Siri ya mafanikio ya bidhaa za Kichina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri ya mafanikio ya bidhaa za Kichina

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jan 9, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Siri ya mafanikio ya bidhaa za Kichina[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD][​IMG]
  Mambo ya Mchina[/TD]
  [TD]
  Kimekuwa na wimbi la bidhaa za Kichina karibu katika kila nchi duniani. Wachambuzi mbalimbali wamejaribu kuelezea siri za mafanikio ya Wachina kama ifuatavyo:[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]1- China ni nchi yenye watu wengi kabisa dunia na ni nchin inayotoa kiwango kidogo cha mishahara ukilinganisha na nchi za Magharibi. Sababu hii imeyafanya

  masoko ya dunia kuzipokea bidhaa za Kichina kwa vile zinakuwa ni za bei nafuu kwa sababu hazitumii gharama kubwa kuzizalisha, hasa gharama za malipo ya wafanyakazi.
  2- Kusoma na kutafiti masoko ya dunia. Wachina ni mahodari sana wa kufanya tafiti za kibiashara na kujua watu wa nchi gani wanahitaji nini na kwa ubora wa

  kiwango gani. Wakitumia matokeo ya utafiti wao, wanazalisha bidhaa kwa mujibu wa soko. Kila soko linapeklekewa bidhaa wanazozihitaji kwa kiwango wanachokihitaji.
  3- Kuchapa kazi kishujaa. Wachina ni watu wanaojitahidi kufanyabiashara katika mazingira magumu. Vijana kwa wazee wa Kichina wameenea mitaa ya nchi

  mbalimbali wakitangaza na kuuza bidhaa za Kichina, huku wengi wao wakiwa hawajui hata lugha za nchi husika. Mara nyingi wanatumia KIKOKOTOZI (calculator) ili kuwasiliana na wateja zao. Vilevile Wachina ni wajanja wa kujifunza

  lugha za nchi wanazokusudia kuzipelekea bidhaa zao. Mara nyingi bidhaa za kichina zina maelezo ya utumiaji wake kwa lugha ya sehemu husika.
  4- Kuheshimu tamaduni za nchi husika. Wachina si wakoloni wala wamishionari, hawana lengo la kutangaza dini yao wala kutawala nchi wanazozitembelea.

  Wikiwa Arabuni kwa mfano, wanajifunza kiarabu na utamaduni wa Kiislam. Wanavaa mavazi yanayokubalika Arabuni. Si watongozaji wa mabinti wa

  kiarabu au wavulana wa Kiarabu. Wao ni biashara kwa kwenda mbele.
  5- Kuridhika na faida ndogo. Kwani wao wanaamini kuwa “Ndondondo si chururu” Yaani kipato kinachoingia kidogo kidogo na kikadumu ni bora kuliko

  kipato cha kikubwa cha mpito. Hizi ni sababu kuu ambazo mwandishi ameweza kuzikusanya. Hata hivyo zipo sababu nyingine nyingi ambazo mwandishi hakuzitaja. Watanzania tusome kwa wenzetu[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Mchina afanya Vitu vyake duniani doleee
   
 2. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  ni hao!
   
Loading...