Sitamsahau Mama Wa Kambo!

Sitamsahau Mama Wa Kambo!

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
496
Reaction score
379
Wanaume kama hatuna sababu za msingi za kuachana na kuoa mke mdogo tuwe tunaacha au Tuwe makini sana! Sijajua ni umakini wa aina gani!!

Baba yangu mzazi alimuoa mama yangu miaka 40 iliyopita, mama ni mtu wa kaskazini yaan mchaga na baba ni mtu wa Mara tena ana kazi nzuri sana serikalini, mama yangu mzazi alifanikiwa kuzaa watoto 5 na baba yangu huyu, lakini katika hali isiyotarajiwa, siku moja nikiwa shuleni Buturi shule ya msingi huko Rorya nilipata habari za kunishtua sana, mmoja wa wakazi wa kijiji chetu cha Nyamagaro alikuja kututembelea wakati anaaga kuondoka kurudi kijijini tukamwambia, "Msalimie mama" yeye akajibu, nani kawaambia mama yenu yupo? mbona baba yenu kampiga sana na kamfukuza?

Loo!! niliishiwa nguvu sana, ndipo akaanza kutusimulia kuwa, baba yangu wiki iliyopita ya mwaka 2001 alikuja kijijini kutokea Buturi, alipofika kijijini alipita kwa shemeji yake yaani kwa mke wa kaka yake, ndipo alipoambiwa kuwa "mama yangu ana mahusiano na afisa mtendaji wa kata" mzee bila kutafakari kwa kina alipofika nyumbani akamwita chumbani na kufunga mlango wa chumbani kwao na kumfunga kamba mikononi na kuirusha juu ya dari na hapo akaanza kumchapa huku akitishia kumuua.

Aliyemwokoa mama ni mjomba wake mme wake anayeheshimika sana pale kijijini ndiye aliyekuja akamkuta mama tayari amevimba mwili mzima na damu zinamtoka ndo akaomba akandwe na maji ya moto, mama aliamua kuondoa kurudi kwao Moshi huko URU-SHIMBWE.

Wakati hayo yote yanatokea mimi nilikuwa darasa la saba pale shule ya msingi buturi. Mzee alipokuja kutoka kijijini, wakati anaelekea bafuni kuoga ndipo alipotuita, "Njooni hapa" Mama yenu ameondoka kwenda kwao, sijajua tatizo ni nini? alisema baba ambaye wakati huo alikuwa Makamu mkuu wa shule pale Buturi sekondari.

Kwa kweli iliniuma sana hadi sasa inaniuma sana, Baba aliamua kuoa mke mwingine huyu alikuwa ni binti tu aliyemaliza pale Maswa girls huyu binti kwao ni Busanga, mwanzoni ali-pretend kuwa mpole sana lakini kumbe!!! baadae mzee alipata uhamisho kwenda Arusha-wilayani Ngorongoro, wote tulihama, kufika huko ndipo mambo yalipokuwa machungu, kwanza mzee akiondoka kwenda safari-toka siku hiyo hadi mzee atakaporudi ni ugali-maharage tu, pili, hata kama una shida lazima kwanza umwambie yeye na yeye ndo atamwambia mzee, tatu, Mzee akipata mshahara anawaita watoto wa jirani kuja kumsaidia kuhesabu, nne, hataki tuwe karibu na mzee, tano, Alikuwa ana-change wanaume mara tu mme wake anapoondoa kwenda safari kikazi, alikuwa hataki tusome na anasema wazi wazi kuwa tunamaliza tu pesa bure hatutafika mbali.


Yeye alipata ZIro form four Maswa, Tulipofika Arusha mzee akampeleka Eckenford ili ali-sit paper la form four pia wakati huo huo anasomea Ualimu wa grade A, LAKINI vyote alishindwa akarudi nyumbani kuendelea kuwa mama wa nyumbani.

Siku moja tukiwa nyumbani hapo hapo WASO-NGORONGORO, mzee hakuwepo alikuwa Arusha mjini kikazi, hakununua chakula na wala hakupika, nilikuwa na njaa sana, ndipo nikategea ameenda kanisani nakumbuka ilikuwa alihamisi ya majivu, mimi niliingia ndani nikachota sukari nikaificha chumbani kwangu maana mimi nilikuwa nalala chumba cha nje ya nyumba ambapo ndipo kulikuwa na jiko, nikaficha sukari katikati ya chaga za kitanda, lengo ni kuwa usiku nipike uji ninywe nilale hadi kesho yake, aliporudi sijui alijuaje wakati nimetoka kwenda Loliondo sekondari maana tulikuwa tunaishi katika nyumba za sekondari pale nikakuta kikombe kipo lakini sukari haipo ila kuna mchanga tu! nikamuuza mdogo wake nani aliyeweka mchanga humo akasema hajui ila anahisi ni dada yake maana alimuona amebeba kitu anaingia nacho chumbani kwangu.

