sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,487
Timua ya wabunge kutoka kwenye vikao vya bunge, haikuanzia kwa kina Bulaya bali kwa kumbukumbu zangu, mh. Samwel Sitta alishamtimua Zitto Kabwe kipindi cha Kikwete.
Kilichotokea baada ya Zitto kutimuliwa ni kama ukimpiga chura teke unamwongezea mwendo, na ndivyo ilikuwa kwa Zitto kuwa, kufukuzwa kwake kulimwimarisha kisiasa.
Sasa kwa tukio la sasa la kuwasimamisha wabunge 7 wa upinzani kunaweza kukawaimarisha kisiasa ama kukawaangamiza kisiasa kulingana na hoja waliyokuwa wanaisimamia. Swali ni kwamba hoja waliyokuwa wanaisimamia ina maslahi gani kwa taifa ukilinganisha na ile ya Zitto kwa wakati ule?
Tusibeze sana, tusiwasikitikie sana, tusiwapongeze sana, tusiwalaumu sana, tuwape muda. Haya yalifanyika kwa Zitto wakati ule na sasa amekuwa maarufu zaidi. Haya yalifanyika kwa Kafulila na leo amesahaulika kabisa. Tuwape muda pengine inaweza ikawa faida kwao ama hasara katika kujiimarisha kisiasa ama kujichimbia shimo refu la siasa.
Tujue kwamba hakuna serikali ambayo ipo "flexible" kote duniani. Sitta aliwahi kusema mwanasiasa sharti uwe na ngozi ngumu na siasa siyo uadui. Leo Tulia kamtimua Zitto, miaka michache ijayo unaweza ukakuta wamekuwa mume na mke. Tuwape muda.