Kwani wewe ukitongoza huwa unamwambia?
Kwani wewe ukitongoza huwa unamwambia?
Umemaliza kila kituKwa mila na desturi zetu, kabla ya mwanamke hajaolewa na au mara tu anapovunja ungo hupewa mafunzo maalumu
yanayojulikana kama unyago, msondo, nk. Katika mafunzo haya mwanamke anafundishwa namna ya kuishi na mume,
kumtunza mume na watoto, nakadhalika. Mwanamke hatarajiwi kuwa sababu ya fadhaa, wasiwasi, au hasira ya mumewe, hivyo hatarajiwi kumwelezea mumewe juu ya yeyote anayemtongoza au mahusiano yake ya siku za nyuma. Kikubwa anachotarajiwa ni kuwa mwaminifu kumkataa yeyote anayemtongoza na kutokujiweka katika mazingira ya kutongozwa kwani mwaname hutongoza anapoona kuna mwanya/dalili za kufanikiwa kama akijaribu. Mwanamke ambaye kila kukicha anamueleza mumewe kuwa fulani kamtongoza basi hajafuzu mafunzo ya unyago, atamfanya mumewe kuwa na wasiwasi wakati wote na kushindwa kufanya kazi, pia atamgombanisha na marafiki, jamaa na ndugu zake. Mwanamke ukijiweka katika mazingira ya kutongozwa, mfano kujichekeshachekesha, kuombaomba ofa, kukubali mialiko isiyo ya kazi wala biashara, kupenda sana kusifiwa kuhusu sura na umbile lake,kupenda sana kuwaelezea watu kuhusu madhaifu ya mumewe, na kugawa ovyo namba yake ya simu ni baadhi tu mazingira yanayotoa mwanya wa kutongozwa.
Wanaume tunajua kuwa kuna mwanamke ambaye hata kama unamtamani kiasi gani lakini kila ukimwangalia usoni huoni uwezekano/nafasi ya kukubaliwa, hivyo hujikuta ukiahirisha kila mara wazo la kumtongoza.
Kwa mila na desturi zetu, kabla ya mwanamke hajaolewa na au mara tu anapovunja ungo hupewa mafunzo maalumu

ndio.Kwa hiyo huwenda wake zetu pia wanatongozwa lakini hawatuambii tu