Siri yafichuka: CCM, Serikali na Bunge katika hali tete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri yafichuka: CCM, Serikali na Bunge katika hali tete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paparazi Muwazi, Feb 3, 2012.

 1. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Siri yafichuka: CCM, Serikali na Bunge katika hali teteIkiwa zimebaki siku mbili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuadhimisha sherehe za miaka 35 tangu kuzaliwa kwake hali katika chama hicho ni tete.Mivutano ya wazi na ishara za kushindwa zinazidi kujidhihirisha huku uwajibikaji wa pamoja ukipotea katika miongoni mwa chama hicho, serikali na wabunge wake inazidi kuongezeka.Kukataliwa kwa hoja mbili za serikali jana kwa wabunge wa chama hicho kuunga mkono hoja za kambi rasmi ya upinzani inayoongozwa na CHADEMA ni kati ya matukio ya wazi.Vyanzo toka ndani ya CCM vinaaleza kuwa uamuzi wa wabunge wa chama hicho ‘kuasi’ unatokana na kauli za Rais Kikwete kupitia kwa ikulu na kupitia CCM kuwageuka wabunge hao katika makubaliano waliyofikia katika kikao kati ya mwenyekiti huyo CCM kilichofanyika Dodoma mwishoni mwa mwaka jana.Katika mkutano huo Rais Kikwete aliwapongeza wabunge kwa kupitisha muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba na kuwapa kazi ya kwenda kutoa elimu juu ya sheria hiyo kwa wananchi, sambamba na kukubali uamuzi wa Spika wa kuongeza posho za vikao kwa wabunge.“Tumeamua kuionyesha serikali kwamba bunge ni chombo chenye nguvu, Rais Kikwete ametegeuka katika suala la posho na kufanya wabunge ndio tuonekane tumepandisha wenyewe posho bila ridhaa yake. Tutakaa mambo yao wajue kwamba tumeshikilia mpini, na tuweze kurejesha imani kwa wananchi”, alisema mbunge mmoja machachari ambaye hakutaka kutaja jina lake kuhofia mikakati yao kukwama.Kwa mujibu wa mbunge mwingine amesema kwamba wabunge wa chama hicho katika kikao chao cha kamati ya wabunge cha jana walimbana Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu mgomo wa madaktari wakieleza kwamba hali imekuwa mbaya kutokana na udhaifu wake wa kiutendaji. Hata hivyo, baadhi ya wabunge wamemlaumu Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai kwa kuungana na wabunge wa upinzani katika kuibana serikali. Awali katika kikao cha jana wabunge hao walikubaliana kwa Spika atumie kila mbinu kauli ya mawaziri isijadiliwe ili kuweza kuilinda serikali. Hata hivyo kufuatia muongozo ulioombwa na John Mnyika akitaka bunge litimize wajibu wa katiba wa kuisimamia serikali na kueleza kwamba serikali ni watuhumiwa ikiwemo waziri ambaye anapaswa kuwajibishwa hivyo wabunge wachukue nafasi yao, Ndugai aliungana naye na kuagiza Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ichukue hatua kwa haraka.Katika mkutano wa leo unaoendelea hivi sasa mvutano mkubwa umetawala huku wabunge walio wengi wakitaka maelezo toka kwa serikali kwa kuleta hoja zenye kasoro katika bunge na hivyo kufanya wabunge washindwe kutetea hoja za serikali. Wabunge hao wametaja mifano ya hoja hizo kuwa ni Azimio kuhusu Muswada wa ushuru wa Bidhaa liliwasilishwa na Waziri wa Fedha Mustapha Mkullo na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali yote ikiwa imewasilishwa na serikali jana. Huku wengine wakitaja muswada wa marekebisho ya sheria ya udhibiti wa fedha haramu uliojadiliwa leo ambao umeliingiza bunge katika kashfa ya kupitisha kifungu cha sheria kilichowasilishwa na Mbunge wa Ubungo cha kuongeza ukubwa wa adhabu kwa watakaobainika kufanya makosa yahusuyo fedha haramu kwa sheria kusomwa kwa mara zake zote tatu, halafu baadaye Mwenyekiti wa Bunge kutangaza kwamba ilipitishwa kimakosa na hivyo kusema anafuta maneno yake kwenye hansard aliyoyasema wakati bunge lilipokaa kama kamati.Katika suala hilo Serikali imejitetea kuwa siyo makosa yake bali ya Mwenyekiti wa Bunge aliyetajwa kwa jina moja la Mabumba kushindwa kuwaongoza wabunge. Hata hivyo mwenyekiti ametetewa na wabunge kutoka Zanzibar ambao wamesema kosa ni la wabunge wa CCM kwa kuitikia ndio bila kujua athari za kifungu ambacho walikipitisha. Kikao hicho kinatarajiwa kuendelea mpaka usiku zaidi kwa kuwa mvutano mkali zaidi unatarajiwa wakati wa kujadili msimamo wa chama hicho kuhusu muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba.Mivutano hiyo miongoni mwa wabunge wa CCM vinara wakiwa ni viongozi waandamizi katika chama hicho, bunge na serikali kunadhihirisha hali tete huku turufu ikiwa kwa Rais Kikwete ambaye anatarajiwa kuzungumza na wabunge hao na pia kufanya mabadiliko katika baraza mawaziri hivi karibuni. PM
   
 2. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Ni vigumu sana kusoma maandishi yako, fanya uhariri
   
 3. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  error 604 try again!
   
 4. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ukweli mtupu
   
 5. O

  OLEWAO Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Niliwakumbusha watu siku chache zilizopita kuwa utawala ukifitinika hauwezi kusimama!CCM hawawezi tena kutawala kinachosubiriwa ni muda tu ufike yatimie. Watatoka hata kwa kuanzisha wao wenyewe. Tusubiri tuone.
   
 6. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Haya ni mawazo yako au vipi mbona maelezo yako sio realistic
   
 7. c

  cholo Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  at work
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  ufalme umefitinika, kamwe hautapona!!!
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
 10. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Plz edit tukusome
   
 11. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kila nikimkuta mtoto njiani namjulisha chadema ndiyo serikali,sio magamba.
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Naona Shehe Yahya Husein,yule mtabiri wa nyota Afrika mashariki na kati amefufuka
   
 13. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naskia wabunge wamepania kukwamisha hoja binafsi za January na Zitto wanazotarajia kuziwasilisha bungeni kisa wamepinga posho. Wabunge wanawasubiri kwa hamu ili wawakomoe.
  Nashindwa kuelewa tuna wawakilishi wa aina gani wanaojali pesa kuliko maendeleo ya taifa!ikiwa kweli nitawashangaa sana
   
 14. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #14
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eti siri. Haya bhana endelea kutujuza.
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Karne ya thred za madudu ndio hii.hakuna hoja apa.lakini utapata wajinga wenzako watakuunga mkono ambao wana comment bila kusoma
   
 16. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Mkuu, ungefanya editing kidogo kwenye MS Word na kuweka paragraphs na spacing ingetusaidia sana.
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  sasa wewe ndugu unafikiria kutumia kiungo gani cha mwili wako???????????kwa nini USIMPONGEZE RAIS KWA KUKATAA KUSAINI UFISADI WA POSHO KWA WABUNGE BADALA YAKE UNAMLAUMU?????????
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kwanza una mwandiko mbaya sijui mwalimu wako alipata shida kiasi gani kukufundisha
   
 19. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #19
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kama huna la kuchangia kaa kimya usiwaite wenzio wajinga!
   
 20. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #20
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Tutasikia mengi mwaka huu
   
Loading...