USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 11,973
- 28,225
Haishangazi Mbowe kummiminia pongezi Rais Samia.
Freeman Mbowe kwenye mkutano wa hadhara wa CHADEMA, Furahisha, Mwanza, alisema kuwa ameamua kujilipua mabomu kwa kumpongeza Rais Samia.
Mbowe alisema, watu wanaweza wasimwelewe yeye kumpongeza Rais Samia, akasema jambo la maridhiano ya kisiasa na ruhusa ya mikutano aliyoitoa ni mambo ambayo hakuona hiyana kumpongeza.
Alisema, Rais Samia angeweza kuwa na kiburi kama mtangulizi wake, John Magufuli, kisha kuendeleza siasa za uadui na chuki. Rais Samia amechagua kuwa kiongozi muungwana. Mwenye upendo kwa Watanzania wote.
Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph “Sugu" Mbilinyi, alisema Rais Samia ni kiongozi jasiri, sio mwoga, ndio maana ameruhusu mikutano ya hadhara. Na ameruhusu kukosolewa.
Unashangaa?
Mbowe amesema anajivika mabomu kumsifu Rais Samia. Ukweli ni kuwa kummiminia pongezi Rais Samia sio kuvaa mabomu. Mbowe anaogopa bure.
Kila mwenye akili timamu anampongeza Rais Samia kwa kuiweka nchi salama kisiasa na kiuchumi.
Anzia viongozi wa kisiasa wenye akili. Mashehe, Maaskofu, wafanyabiashara hadi wanaharakati wenye akili timamu, wamekuwa na wanaendelea kumpongeza Rais Samia.
Mashehe wa Uamsho na watetezi wao wameshakiri uongozi bora wa Rais Samia. Baba Askofu, Benson Bagonza alishampa heko nyingi Rais Samia. Begonza anafahamika kwa ukosoaji. Kwa Samia kampongeza.
Taasisi ya Muunganiko wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), walishampa tuzo Rais Samia kwa matendo yake ya haki kwa Watanzania. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wameshampongeza Rais Samia.
Wanasiasa Zitto Kabwe, Juma Duni Haji na wengine wote wenye akili timamu wameshampongeza Rais Samia kwa jinsi anavyoongoza nchi vizuri, kwa uadilifu na matokeo chanya.
Kwa kifupi, kila mwenye akili anatambua na kuthamini kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia. Hivyo, Mbowe hajiviki mabomu kumpongeza Rais Samia mbele ya wenye akili. Labda majuha wachache, ndio wanaobeza utendaji bora wa Rais Samia.
Nchi inajengwa na wenye akili. Na wote wenye akili wanamwelewa Rais Samia.
Cecilia Mwalumbe,
Sauti kutoka Maji Matitu
Sent using Jamii Forums mobile app