Sisi Wamachinga tumemkubali Rais Magufuli

Sisi Wamachinga tumemkubali Rais Magufuli

hongera mwenzetu kwa maisha yako kuwa safi chini ya utawala huu. huku mtaani hali sio shwari....
 
Amani ya bwana iwe nanyi.

Mimi kama mfanyabiashara wa kimachinga tangu awamu ya mzee mkapa, naomba nichukue nafasi hii kuipongeza sana serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli.

Kabla ya awamu ya Rais Magufuli kuwa Machinga ilikuwa ni adhabu kubwa.
Vipigo, kuwekwa ndani na kuchukuliwa vitu na mgambo ilikuwa ndio maisha ya wamachinga.!

Leo hii wamachinga tunafanya biashara kwa kujiachia katikati ya mji kama mitaa ya kongo na makoroboi! Tuseme nini waja wako ee bwana??
Chini ya utawala wako maisha ya wamachinga yameboreka sana na biashara hii, sasa inatambulika rasmi.

Rais Magufuli pokea salamu zetu sisi wamachinga na tunakuahidi ushindi wa kishindo uchaguzi wa 2025.


Sent using Jamii Forums mobile app
sisi bodaboda, mama ntilie, wanafunzi wa vyuo vikuu na wakulima hatumtaki hatakumsikiliza,amalize tu hii 5 yake
 
Umachinga siyo kazi, ni matokeo ya kushindwa kwa mipango ya serikali ya Tanzania. Ni upumbavu kwa watu kujivunia umachinga. Hakuna mipango, wanachotaka ni kuchuma tu
Machinga wapo duniani kote, tembea uone siyo kushinda umejifungia hapo ufipa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na keel
Umasikini wako unatuhusu nini sisi,
Kushindwa kununua sukari umeona ni jambo la maana sana kuja kujianika hapa?

Sisi tunapambana na hali zetu kwa kutandaza bidhaa barabarani na wewe pambana na hali yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kweli mnapambana na hali yenu. Hata ya kesho hamjui itakuwaje. Maisha vululuvululu. Mungu anawaona.
 
Sema Mimi machinga acha kutumia wingi,siku hizi naona vichaa mnazidi kuongezeka hapo Lumumba bk 7
 
Uko sahihi maana amewaacha mfanye biashara kila kona hata maeneo ambayo hapo awali yalikuwa hayaruhusiwi kisheria. Lakini zaidi mmefanikiwa kufanya biashara bila kulipa kodi, na waliokuwa wanalipa kodi sasa hivi wanafunga biashara. Hongera zenu kwa kum Win Mhe Rais ila naendelea kujifunza madhara yake pia kwa Taifa kama yapo!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi huku tunatafuta pa kulala baada ya bomoabomoa. Hongera yako wewe usiye na nyumba.
 
Back
Top Bottom