Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 129
Sitapangua kikosi tena - Maximo
na Dina Zubeiry
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbrazil, Marcio Maximo, amesema kwa sasa hatarajii kupangua tena kikosi cha timu hiyo.
Maximo, aliyasema hayo jana baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa jijini Dar es Salaam, akitokea nchini Yemen ambako Stars ilikwenda kucheza mechi ya kirafiki.
Ikiwa huko, Stars iliyo katika kampeni ya kusaka tiketi ya kucheza fainali mpya za Afrika kwa nyota wanaocheza ligi za nyumbani zitakazopigwa mwakani nchini Ivory Coast, ilifungwa mabao 2-1 na timu ya taifa ya Yemen.
Mbali ya kampeni hiyo, Stars pia inajipanga kwa kampeni za kusaka tiketi ya fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini na fainali za Mataifa ya Afrika nchini Angola mwaka 2010.
Mechi iliyo karibu, ni ile ya marudiano dhidi ya Harambee ya Kenya, itakayopigwa Jumapili, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Maximo alisema, ziara hiyo ya Yemen, ilikuwa ya manufaa kwa timu yake kwani aliitumia kupata nyota wanne watakaoongezwa kwenye kikosi chake kilichopo kambini kwa ajili ya mechi ya Jumapili dhidi ya Harambee Stara.
Maximo alisema ingawa mazingira ya hali ya hewa na staili ya uchezaji wa Yemen, ni tofauti na ule wa Stars, lakini vijana wake wamejifunza mengi.
Alisema, asilimia kubwa ya kikosi kilichokwenda Yemen, kilijaa wachezaji wa kikosi B kwa ajili ya kuwapima ili kuwaongeza kikosi cha kwanza.
Alisema, ukiondoa wachezaji wa Yanga na Simba, wengine wanatarajiwa kuanza mazoezi leo jioni kabla ya kuungana na wenzao.
Kuhusu mechi dhidi ya Kenya, Maximo alisema itakuwa ngumu kwani kila timu inahitaji kushinda ili isonge mbele, hasa Stars ambayo iilipoteza mechi ya kwanza.
Hata hivyo, alisema ana matumaini makubwa ya vijana wake kufanya vema kwani wachezaji walio wengi hususani wa Simba na Yanga, walikuwa na timu zao katika michuano ya kimataifa.
Mechi ya kwanza tulifungwa na Kenya, hivyo tutatumia siku mbili hizo kuwekana sawa na tuna imani tutashinda mechi yetu hiyo, alisema Maximo.
Source:Tanzania Daima