Sisi ndio kizazi kinachohusika. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sisi ndio kizazi kinachohusika.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by dekleinson, Oct 11, 2012.

 1. d

  dekleinson New Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=&amp]Zawadi pekee kutoka kwa viongozi ni sera nzuri zenye kumwezesha yule wa kipato cha chini huku zikijaribu kumsimamisha yule wa kipato cha kikubwa. Ukijenga kiwanja au daraja kwamwe haiwezi kumnufaisha maskini hali hawez kuingia au kupita. Tajiri huangalia ya mbele na hufanikiwa kwa kumwibia maskini.[/FONT]


  [FONT=&amp]Mfumo wa ubepari ulibuniwa kukidhi malengo ya Ulaya huku ukilenga kuny’ang’anya alicho nacho MWAFRIKA, sera nyingi za wakomavu hawa wa ubepari kama Free Trade (biashara huru) zimelenga kumwibia mwafrica kwani hazitaji ni kiwango gani cha biashara huru, pia kuangalia yupi ana nini na kipi cha thamani kinachohitaji kupewa kipaumbele ili mmoja asiibiwe. Hakuna sera ya ubepari inayomtazama mny’ang’anywa kwa jicho la huruma lenye upendo wa kumsaidia. Kwangu mimi naona mfumo wa ubepari kama unakaribia mwisho kwani Africa ni bara linalopata akili kila kukicha huku watu wake wakihangaikia mabadiliko kwa kasi. Mabara 5 hayatoweza kuendelea kwa mfumo 1 huku kila 1 akijua mbinu za kuutumia umletee maendeleo na kwa upande wa pili ukimwathiri mwenzake. Hii italeta mgongano na kupelekea kila mtu aunde mfumo mpya utakaomnufaisha yeye, kama bado mwafrica ataendelea kulala au ataridhika na hapo atakapokuwa amefikia si budi tutaendelea kunyonywa kwa mfumo mpya ambao utatungwa na wao wenyewe ukiwa na sera za unyonyaji katika sura ya usawa.[/FONT]
  [FONT=&amp]Mambo makubwa yaliowaondoa waafrika kiu ya maendeleo kwa njia za makaratasi na akili ya kujiendesha ni UDINI, UKABILA. Wakati nchi kama Rwanda zikipata maendeleo kwa kuua sumu zinazosababishwa na vitu hivi, nchi nyingine zimeendelea kukuza ubaguzi ndani ya mambo haya 2 na kupelekea utengano unaositisha maendeleo, ni lazima tukubali mafanikio ya Rwanda na tukiri wao ni mfano mzuri kwetu kwani wamewahi (muda) kupita pale ambapo nchi nyingi hazijapita (zinaelekea huko, kwa sisi tunahitaji kuwahi kuizuia sumu hii kabla haijasambaa) na nyingine zikiwa katika vuguvugu hilo kama Kenya, Somali, Sudan n.k. wengi wetu hatuelewi nini tufanye kwa sababu hatusomi historia yetu na hatujihangaishi kuisoma, kuijua chimbuko lake na kuifananisha na za wenzetu, kujua ni nini tunahitaji na wapi au njia zipi tuzitumie kukipata.

  Hatuhitaji bunduki kuendelea kutoana roho, wala misaada iendelee kutupumbaza, tunahitaji kuunganishwa na kuwa na viongozi wazuri wenye sera nzuri zitakazotuwezesha huku zikipambana na sera za wazungu zenye silaha zote za kutupora.
  Idadi yetu ni rasilimali tosha kama tutafanya kazi kwa bidii na uzalendo. Sabsitute wa future plan yetu ni kizazi kijacho kitakachokuzwa kwa elimu itakayobuniwa na sisi Waafrika wenyewe zikilenga ukombozi kijamii, kisiasa na kimaendeleo, hatuhitaji demokrasia ya wapenda maendeleo yao wenyewe, waroho na walafi wa mali na kutukuzwa. Itakuwa ni kazi bure kama tutakosa wazalendo wa kutuongoza ndani ya demokrasia safi.
  We LOVE you AFRICA, soon utang’ara na kuwa na thamani kama maji jangwani. [/FONT]
   
Loading...