Sirro: Marufuku kuuza mapanga, mishale kwenye foleni

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Dar es Salaam. Jeshi la polisi limepiga marufuku uuzaji wa silaha za jadi kama panga, mishale, manati, visu pembezoni mwa barabara nyakati za foleni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwekuwa na vitendo vya kialifu vikifanyika kwa baadhi ya wafanyabiashara hao pia ni hatari kwa hali ya usalama wa wananchi.

“Biashara hii imeshamiri kwa kasi katika barabara ya Nyerere, Tazara na kwenye mataa ya Chang’ombe na Gerezani huwa wanawaibia watu kwenye magari binafsi na umma vitu kama pochi, kompyuta mpakato, saa na simu za mikononi,” amesema Sirro.

Chanzo: Mwananchi
 
Nilishuhudia mwenyewe maeneo fulani kulikuwa na ugomvi wa wanawake wawili sasa wakati wanapigana mara akapita jamaa amepanga visu kwenye baiskeli basi ghafla mmoja kati ya wale waliokuwa wanapigana akaenda kupora kisu kimoja... kilichotokea hapo!!!
 
Vp na wale wanaosafisha vioo vya magari kwenye feni?, maana nao wamekuwa kero, wanalazimisha kuosha usipompa hela anakichafua kioo chako, ningeona amalozane hao kwanza, manake mtu anaweza kujifanya anakusafishia kioo kumbe anania ya kukuibia kama ilivyo nchi nyingine.
 
Dar es Salaam. Jeshi la polisi limepiga marufuku uuzaji wa silaha za jadi kama panga, mishale, manati, visu pembezoni mwa barabara nyakati za foleni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwekuwa na vitendo vya kialifu vikifanyika kwa baadhi ya wafanyabiashara hao pia ni hatari kwa hali ya usalama wa wananchi.

“Biashara hii imeshamiri kwa kasi katika barabara ya Nyerere, Tazara na kwenye mataa ya Chang’ombe na Gerezani huwa wanawaibia watu kwenye magari binafsi na umma vitu kama pochi, kompyuta mpakato, saa na simu za mikononi,” amesema Sirro.

Chanzo: Mwananchi

Wakauzie wapi?
 
Vp na wale wanaosafisha vioo vya magari kwenye feni?, maana nao wamekuwa kero, wanalazimisha kuosha usipompa hela anakichafua kioo chako, ningeona amalozane hao kwanza, manake mtu anaweza kujifanya anakusafishia kioo kumbe anania ya kukuibia kama ilivyo nchi nyingine.
Tena wale wa moroco ndio wanatisha kbs..vijana wakubwa wale ni vibaka tu..ts dangerous
 
Back
Top Bottom