structuralist
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 1,230
- 907
Imeripotiwa kuwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani jijini dar limekusanya zaidi ya bilioni 1 kwa mwezi wa pili.
Taarifa hii imepokelewa na wengi kama habari nzuri kwakuwa ni kiashiria kuwa mapato sasa yanakwendda serikalini na sio mifukoni mwa asikari kama.hapo ilivokuwa mwanzo.
Hata hivyo nimegundua kuwa hali hiyo imesababishwa na mabadiliko ya matumizi ya barabara ambayo yamefanyika bila wadau wengi kuwa na taarifa sahihi juu ya matumizi yake.
Katika taarifa ya habari ya Azam two wameonesha.namna madereva walivokuwa wakijichanganya na walituzwa faini.
Kwa hali ilivokuwa madereva wengi walikuwa wakilalamikia kutokuwepo kwa elimu ya kutosha...
Hali hii imeonesha wazi kuwa kuna idadi kubwa sana ya madereva walopigwa faini kwa kosa la kutofuata utaratibu mpya wa matumizi ya barabara jambo ambalo kimsingi limesababishwa na elimu duni juu ya mabadiliko hayo.
Licha ya kuwa kamanda Sirro alisema sio lengo lao kukusanya mapato mengi kwahiyo hawatozi faini ili kupata fedha nyingi bali kurekebisha makosa lakini nadhani inawezekana "implicitly" wamelenga kukusanya mapato zaidi na ndio maana wamekomaa sana na faini kwa madereva wasiofahamu matumizi ya sasa ya barabara badala ya kujikita zaidi kwenye kutoa elimu.