olym
JF-Expert Member
- Jul 25, 2019
- 265
- 449
Hello JF Member,
Ni matumaini nyote mko poa kabisa, napenda niwashirikishe jambo moja ambalo najua kwa namna moja ama nyingine kuna watakaopata kitu na kupitia wachangiaji wengine kuna elimu kubwa itapatikana miongoni mwetu.
Kwa uzoefu wangu mdogo kwenye tasnia ya fedha na kuzikuza nimeona nitoe mawazo ya nini ni siri ya mafanikio kwa jamii yetu.
Uvumilivu, wengi wetu hatuna uvumilivu wa kusubiri huku tukiendelea kuweka jitihada zaidi kwa tunachokifanya na kukiamini na kupelekea kupoteza mwelekeo wa mambo mengi tuyafanyao.
Akiba, pia hili ni changamoto kwa wengi na ni moja ya kitu kizuri sana kwenye kufanikiwa, mfano mkiwa wawili mmoja ana akiba ya 1M mwingine hana ikija hata dili la wewe kununua pikipiki mpya inauzwa mtu ana uhitaji mwenye akiba atanunua na kuuza 1.2M au hata 1.5M kwa muda mfupi anakuwa amezalisha ila kama hakuna akiba kuna shida kidogo.
Starehe na matumizi yasiyo lazima, hiki pia ni changamoto ambayo ilitukumbuka vijana wengi baada ya kumaliza vyuo vikuu na kupata ajira zetu za kwanza, starehe inachangia sana kudidimiza maendeleo yetu ikiwa haujui utumie nini na uhifadhi nini, mfano last month nimetoka kuipiga kibiriti pesa nyingi kidogo nakuja kushtuka account haina kitu.
Kutokuwa na taarifa sahihi, hii naiweka hivi haswa kwenye masuala ya biashara ni kuanza au kusikia biashara fulani inalipa bila kujifunza na kuelewa nje na undani wake unaingia na unachoma pesa yako na unarudi hatua nyingine nyuma, naomba niseme hakuna biashara ambayo hailipi ila mikakati yako ndio itakuangusha, kila biashara ina mabilionea kwenye hii dunia.
Mwisho, nafikiri tutaelewa na kujitahidi mwaka huu 2020 uwe wenye baraka na neema kwa kila tunaloliendea.
Olym
Sent using Jamii Forums mobile app