Sitawatazama usoni wala fedha za maendeleo - EL!

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
803
Sitawatazama usoni wala fedha za maendeleo

Na Joseph Mwendapole, Mwanza

Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, amesema hatamwangalia mtu usoni atakapochukua maamuzi dhidi ya viongozi wanaotafuna fedha za maendeleo ya wananchi.

Kadhalika, amesema kiongozi asiyeweza kwenda na kasi yake ni heri akajiondoa mapema kabla hayajamkuta ya kumkuta kwa kuwa hapendi viongozi legelege.

Aliyasema hayo juzi wakati wa majumuisho ya ziara yake ya siku nane katika wilaya za Misungwi, Kwimba, Magu, Geita, Nyamagana, Ukerewe, Ilemelwa na Sengerema.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wakuu wa wilaya hizo, madiwani wa mkoa wa Mwanza na karibu viongozi wa mkoa huo.

Bw. Lowassa alisema hatakuwa na msalie mtume kwa viongozi watakaothibitika kutafuna fedha zinazotolewa na serikali kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha, alisema ziara anazofanya si za kutalii bali ni za kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kama walivyoahidi katika uchaguzi mkuu uliopita.

Aidha, aliwaonya viongozi wa wilaya wanaompa takwimu za kupika, ambazo zimekuwa zikileta mkanganyiko katika ziara hizo.
Alisema takwimu nyingi zilizopo katika taarifa za wilaya zinakinzana na zile zilizomo katika taarifa ya mkoa.

``Ninapokuja huku nakuja kufanyakazi sio kutalii kwa hiyo hii tabia ya kufanya mzaha na kunipa takwimu za kutunga sitaki kuanzia leo,` alisema.

Waziri Mkuu alisema hataki kusikia malalamiko ya wananchi kama aliyoyakuta alipotembelea wilaya hizo na aliwataka watendaji kujipanga upya kwa ajili ya kuzitatua.

``Nimesikia malalamiko mengi sana na hii inaonyesha kuna udhaifu mkubwa katika suala la uwajibikaji?nasema sitaki kusikia wananchi wakiishi kwa kuinung?unikia serikali fanyeni kazi,`` alisema.

Sehemu nyingi alizotembelea Waziri Mkuu, wananchi walilalamika kuwa rushwa imetawala katika utoaji wa maamuzi na kwamba mtu mwenye uwezo ndiye mwenye haki siku zote.

Baadhi ya wananchi waliwashitaki viongozi wao kwa Bw. Lowassa kuwa wamekuwa wakiwafukuza maofisini mwao wanapokwenda kuwasilisha malalamiko mbalimbali. ?

SOURCE: Nipashe
 
Wewe huyo Lowassa? ungeanza na kutojiangalia kwenye kioo maana utauona uso wako ukiwa kinala wa MAFISADI!
 
Mh EL

Je, na wewe ikithibitika kwamba ni fisadi tukufanye nini? Au kwa vile swahiba hawezi kukufanya lolote ndiyo maana unatishia wengine?

Hao wanaopika report/takwimu za wilaya, wamejifunza kutoka kwa viongozi wakubwa wa serikalini. Ukipewa report fake usilalamike sana, mbona serikali yako inatoa majibu fake kwenye tuhuma za ufisadi?

Kuna kero nyingine zinahitaji kutatuliwa kwa fedha za kutosha, lakini kama mmewagawia sungura unategemea watatatuaje hizo kero za wananchi? Mbaya zaidi sehemu kubwa ya kasungura mnakamalizia juu kwa juu na wenzako, halafu mifupa na makombo ndiyo mnawapeleka wananchi huko wilayani. Kweli watashiba? Au mnawapelekea shombo ya sungura ili na wao waonekane wamekula sungura ilhali hawashibi na kuishia kuuliza nyama nyingine inakuja lini au paja la sungura liko wapi? Ndiyo maana walikuuliza "maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi?". Hapo kilichokosekana ni sentensi ya nyongeza kwamba mbona pamoja na huu ugumu wa maisha wewe wanakuona umenawiri wakati wao wamepigika ile mbaya na bado unasema ndege unapaa!
 
