba zao zikoje? Unatunga katiba ya kumlinda kiongozi, unategemea nini, waTZ wengi wajinga sana.

Hata Mzee mwenyewe Moses Nnauye alikufa maskini hata kibanda hana Dar, muulize huyo kama an hata banda la kurithi.
 
Katika pitapita yangu nimekutana na tangazo hili , " KARIBU TANZANIA , NCHI AMBAYO DEREVA WA SERIKALI NI LAZIMA AWE NA ANGALAU ELIMU YA KIDATO CHA 4 BILA KUSAHAU CHETI CHA VETA , ILA KIONGOZI WA SERIKALI ANATAKIWA KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA TU ! " mwisho wa kunukuu .

Sasa we ulitegemea Chenge aandke katiba ya aina gani?
Wajumbe walikuwa pale kula posho tu!
 
Back
Top Bottom