Ikumbukwe kuwa wakati hayo yote yanatokea nilikuwa form two shule ya sekondari Digo digo iliyopo kule samunge, na wakati wa likizo ndo nilikuwa nakuja hapa nyumbani Waso.

Vile vile, dada zangu wakati huo walikuwa wamepelekwa shule mwingine akipelekwa Dar es salaam na mwingine akipelekwa huko Rufiji, mmoja alikuwa tayari ameolewa na mwingine alibaki nyumbani yaani Nyamagaro, na mwingine akipelekwa Bugisi -huko shinyanga kusoma.

Siku moja nikiwa shuleni Digo digo, ghafla wazo liliniijia kuwa "kwa nini nisiende kwa mama"? kwa kweli nilianza kupanga safari huku nikitunza pesa nilizokuwa napewa kwa ajili ya matumizi-sh. 5000, au 10000 zote nilikuwa natunza, kipindi kile sijajua kwa sasa, Mamlaka ya Hifadhi ya wanyama Ngoro ngoro walikuwa wanaleta magari yao kuwachukua wanafunzi wa jamii ya kimasai na kuwapeleka makwao baada ya shule kufungwa, ni katika hali hiyo, ndipo na mimi nilipozama ndani ya gari na kupelekwa hadi mji mmoja hivi huko Ngorongoro kwa sasa nimeusahau jina ila Kuna baridi sana pale ila MARAMBO tulivuka na ukiwa ktk mji ule ziwa Natroni unaliona vizuri, nakumbuka tulifika pale muda wa saa 10 jioni na hakukuwa na gari la kwenda ARUSHA muda ule na hela ya Guest sikuwa nayo, niliamua kuomba dereva mmoja wa Lori lililokuwa na vyuma ndani yake tukalala mimi na rafiki yangu anayeitwa ANANIA ALBERT sasa hivi nasikia ni ASKARI, kesho yake asubuhi tulipanda gari hadi Arusha mjini na mimi nikaunganisha hadi Moshi.

Muda wote huo nilikuwa sipajui moshi ila nilisimuliwa wakati nikiwa Musoma kuwa Mama yangu mdogo huwa nafanya biashara ya nguo pale karibu na KCMC ni nje ya uzio wa hospitali, kwa hiyo ramani hiyo ndo niliyoitumia na jina lake nilikuwa nalifahamu sana, baada ya kufika pale moshi mjini nikapanda hiece za KCMC hadi kituo cha ndani pale KCMC nikashuka, nikaanza kuulizia wanapouza nguo nje ya KCMC Hospital, nikaonyeshwa kufika pale nikauliza "Namuulizia mama festo" nikaambiwa yule pale" kweli wanafanana sana mama yangu punde nikamwona mama yangu mzazi na yeye kumbe alikuwa pale kijiweni ila alikuwa ametoka kidogo, mara aliponiona akaanza kulia kwa mshangao sana ni kwa vipi nimefika?

Kumbuka kuwa nilitoroka wala sikuaga nyumbani mbali ya mkuu wangu wa shule na rafiki yangu mkubwa Mwalimu ERNEST SHAYO baadae alihamishiwa shule ya sekondari EMBARWAY muda huu sijui kama bado yupo hapo au la!

Baba nasikia alianza kunitafuta, kumbe alikuwa na namba ya simu ya mama mdogo ndipo alipompigia simu na kumuuliza kama nilikuwa moshi, mama mdogo akamwambia kuwa ni kweli nipo moshi. Nilikaa moshi mwezi mzima wa likizo na nikarudi Nyumbani ngorongoro-waso, bahati nzuri baba hakunipiga mbali na kuniuliza kama mama na bibi ni wazima!! ila yule mama mdogo yeye aliponiona alikuwa na wasiwasi kuwa labda mama yangu atakuwa amenipa dawa ili nimfanyie aondoke, marafiki zake walinieleza mimi nikawaambia kuwa wamwambie asiwe na wasi wasi kwani mama yangu kwanza hamjui, na mama yangu hawezi na hayajui hayo mambo labda kama yeye ndo anayafanya.

