Sitakusahau

Sitakusahau

Habarini Wakuu!

"KWA HERI JOKA" Ulikuwa ni ujumbe wa simu kutoka kwa Mpenzi wangu Dayana. Ujumbe uliofungua akiba ya maswali mengi katika kichwa changu. "Kwa heri?" Nilijikuta narudia maneno ya ujumbe ule. Kwa heri ya nini. Anaenda wapi. Kufanya nini. Ulikuwa ni msururu wa maswali yaliyoshikana mithili ya gololi za shanga. Niliamua kumpigia simu lakini kwa bahati mbaya simu haikuwa na salio. "huuh!" Nilishusha pumzi kama mtu aliyekuwa amechoka. Nilitoka kwenda kununua vocha ili nipate kuwasiliana na kipenzi cha moyo wangu Dayana.

Hata hivyo nilipoweka vocha na kujaribu kumpigia nilipokea ujumbe kuwa namba yake ilikuwa haipatikani. Nilijikuta na hasira ambazo hata hivyo sikujua chanzo chake. " Ndio mambo gani haya'" Niliongea kwa ghadhabu nikiwa nimeikodolea macho simu yangu. Wasi wasi ulinipuliza moyoni mwangu. Mashaka yaliweka kambi nafsini mwangu. Mwili wote ulikufa ganzi nisijue cha kufanya.

Niliamua kuvaa nguo nakumfuta Dayana. Nilivaa chapu chapu mithili ya mwanajeshi wa Palestina aliyekurupushwa na sauti ya bomu. Hii yote ni kutaka kujua ni nini kimempata Mchumba wangu, Asali wangu, Kipepeo wa joka jeusi. Hata ingekuwa ni wewe lazima ungekuwa kama mimi. Embu fikiria kitoto kizuri ukipendacho kimetuma ujumbe kama huo bila maelezo yoyote. Lazima ungeingiwa na wasi wasi.

Kutoka nilipokuwa naishi mpaka alipokuwa anaishi Dayana hapakuwa mbali. Ulikuwa ni mwendo wa dakika ishirini tu. Mbele yangu ulikuwa ni mlango wa alipokuwa anaishi Dayana. Nilibisha hodi bila mafanikio. Niliamua kuipigia simu yake lakini haikuwa inapatikana. " My Dayana upo wapi?" Niliongea bado nikiwa naugonga mlango. Mara simu yangu iliita na kwenye kioo ilionyesha namba ambayo haina jina. Kuashiria ni namba ngeni. Nilitulia kwa kitambo nikijaribu kutuliza mtiririko wa mawazo.

"Hello, naongea na Joka" Sauti ya kike tulivu ilisikika baada ya kupokea simu.
"Ndio" Nilijibu
"Njoo hapa hospitalini Dayana amepata tatizo"
"Tatizo..." Simu ilikatika ikiniacha nikiwa nimechanganyikiwa. Nilianza kukimbia kama mwehu kuelekea hospitalini. Njiani watu walinishangaa, wapo walioniona huenda nimewehuka, wapo waliofikiri kuwa huenda ni jambo la muhimu nafuata, wengine walibaki na maswali kuwa ni nini kinanifanya nikimbie. Hakuma miongoni mwao aliyekuwa na jibu la uhakika.

Niliingia hospitalini kama kiberenge kisicho na mzigo. Nilianza kuitaa " Dayana! Dayana! upo wapi Dayana! Mmeo nimekuja" Niliangaza macho huku na huko nikitembea kwa kasi. Kila Mtu aliyevaa Koti jeupe nilimuuliza Dayana yupo wapi. Hata hivyo wengi wa madaktari na wauguzi hawakunijibu zaidi ya kuduwaa tuu.

Punde niliona Manesi waliovalia sare za kijani wakisukuma kitanda ambachp juu yake kulikuwa na mtu aliyefunikwa gubigubi na shuka jeupe pee. Moyo ulipiga paa! mithili ya mizinga ya bundauki. Niliwakimbilia nikipiga kelele "Mnampeleka wapi.... Mnampeleka wapi nyie" Hakika nilikuwa nimechanganyikiwa. Nilimshika Muuguzi mmoja shati lake nusura nilichane. Aligeuka na kukutana na uso wangu uliokuwa ukivuja jasho. "Mnampeleka wapi?" Nilimuuliza. Alishusha pumzi kisha kwa sauti ya unyonge alijibu "Tayari ameaga dunia, pole mwaya". Nilihisi kizunguzungu na hapo hapo fahamu zilinitoka.

Nilizinduka kesho yake asubuhi. Dayana haiwezekani. Dayana umeendaje. Sikuamini kama mimi ndiye ningekuwa chanzo kikuu cha kifo cha mtu nimpendaye. Mwanamke pekee aliyeufurahisha moyo wangu. Aliyenipa faraja nikapata matumaini. Aliyenipa mapenzi nikapata amani. Aliyenidekeze ukubwani nikakumbuka utotoni. Leo nimemuua mwenyewe. Ee Mola wangu nisamehe.

Zilikuwa ni kumbukumbu za Joka Jeusi. Kumbukumbu za miaka saba iliyopita. Kumbukumbu zilizokuwa kama jeraha kwangu. Mimi nisingekuwa hivi jamani. Nisingekuwa mtu wa kuhangaika kutafuta mtoto. Nilimshauri Dayana atoe Mimba hali iliyopelekea umauti wake. Nikapoteza bara na pwani. Yaani Nikampoteza Dayana wangu na mwanangu. Masikini Mimi, sasa ningekuwa na mtoto mkubwa tuu wa miaka saba. Lakini ona ninavyohangaika kutafuta watoto. Si Mimi si Mke wangu niliyemuoa na ambaye ninaishi naye. Wote hatuna uwezo wa kupata watoto.

Dayana mpenzi huko ulipo naomba unisamehe. Mwambie na mwanangu anisamehe. (Nilianza kulia kwa kwikwi) Mungu Baba nisamehe Nimetambua kosa langu. Ee Mola wangu nisikie.

Sitakaa nikusahau Dayana!

Jioni Njema

JOKAJEUSI
Pole sana joka jeusi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mtoa mada unaishi wapi nataka kuja na afande marwa haiwezekani ukatenda uzembe wa namna hiyo.
 
"Kwa heri Joka". Ujumbe uliobeba maneno hayo, alikutumia wakati anakata roho?

Ila simulizi nzuri mkuu, kuna mistari umeandika ya maneno mawili mafupi yanayofanana nimeyapenda sana!
 
Back
Top Bottom