maharage ya ukweni
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 1,493
- 3,382
Kwanza Achana na akili za mchana sio kila unalo liota linakuwa la kweli nyingine huwa ni fikra ulizo nazo we mwenyewe huwa zina tabia ya kujirudia rudia.Pili Mungu hana uhusiano wowote na rupia ukitaka kujua vizuri kuhusu rupia tafuta watu wanaijua rupia watakuelezea mambo mengi usiyo yajua juu ya rupia.Tatu upatikanaji wa rupia ni wakimazingara ndiyo maana huwa inauzwa bei ghali kwa sababu haipatikani kiurahisi.Once again Mungu hana mahusiano ya aina yoyote na rupia,Hongera kwa kupata kazi ambayo ni ngumu kuipata.Rupia pamoja hela fulani za zamani ambazo zinatafutwa sana na watu hata kwakununuliwa kwa mabilioni ya fedha kuna uhusiano fulani na baraka za kutoka kwa mungu.Hili swala nalizungumzia kwa ushahidi ambao umenitokea baada ya kuota nimeokota rupia kwenye mchanga,niliota mara mbili mara ya kwanza niliota nimeokota rupia baada ya kuingiza mkono wangu na kufukua kwenye mchanga mwingi.Siku iliyofuata ninilipewa kiasi kikubwa cha pesa ambacho nilimuomba tajiri mmoja mkubwa mionogoni mwa matajiri hapa Tanzania.
Mara ya pili niliota niko msikitini nasubiri kuswali jamaa na nilikua nina msongo mubwa sana wa mawazo kutokana na maisha yangu kua magumu na wala hakuna mtu wenye uwezo katika familia yangu ambaye ana nia ya kunisaidia ili nipate nafuu ya maisha.Basi nilivyotoka msikitini nje nilikutana na mtu sio mzungu,mwarabu,muhindi wala mchina basi nikamsalimia baada ya hapo yule mtu akanipa rupia tatu moja iliyokua juu ilikua na picha ya Eagle basi nikawa nazishangaa sana zile hela huku nasema hizi hela zinatafutwa sana na mtu ukizipata unakua tajiri nikiwa nimeinama naziaangalia zile hela kwenye kiganja changu cha mkono.
Nikasikia yule mtu ananiambia usishangae wewe nenda,yule mtu na yeye alikua anatoka msikitini na kuelekea kule ambako mimi naelekea.Basi nilivyonyenyua kichwa niende nikaangalia mbele lakini kilichonishangaza yule mtu sikumuona na mbele yangu hakukua na nyumba wala kichochoro na hata yule mtu angekua anakimbia kama Usain Bolt bado ningemuona.Basi kuanzia nilivyoamka mpaka leo hali yangu ya kimaisha inaonesha ntakua na maisha mazuri sana baadae inshaalah kwani nimepata nafasi ya kazi ambayo kuipata ni vigumu sana
Kwa ndoto hizi mbili nimegundua kua kuna uhusiano mkubwa sana kati ya baraka za mungu na rupia kwani mimi sio mshirikina,swala tano na sunnah juu.pia nimegundua nina nguvu sana ambazo mungu amenijaalia na kuna watu wamegundua kua nina future nzuri ndio maana nilikua najiuliza mimi masikini lakini mbona nafanyiwa sana fitina,nachukiwa bila ya sababu za msingi mpaka na watu ambao maisha yao ni mazuri sana.Jamani nawashauri dunia isitudanganye tumrudie mungu kwani maisha baada ya kifo yapo na mungu ndio kila kitu,riziki anatoa mungu na akisema kua basi inakua na hakuna ambaye anaweza uzuia
Ndugu yangu hujanielewa ninachomaanisha ni kwamba kuota umeokota rupia ni ishara ya kupata pesa au mafanikio makubwa kwenye jambo fulani ambalo unalifanya.Sikulazimishi uniamini kwani jambo hili nimelielezea kwa ushahidi ambao ninao na kwasasa kazi niliyoipata na digirii yangu ya lower second class ni uthibitisho wala sisubiri mtu aniamini.Pia napenda kukufahamisha kwamba mama yangu mzazi,mke wangu na wadogo zangu wameshaamini kwamba nina kipaji ambacho nimejaaliwa.Kwasasa nimeamua kutoa taarifa kwa wengi kwani kuna baadhi ya mambo ambayo ninayoyaota na yanatokea hayaihusu familia yangu.Hivi hizi adacadabra za rupia mtaziacha lini?