Mwaka 2005 baba yangu alipata uhamisho tena na kupelekwa Bukoba mjini pale, wakati huo mimi nikiwa form 4, waliniacha nikijiandaa na paper wao wakaondoka, baada ya paper nilirudi MUSOMA kusubiria matokeo yangu, kumbe baada ya baba kuona kuwa tayari nishapata mawasiliano na mama yangu alimtuma mtu aende moshi akamuombe mama yangu arudi Nyumbani, wa kwao mama walikataa wakitaka yeye mwenyewe yaan baba aende aombe radhi personally, naona alikuwa amishajua kuwa endapo angeenda angepigwa na shemeji zake, maana kipigo alichompa dada yao kilikuwa hakielezeki na mama alienda na kamba ilotumika kumfunga mikono, ilikuwa ni kamba nene sana.

Lakini baada ya mama kutafakari sana na kuwa alikuwa ameacha watoto ndipo alipoamua kurudi Kijijini Nyamagaro hadi sasa.
Matokeo yangu yalipotoka nilikuwa na 4 ya 27 lakini mzee alitaka kukataa nisiendelee kusoma, ilikuwa kama ndoto hivi bwana mmoja nimemsahau jina alipita pale nyumbani akanikuta aliponihoji maswali akamwambia mama kuwa ni vizuri nikaenda kimya kimya hadi BUKOBA kwa baba ili anisomeshe na muda huo huo huyu mama wa kambo alikuwa anatamba kuwa "kwa sasa hakuna pesa ya kunisomesha tena na hayupo tayari tena kuishi na mimi"

Mama yangu akaniambia kuwa nijiandae na safari kesho yake ili niende Bukoba kwa baba, nakumbuka alinipa sh. 25,000, nauli, kesho yake asubuhi nilipanda gari hadi tarime na nikapata basi hadi Mwanza na mwanza simu ilipigwa kwa baba mkubwa wa mwnza kuwa anipokee stand hapa mwanza wakati huo mimi sikuwa na simu, baada ya kufika Mwanza nilienda kwenye huduma ya simu ili kumpigia baba mkubwa kumuuliza yupo wapi? bahati nzuri nilimpata na tukakutana na kwenda hadi kwake, yeye akaenda Bandarini mwanza kukata ticket ili jioni niondoke bahati nzuri sana Mungu mkubwa pale kwa baba mkubwa nilimkuta ba mdogo wangu naye alikuwa anaenda Bukoba ku-report kazini ndipo serikali ilikuwa imetangaza na kuwapangia vituo vya kazi walimu kwa hiyo jioni nikaenda naye bandarini na tukapanda Meri ya MV-VICTORIA.

Asubuhi yake, meri ilitua nanga na bahati nzuri au mbaya Ba mdogo alikuwa na yeye ni mgeni Bukoba na alikuwa amewasiliana na Baba yangu mzazi kuwa ampokee pale bandarini, kwa hiyo asubuhi sana Baba akiwa na Ma mdogo walikuja na Gari ya KAZINI kwa baba kuja kumpokea ba mdogo, Kwa Mshangao sana baba aliponiona akashtuka sana mimi nilikuwa makini sana kumwangalia usoni, mke wake mdogo yeye hakuficha hisia zake alitamka maneno haya "Watu wengine wanakuja hata bila kuitwa" khaa! ...............itaendelea.......
 
siku hizi nimekuwa mjanja, nikiona story naangalia kwanza mwisho kabla ya kusoma, nikiona neno itaendelea natoka kimya kimya ikiisha ntarudi kusoma ikiwa nzima..
 
mama wa kambo ni mama mimi naye twapendana, huyu mtunzi alikuwa naana gani alipoimba hivvv
 
@B. G. Tantawi, aisee huyo Anania Albert namfahamu sana nahisi bado ni askari na mara ya mwisho alikuwa Dom.

BTW hii tabia yako ya kuleta hadithi nusunusu si nzuri bana.

Ila kwa kuwa ina elements za ukweli ngoja nkuvumilie hadi umalize ndo nikupe maneno yako!!!
 
@B. G. Tantawi, aisee huyo Anania Albert namfahamu sana nahisi bado ni askari na mara ya mwisho alikuwa Dom.

BTW hii tabia yako ya kuleta hadithi nusunusu si nzuri bana.

Ila kwa kuwa ina elements za ukweli ngoja nkuvumilie hadi umalize ndo nikupe maneno yako!!!

Mkuu ASante, kama una namba yake naiomba aise, hata mimi nilisikia kuwa yupo DOM ila cna mawasiliano yake, hii issue bwana nathibitisha bila shaka kuwa imenitokea ila kwa sasa namshukuru mungu sana.

Ngoja Mods waiunganishe nimishaimalizia tayari mkuu, ASante.
 
Back
Top Bottom