SITA WAUAWA KATIKA SHAMBULIO
LA KUJITOA MHANGA NIGERIA
Mlipuaji wa kujitoa mhanga ameua watu wasiopungua sita katika chuo
kikuu kimoja katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria. Watu wengine
kadhaa wamejeruhiwa. Mlipuko huo umetokea wakati makundi makubwa ya
wanafunzi wamekusanyika kutazama matokeo yao kwenye ubao wa matangazo.
Watu walioshuhudia wamesema wameona miili ya watu imetapakaa. Hili ni
shambulio la tano mjini Kano tangu siku ya Jumapili. Takriban
mashambulio matatu yamefanywa na walipuaji wa kujitoa mhanga wa kike.
Waandishi wa habari wanasema
huenda kundi la Boko
Haram linahusika na mashambulio hayo.
source:
Salim
Kikeke