Sitaki kuamini....

Sembeta jr

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
805
366
- Sitaki kuamini Tanzania yetu yenye kila aina ya neema na utajiri usio elezeka kama mlima Kilimanjaro, Mbuga za wanyama, Maziwa mpaka mengine tunataka nyang'anywa na majirani zetu (ref…ziwa Nyasa), mito, bahari, madini mengi tu kama dhahabu, almasi, tanzanite n.k, ardhi kubwa yenye rutuba achilia mbali mafuta na uranium:-

- Sitaki kuamini leo hii kuna watu ndani ya Tanzania wanashindia sh. 900 au chini ya hapo.

- Sitaki kuamini kuna familia pale masaki wanakula million moja kwa siku (proved) wakati pale buguruni kuna familia wankula shilingi 900 tu (proved).

- Sitaki kuamini kuna watu wanatumia mpaka milioni tisini katika harusi tu wakati kule kwao Singida vijijini wanatumia maji ya kisima tena ukipata ndoo moja kwa siku unamshukuru mungu.

- Sitaki kuamini Serikali inaweza kuanunua mashangingi mapya wakati kuna shule hazina madawati, wanafunzi wanakaa chini tena zipo mijini kabisa mfano S/m Chamwino Morogoro achilia mbali huko vijijini.

- Sitaki kuamini kamati ya Olympic nchini au wanaohusika na michezo walishindwa kupeleka wanamichezo kule London kushiriki Olympic na wasiweze kurudi na medali hata moja

- Sitaki kuamini kwamba neema na utajiri wote aliotupa mwenyeenzi mugu ashindwe kutupa vipaji kama vya kina Bolt

- Sitaki kuamini kwamba Usain Bolt ni binadamu mwenye kasi zaidi dunian au kuliko yeyote hapa kwetu Tanzania wakati tuna watu wengi tu wenye sifa za kukimbia sana tu kama watu wa kaskazini

- Sitaki kuamini wakenya wanaweza pata medali kule Olympic sisi tusipate wakati ni majirani zetu kabisa kabisa

- Sitaki kuamkini wahaya ndio kabila lenye wasomi wengi pia wana umoja na mshikamano sana tu wakifuatiwa na wachaga hata wewe unayesoma ni shahidi mana hata hapo ulipo unawaona tu, halafu makabila mengine washindwe kufanya hivyo kwa nini?

- Sitaki kuamini wewe muislam uliye funga leo unakwenda kwako kula futari zaidi ya saba katika mkeka (tunaita draft) wakati kuna muislamu mwenzio amefunga na anaftari vipande vya mihogo ya kuchemsha na maji tu

- Sitaki kuamini kila kinachotokea katika Tanzania yetu ni mipango ya mungu…sitaki….sitaki….

- Sitaki kuamini nilichoandika hapa hakuna hata kimoja chenye ukweli na kinachokulenga wewe unaye soma.

- Sitaki kuamini kuna watu watakuja na kukejeli post hii

- Sitaki kuamini …..……
 
Transporter mimi napita tu...... nitarudi baadaye..
 
Yooote haya uliyoandika yako vere common hapa Bongo! Kwa mawazo na uzalendo wako, nini kifanyike? Otherwise leta issue mpya kijana.
 
Hapa Bongo mkuu hatuishi kwa kuamini, tunaishi kwa kuthubutu na magumashi. Ukitaka kuamini hamia Vatican au Makkah.
 
- Sitaki kuamkini wahaya ndio kabila lenye wasomi wengi pia wana umoja na mshikamano sana tu wakifuatiwa na wachaga hata wewe unayesoma ni shahidi mana hata hapo ulipo unawaona tu, halafu makabila mengine washindwe kufanya hivyo kwa nini?

usomi wa vitabuni, ungetuletea walichokifanya kwa elimu zao ningekuona wa maana sana.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom