Makocha wote duniani wanaajiriwa on assignment basis.
Mclaren alishindwa kuwapeleka Euro Waingereza,wamemwondoa na sasa wanaye Cappelo.
Huyu bwana ameshindwa Ghana 2008 assignment yake ya mwisho ni World Cup RSA akishindwa aondoke.
Natofautiana na wale wanaofikiri kuwa tumefika hapa kwa juhudi za Maximo na wachezaji tulionao hawana uwezo.
Tujikumbushe back then 1980 tulipo qualify kwenda Lagos tulikuwa tunarank wa ngapi ktk FIFA?,Maximo hajatutoa shimoni bwana.
Wachezaji wetu ni wazuri sana lakini our very best players HAWASHIRIKISHWI.
TATIZO NI SPORTS ADMNISRATION hususani Kurugenzi ya Ufundi ya TFF.Wachezaji wanaochaguliwa ni wale watakao toa 10% ya mapato yao kwa viongozi waliowachagua,Maximo hachagui wachezaji peke yake kama mlikuwa mnafikiri hivyo hamkuwa sahihi.
Mfano Timu iliyokwenda Rwanda, wale vijana wa Copa Cocacola selection ile ilikuwa aibu tu.Vijana halisi waliachwa wakachukuliwa vijana wa viongozi wa michezo.Tunalijua hilo.Je?,hii ni timu ambayo unasema kesho ndio itakuwa timu ya wakubwa, unatarajia nini? .Mifano ni mingi ufisadi umetawala katika sekta hii ya michezo.
Bado nasema wachezaji wetu ni wazuri. nani amewasahau raha waliokuwa wanatupa akina Eddo Chumila,Hamza maneno,Rajabu Rashid "double R" ,Fumo,Frank Kasanga,OCD Njohole,Danny Muhoja,Issa Athumani,Octavian Mrope, Peter Mhina ,Juma Mgunda,Mwameja,Yassin Abuu Napil,Kassa Mussa,Ali Maumba,Sentahafu Mhando Mdeve,BEki mstaarabu Samli Ayub,je sports academy zilikuwepo kipindi hicho huu ni utapeli mtupu.Kumbuka Said Mrisho "ZICO wa Kilosa",Kitwana Selemani hao ni wachache wa mid and late 90's hatutaki kurudi kwa kina Boniface Mkwasa,"Homa ya Jiji" Makumbi Juma,"Golden Boy" Mogella,Athumani Chama "Jogoo" .
Tuache kuwakashifu na kutukana wachezaji wetu.
"Mwanafunzi mjinga au asiye na uwezo ni reflection ya mwalimu aliyemfundisha".
1.Tuache ufisadi wa kuleta nyasi bandia feki ambazo hazicomply na Specs zinazotakiwa.
2.Tuache kujuana.Kwani soka sasa hivi bwana mihela ipo kedekede ya NMB ,Serengeti.Tufuate vipaji mchangani tulipowatoa akina Chumila then tuwe na serious and REAL SPORTS ACADEMY.
3.Tuwe wazi ktk taratibu za kusource walimu wenye sifa.Tulikuwa na akina Hudson yuje mjerumani.Acha kina Victor.
Huyu Jamaa ni msanii.
Huwezi kwenda Brazil ukacheza mechi 5 huku ukifungwa idadi ndogo ya magoli kila mechi na nyingine utoedraw... then uende dakar upigwe goli 4.Pale kulikuwa na usanii wa hali ya juu.Maximo alitutafutia timu zisizo na uwezo makusudi asijichafulie rekodi yake.Amekuwa anafanya hivyo hata kwenye hizi trial matches zake.
Huyu jamaa ni msanii perse.Binafsi nasema akishindwa assignment yake ya mwisho yakutupeleka RSA, AONDOKE.