Sitosahau jinsi nilivyonusurika kuwa Mwalimu

Sitosahau jinsi nilivyonusurika kuwa Mwalimu

Kiongozi Miongoni

Senior Member
Joined
Feb 6, 2021
Posts
195
Reaction score
256
Wasalaam wana wa Jehova.

Ilikuwa mwaka 2007 wakati nimemaliza kidato cha nne nakumbuka wakati huo tunajaza form maalumu za kuchagua vyuo vya kati na shule za Advanced level.

Kulikuwa na MWALIMU mmoja ambaye alikuwa ni rafiki wa familia pia wakati huo aliungana na wazazi wangu wakinitaka nijaze form hizo ili niweze kuchaguliwa kujiunga na vyuo vya walimu kwa ngazi ya cheti.

Moyo wangu ulikataa kujaza uchaguzi huo na nikachagua shule za advance na hatimaye nilipata nafasi ya kujiunga na kidato cha tano mwaka 2008 na ninamshukuru Mungu kwa kuniepusha na suala hilo na hadi sasa nanaitumikia nchi yangu kwenye kada nyingine tofauti na walimu lakini kila nikikumbuka tukio hilo moyo huwa unaenda mbio sana.
 
Huko advance ungeenda kusoma vipi kama kusingekuwa na walim?

Kuna baadhi ya vitu tujifunze kumezea. Kuna methali moja wakati nipo primary ilikuwa inasema;

"Ganda la muwa la jana, chungu kaona kivuno".

Nadhani wengi hawakuielewa ilimaanisha nini, na wewe ni mmoja wao.
 
Back
Top Bottom