Kuota umeokota rupia ni ishara na wala sio utaokoa rupia,kwamfano ukiota umeokota rupia basi hilo jambo utafanikiwa kwa mara moja na kwisha.Kama kuna mtu ulimuomba hela halafu usiku ukaota umeokota rupia basi siku inayofuata au ndani ya wiki yw siku inayofata atakupa lakini hapa inahusisha kiasi kikubwa cha pesa.Halafu kama ukiota umepewa rupia tatu basi utapata mafanikio yenye kuendelea,katika hili kuna ishara nyingi sio lazima uote umepewa rupia.Kwani unaweza kuota umeona kitu ambacho ni vigumu sana kuviona.Hongera sana kwa kufanikiwa japo katika hadithi yako ya kufikirika hujatuambia hizo rupia ulizifanyia nn au kitendo cha kuwa nazo tu ndo sababu ya mafanikio hayo ?
Kijana umekurupuka na wala hujanielewa ninachomaanisha ni kwamba rupia ni ishara so ukiota umeokota au umepewa basi ni ishara ya kupata jambo la kheri sana.Ukiota umeokota rupia moja basi hilo jambo mafanikio yake sio yenye kuendelea,kama ulimuomba mtu kiasi kukubwa cha pesa basi atakupa.Lakini ukiota umepewa rupia tatu na mtu ambaye humfahamu au kama unamfahamu ni tajiri mkubwa sana basi utapata mafanikio yenye kuendelea.NB;sijakurupuka kuandika hii thread na wala sihitaji kua mtabiri.Ila haya mambo ninayoota yamefikia kiwango ambacho nimeona bora niwe natoa taarifa tu,nimeamua niwe nasema ili nipate nafuu kwani nimekua nawaza sana kwanini nakua na hii hali na nimeona kwakutoa taarifa itanisaidi kupunguza mawazo maana hua inafikia kipindi natumia mda mwingi sana kujiuliaza na kupata msongo wa mawazo.NB;Sio lazima uote umeokota rupia kwani kuna ishara nyingi sana na ishara hizo hua ni vitu ambavyo ni vigumu sana kuviona au kuvipata na rupia ni miongoni mwa ishara.NB;2:Niko hapa sina nia ya kupata wateja kwani mimi hii sio kazi yangu ya kuniingizia kipato na wala haitakua kazi yanguAmakweli ndio maana umejiita maharage ya ukweni, bado unafikila za kupata utajili kupitia Rupia!.
kama huna habari sasa hivi niko ofisini kwangu nakula kiyoyozi yaani bonge la ofisi niko peke yangu,nimeshapiga chai safi,maziwa na mchana leo kuna ratiba ya biriani.Hapa nilipo nasubiria mafaili niyafanyie kazi ndio maana nimepata mda wa kuchati.Mimi nimesoma na digirii yangu inanisaidia na napiga swala tano na sunnah juuMatapeli ya namna nyingi ya kutafuta wateja.!
Umemfumbua macho kidogo naona alitaka kumhusisha Mungu na mambo ya kishirikina tangu lini Mungu akaibariki pesa kwa namna kama hiyoKwanza Achana na akili za mchana sio kila unalo liota linakuwa la kweli nyingine huwa ni fikra ulizo nazo we mwenyewe huwa zina tabia ya kujirudia rudia.Pili Mungu hana uhusiano wowote na rupia ukitaka kujua vizuri kuhusu rupia tafuta watu wanaijua rupia watakuelezea mambo mengi usiyo yajua juu ya rupia.Tatu upatikanaji wa rupia ni wakimazingara ndiyo maana huwa inauzwa bei ghali kwa sababu haipatikani kiurahisi.Once again Mungu hana mahusiano ya aina yoyote na rupia,Hongera kwa kupata kazi ambayo ni ngumu kuipata.
Ndugu yangu usidhani mi mjinga kama elimu nina digirii moja nama njaa hela ya kula mimi na mke wangu napata,nimeandika thread coz ndoto ninazoota asilimia tisini hua zinatokea kweli tena naweza kuota leo halafu hicho kitu kikatokea baada ya wiki,mwezi,miezi au mwaka na kikitokea kitu ambacho nilikiota kwenye ndoto basi ghafla lazima ntaikumbuka ndoto ambayo niliota hata kama umepita mwaka.Tatizo wengi mmezoea kwenda kwa waganga kumbe ukichukia na kuacha kutenda machafu unakua na mawasiliano mazuri na malaika wako ambao mungu amekuwekea wakulinde pamoja na kukufahamisha mambo fulani ya ghaibu.NB;mimi sio mganga wala mshirikina na wala sina nia ya kupata pesa kwa njia hii coz nina kazi yangu nzuri yaani bonge la ofisi niko peke yangu halafu full kiyoyoziPOLE SANA KWA NDOTO ZAKO ZA KUTAMANI DUNIA KUWA KIJIJI.