Sitawatazama usoni wala fedha za maendeleo
Na Joseph Mwendapole, Mwanza
Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, amesema hatamwangalia mtu usoni atakapochukua maamuzi dhidi ya viongozi wanaotafuna fedha za maendeleo ya wananchi.
Kadhalika, amesema kiongozi asiyeweza kwenda na kasi yake ni heri akajiondoa mapema kabla hayajamkuta ya kumkuta kwa kuwa hapendi viongozi legelege.
Aliyasema hayo juzi wakati wa majumuisho ya ziara yake ya siku nane katika wilaya za Misungwi, Kwimba, Magu, Geita, Nyamagana, Ukerewe, Ilemelwa na Sengerema.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wakuu wa wilaya hizo, madiwani wa mkoa wa Mwanza na karibu viongozi wa mkoa huo.
Bw. Lowassa alisema hatakuwa na msalie mtume kwa viongozi watakaothibitika kutafuna fedha zinazotolewa na serikali kuwaletea wananchi maendeleo.
Aidha, alisema ziara anazofanya si za kutalii bali ni za kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kama walivyoahidi katika uchaguzi mkuu uliopita.
Aidha, aliwaonya viongozi wa wilaya wanaompa takwimu za kupika, ambazo zimekuwa zikileta mkanganyiko katika ziara hizo.
Alisema takwimu nyingi zilizopo katika taarifa za wilaya zinakinzana na zile zilizomo katika taarifa ya mkoa.
``Ninapokuja huku nakuja kufanyakazi sio kutalii kwa hiyo hii tabia ya kufanya mzaha na kunipa takwimu za kutunga sitaki kuanzia leo,` alisema.
Waziri Mkuu alisema hataki kusikia malalamiko ya wananchi kama aliyoyakuta alipotembelea wilaya hizo na aliwataka watendaji kujipanga upya kwa ajili ya kuzitatua.
``Nimesikia malalamiko mengi sana na hii inaonyesha kuna udhaifu mkubwa katika suala la uwajibikaji?nasema sitaki kusikia wananchi wakiishi kwa kuinung?unikia serikali fanyeni kazi,`` alisema.
Sehemu nyingi alizotembelea Waziri Mkuu, wananchi walilalamika kuwa rushwa imetawala katika utoaji wa maamuzi na kwamba mtu mwenye uwezo ndiye mwenye haki siku zote.
Baadhi ya wananchi waliwashitaki viongozi wao kwa Bw. Lowassa kuwa wamekuwa wakiwafukuza maofisini mwao wanapokwenda kuwasilisha malalamiko mbalimbali. ?
SOURCE: Nipashe