Hata Nikitaka Kum tetea Lowasa - Nashindwa!!....
(((((((((((Aibu)))))))))))
 
mie sishangai na kauli kama hizi kutoka kwa EL,
Mambo ya RICHMOND keshasahau?
suala la CITY water mbona hakuajibishwa?
aanze yeye na wengine watafuata<je ataweza>!
tunawasubiri na ziara zenu za kutuelezea maisha bora kwa kila mtanzania kuanzia j3..
nawaomba wana wa watanzania kwa moyo mmoja,kwa ari mpya,kwa nguvu mpya muwazomee kila watakapopita !
andaeni na mabango kuanzia j3
 
EL energy hii ya kusema maneno haya kaipata wapi?Wala wakubwa na yeye yumo ndani,au amesehau pale alipoagiza magari ya wabunge '90's ame sahahu?
 
Sitawatazama usoni wala fedha za maendeleo

Na Joseph Mwendapole, Mwanza

Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, amesema hatamwangalia mtu usoni atakapochukua maamuzi dhidi ya viongozi wanaotafuna fedha za maendeleo ya wananchi.


Pure nonesense!
 
Lowasa kasahau kuwa hayo ndio malezi ya CCM. Alisema TZ inapaa, kama huko si kupika ni nini?
 
People in this forum are not patriotic one bit. U guys just want to blame Lowassa & the govt. Can't yall see how Takuru is performing in combating corruption?? Don't U people read the newspaper and see cases & cases of people being arrested all over the country?? Didn't U see what happened to MPs in Arusha?? Lowassa is serious and he is on top of his game.

Oh wait a minute, what did I just say ahaahhahahahahhahaha

sorry guys TZ magic tricks (mazingaumbwe) got me for a second ahahahha
 
If he really mean what he says, then it is not too late for him to join on the war against corruption and government resources mismanegement,

It will be very bad if he says that he is against corruption while infact not. But i still hail him for his determination to see development funds are well utilized.

No doubt that a lot of resources allocated by the Central government to the local governments have been misused for a long time.So it takes someone of prime minister position to interfere with this situation,one cannot allow this to continue forever, and so long as the prime Minister is doing this Job then i congratulate him for taking this issue seriously.


Concerning his statement of "kupaa", i would like to say that the statement itself will never make a right decision taken by the prime minister in the future to be wrong just because the statement seem controversial to many people .

I think if the prime Minister continue to address issues with seriousness, firmness, passion, as he has been showing to do recently, then according to me, he will be the second prime Minister next to Sokoine(though i dont agree with his philosophy of "wahujumu uchumi") who is tough and practical enough to take seriously the accountability of local government officials issue in the whole history of the United Republic.

Tanzania needs practical men, men of firmness, especially a President and a Prime minister, otherwise nothing will be done.
 
Huyu jamaa anaropoka sana.. Yaani hiyo kanda ya ziwa ndiko Migodi ilipouzwa kwa bei nafuu, na leo anawashauri wa kazi wa zone hiyo hiyo.

Story za huyu jamaa kama Ken Lay wa Enron, alikuwa anatembea na kitabu cha ethical code ya Enron, kumbe yeye ndio unethical wa kwanza.
 
....unajua haya mambo ya kwenda huku na kule ukijipigisha mikelele kama ya Lowassa huku huna plan or system ya kufuatilia au kuwafanya watu wafanye kazi na wasile hizo pesa unaonekana chizi tuu na tapeli...nchi za wenzetu zimeendelea kwa sababu kuna system nzuri ya uhakika kuwafanya watu wasile pesa za umma na wasile rushwa na sio kwa sababu wao ni wema sana,kuliko kutafuta hiyo cheap popularity ni bora kutumia hizo pesa wakaka chini na wataalam wasugue vichwa namna ya kutrack perfomance na pesa wanazotoa kuliko kusema kuanzia leo sitaki tena tabia hii.
 
Lowasa kasahau kuwa hayo ndio malezi ya CCM. Alisema TZ inapaa, kama huko si kupika ni nini?

Yaani na yeye takwimu zake za Kupikwa?
Any way naona anataka ku-rescue his position from the firing .....
 
Back
Top Bottom