Sitta Aibeza CCM Asema Dola isitumike dhidi ya Chadema!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta Aibeza CCM Asema Dola isitumike dhidi ya Chadema!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mr. Zero, Mar 9, 2011.

 1. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Sitta: Dola isitumike dhidi ya Chadema Send to a friend
  Tuesday, 08 March 2011 21:58 0diggsdigg

  Sheilla Sezzy, Mwanza
  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta ameishauri Serikali isitumie vyombo vya dola kuzima moto wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutokana na kauli zao za uchochezi. Kauli hiyo inapingana na msimamo wa CCM uliotolewa hivi karibuni na Katibu wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Itikadi na Uenezi, John Chiligati ulioitaka serikali na vyombo vya dola kuchukua hatua dhidi ya viongozi wakuu wa Chadema kwa kuwa, wanachochea uasi dhidi ya serikali iliyopo madarakani.

  Sitta amesema hayo siku nne tu baada ya Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya tatu, Frederick Sumaye kukitaka CCM kukabiliana na hoja za Chadema kisiasa badala ya kuiachia serikali ipambane nao akisema kazi ya siasa ni ya chama na si serikali. Hivyo kinapaswa kuwa mstari wa mbele kupambana na Chadema kwa sera na kujibu hoja zao zote ili kuongeza imani ya wananchi kwa chama hicho.
  “Wale (Chadema) wanafanya kazi za siasa na hawa (CCM) wamekaa kimya, wanaiachia serikali ndiyo inatoa majibu, hali hiyo si nzuri. Chama kinapaswa kujibu hoja zote na kama hakina majibu, kiombe kwa serikali,” alisema Sumaye.

  Akizungumza wakati wa mapumziko kwenye mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini hapa, Sitta alisema kuwa Serikali inatakiwa kutambua kuwa vyama vya upinzani vipo na vimejiimarisha kutaka kuing'oa serikali hii na kwamba ndani yake kuna viongozi ambao wanakubalika kwa wananchi.
  "Kutokana na uimara walionao, Serikali isitegemee kwamba wapinzani wataongea lugha nyepesi juu yake na viongozi wake na wala tusitegemee kuwa wapinzani ni rafiki zetu watatuonea huruma. Kinachotakiwa ni kujirekebisha haraka na kuwa wepesi wa kukubaliana na mambo," alisema Sitta.

  Lakini alisema Serikali inatakiwa kuchukua hatua mapema katika jambo lolote linalokwenda kinyume na taratibu badala ya kukaa muda mrefu na kuwaingiza wananchi katika wasiwasi.Sitta alisema kuwa viongozi waliopo madarakani wanatakiwa kujitazama na kuachana na tabia ya kutumia vyeo vyao kuendeleza biashara zao jambo ambalo hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alilikemea na kuwataka watu wote kuwa sawa.
  "Mimi binafsi nashangaa kiongozi ambaye ni mbunge ni mfanyabiashara mkubwa mwenye biashara kubwa sana anapata wapi muda wa kufanyabiashara hiyo kama siyo kutumia madaraka yake katika kuendeleza biashara hizo?" Alihoji Sitta. Alisema kuwa wananchi wana macho na wanaona chama hakifai kutokana na viongozi kutumia madaraka kujinufaisha wenyewe na kwamba hiyo ndiyo inayochafua mazuri ya CCM.

  Anaamini kuwa wakati umefika kwa chama kuchukua hatua kama Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete alivyobainisha awali kwa kuwa hakiwezi kuyaacha mazuri ya CCM yakayeyuka pasipo sababu. "Naamini viongozi wa katika ngazi ya Taifa watahakikisha amani inakuwapo ndani ya chama. Bado tuna mashabiki wengi wanaokipenda chama ila wanakwazika pindi wanapoona kunakuwapo na ucheleweshwaji wa kuchukua hatua," alisema Sitta.
  Akizungumzia vuguvugu la siasa nchini, Sitta aliwataka wapinzani wasitumie ukame unaolikabili taifa kuwahadaa wananchi kwa sababu, hali hiyo inaweza kuikumba serikali ya nchi na chama chochote duniani na kwamba hii iliyopo madarakani, haipaswi kubebeshwa lawama.
  Alisema kuwa si busara kwa wapinzani kuhubiri habari za kumwaga damu na kuwataka wananchi kulinganisha wapinzani na serikali iliyopo madarakani kwa kuhoji kama itaweza kuwa serikali mbadala badala ya CCM. Alisisitiza kwamba CCM ina hazina kubwa ya viongozi ambao wanaweza kuendesha nchi hii na kudai kuwa, wanachama wa chama hicho tawala wana nafasi ya kuwaondoa viongozi wabovu kwenye uchaguzi ndani ya chama utakaofanyika mwaka 2012.
  Mjadala wa uhalali wa mikutano na maandamano ya Chadema uliibuliwa na Rais Jakaya Kikwete alipolieleza taifa kuwa, chama hicho cha upinzani kina lengo la kuleta machafuko nchini. Rais Kikwete alisema hayo alipokuwa akilihutubia taifa mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu kupitia redio na televisheni.Kauli hiyo ya Rais Kikwete ambaye Chadema waliipuuza, ilisisitizwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira aliyeonya kuwa Chadema kisije kuilaumu serikali ikikosa uvumulivu na kuanza kutumia dola kukishughulikia.

  Source: Mwananchi

  My take: Inaelekea hii serikali sasa haina nahodha bali inajiendea tu. Ndiyo maana tunasikia PM inamshughulikia Magufuri kupitia vyombo vya habari. Kamati ya nishati na madini wanakuwa na nguvu kuliko waziri. Akina Wassira na Chiligati wanawatisha wananchi bila sababu. Tambwe anakuwa msemaji wa Rais, wakati Makamba kaingia mtini.

  Kweli inaelekea huu moto wa CDM limewafikisha joto CCM.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  serikali haina nahodha maana yuko bize huku ughaibuni anahudhuria makongamano akitoka huko apite Loiliondo ndo aje dar
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Umenichekesha kweli mkuu
   
 4. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Mh.Sumaye alikwisha tabiri kuwa " Anayetumia kalamu ya waandishi wa habari kujisafishia njia kwenda ikulu akiingia huko atatumia risasi kujihakikishia Legacy" Hayo yanamkuta Kikwete maana sasa ni mabavu kwa kuidhibiti CDM.hONGERA Sumaye kwa reliable forecast yako
   
 5. coby

  coby JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wanachemshwa mbayaaaa
   

  Attached Files:

 6. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,968
  Trophy Points: 280
  sitta yuko kama amezaliwa upya lakini alipaswa kumtaja rostam waziwazi sio kufumbafumba hawa ndio wanaotuchelewesha
   
Loading...