Hute
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,537
- 6,479
sitasahau kituko hiki, nikikumbuka huwa nacheka peke yangu halafu najishangaa.
simu yangu ya kwanza kabisa katika maisha yangu ilikuwa siemens lakini kipindi kile simu ya mkononi tulikuwa tunaiita mobitel kwasababu ndio ulikuwa mtandao wa simu wakati huo kabla ya buzz na tigo. nilikuwa ndio nimemaliza form six na nimenunua simu hiyo, ilikuwa imara sana hata ukidondosha. niliwaringishia sana vijana wenzengu form six leaver si unajua kuwa na simu ya mkononi!
siku moja nikiwa miyomboni Iringa kuna mgahawa mzuriiii pale, niliingia nikala chakula changu safi. nikahisi kwenda msalani. choo ilikuwa ya kiarabu/asian yaani choo ya kibakuli sio ya kukaa ni ya kuchuchumaaa.
nikashusha suruali yangu, nikamaliza mambo yangu simu ilikuwa mfukoni. ile napandisha suruari baada ya kumaliza safari yangu, siemens yangu ikadondokea kwenye ile choo ikaserereka hadi ikaingia ikazama na kupotea kabisa. sikuamini macho yangu.
mle kwenye simu kulikuwa na namba ya msichana wangu wa muhimu sana ambayo bado nilikuwa sijaishika kichwani nimeisevu na ilikuwa nikiwa pale iringa nionane naye tusalimiane zilipendwa. huwezi amini.....niliangalia kama mlango nimeufunga vizuri...kilichoendelea hapo unakijua. ila simu yangu niliipata na choo ile ilikuwa na maji mengi ya bomba, nilinawa sabuni mara saba hivi, na wiki nzima sikuwa na hamu ya kula...hahahahahahaaaaaaaaaaaaaa
ungekuwa wewe ungefanyeje?