Siri ya kuachwa Katibu Mkuu Kinana na Sekretarieti nzima

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Hakuna jambo jingine lolote zaidi ya Mwenyekiti Magufuli kutokuwa tayari kuongoza CCM. Mwenyekiti wetu mpya hakuwa tayari kukabidhiwa Uenyekiti sasa. Hata yeye na Mwenyekiti mstaafu wamesema.Ndiyo maana amewaachia uongozi 'kijanja' walewale.

Kiongozi mpya huingia na viongozi wapya. Tazameni na mshuhudie kilichotokea na kinachoendelea Serikalini. Imeshindikana vipi chamani? Utayari wa uongozi wa chama haukuwepo. Ndiyo maana waonambali tuling'amua. Tukashauri ima Kikwete aendelee au uchaguzi 'wa kweli' ufanyike.

Kumwacha Kinana na Sekretarieti nzima ni uthibitisho wa hoja zetu. Mazoea na kulazimisha yamejidhihiri kwa umahiri. Eti amepata kura zote za NDIYO! Mwenyekiti mpya akiwa tayari na wakati wake kufika,ataanza kuongoza. Kwasasa,'hajachukua' madaraka yake. Amewaachia 'wenyewe'!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa ZOTE-NDIYO Dodoma)
 
Acha ramli chonganishi wewe
Uchaguzi wa chama unaanza july mwakani,busara tu imemuongoza aanze na kinana walau kwa muda mfupi ili aweze kupata uwanja wa kukijua chama
Magufuli ameshapewa chama,mnahangaika kuzua tu,ulitaka kinana asirejeshwe?
 
Tupatupa huoni ama huelewi nini? Unajua fika Sefue aliachiwa muda kkama wa Kinana. Tulia wa kuisoma wako wengi.

Hakuna jambo jingine lolote zaidi ya Mwenyekiti Magufuli kutokuwa tayari kuongoza CCM. Mwenyekiti wetu mpya hakuwa tayari kukabidhiwa Uenyekiti sasa. Hata yeye na Mwenyekiti mstaafu wamesema.Ndiyo maana amewaachia uongozi 'kijanja' walewale.

Kiongozi mpya huingia na viongozi wapya. Tazameni na mshuhudie kilichotokea na kinachoendelea Serikalini. Imeshindikana vipi chamani? Utayari wa uongozi wa chama haukuwepo. Ndiyo maana waonambali tuling'amua. Tukashauri ima Kikwete aendelee au uchaguzi 'wa kweli' ufanyike.

Kumwacha Kinana na Sekretarieti nzima ni uthibitisho wa hoja zetu. Mazoea na kulazimisha yamejidhihiri kwa umahiri. Eti amepata kura zote za NDIYO! Mwenyekiti mpya akiwa tayari na wakati wake kufika,ataanza kuongoza. Kwasasa,'hajachukua' madaraka yake. Amewaachia 'wenyewe'!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa ZOTE-NDIYO Dodoma)
 
Acha ramli chonganishi wewe
Uchaguzi wa chama unaanza july mwakani,busara tu imemuongoza aane na kinana walau kwa muda mfupi ili aweze kupata uwanja wa kukijua chama
Jana amesema kuwa yeye si mgeni ndani ya chama, na kuwa amekuwa chamani kwa miaka zaidi ya 40, sasa unadhani anataka kukijua chama kwa namna gani zaidi?
 
Kwa mtazamo wangu nadhani hakukuwa Na umuhimu wa kupiga Kura ili hali majibu yanajulikana,kilichotakiwa ni chama kumpitisha kwa kauli mmoja kuwa mwenyekiti mpya wa CCM.
 
Yaelekea ndugu PM kwa sasa umechanganyikiwa sana. Hujui pa kushikia. Kina unachogusa kinateleza. Unalia na kusaga meno. Moyo unatweta mithili ya mtu aliyefumaniwa. Naam. Huyo ndiye JPM. Nikuhakikishie kuwa alichofanya JPM si kipya na wala hakijaenda tofauti na misimamo yake. Hakuna cha kuwaachia akina Kinana waongoze chama kijanja.

Katika kila eneo, ni lazima ufahamu misingi yake. Alipochaguliwa kuwa Rais na kuapishwa, haraka sana alimteua Ombeni Sefue kuwa Katibu Mkuu kiongozi. Alijua kuwa hawezi kufanya lolote bila kuwa na msaidizi wake. Pia wakati huo huo akamteua Masaju kuwa Mwanasheria wake. Alijua kuwa bila Mwanasheria hawezi kufanya kazi. Ombeni Sefue na Masaju ni wayeule wa Kikwete ambao JPM aliwakuta wakati anaapishwa na ndio waliosimamia kuapishwa kwake.

Baada ya muda kidogo, Rais akafanya mabadiliko ya nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi. Ombeni Sefue Out. Masaju anaendelea. Hivyo si kweli kwamba kila unachokikuta lazima kiondoke. Huu ni mtazamo hasi na wanaowaza aina hii ni wale wale ambao walikuwa wanawaza kuwa ipo siku CCM itakuja kuanguka.

Tukija kwenye hoja yako ya Msingi, jana ilikuwa ni Mkutano Mkuu Maalum na ajenda kuu ilikuwa moja tu. ya kumchagua Mwenyekiti wa CCM baada ya Kikwete kuachia ngazi. Naam Magufuli kachaguliwa. Katika protokali za kawaida, mkubwa akimaliza kuongea, mtoto huna fursa yena ya kuongea. Ndio maana wanapishwa kwanza watoto na ndipo mkubwa huongea mwisho. Siamini kama na hili Mzee Tupatupa hulijui.

Hata kwenye mikutano. Unaanza Mkutano wa Kamati Kuu then Halmashauri Kuu then Mkutano Mkuu. Ukishafika Mkutano Mkuu, huwezi tena kwenda kinyume ukaitisha tena Halmashauri Kuu. Utakuwa Mwendawazimu. Siamini kwa ukada wako Mzee Tupatupa hulijui hili.

Hivyo baada ya Mkutano Mkuu kumalizika, JPM kachaguliwa, hakupaswa tena kiprotokali kuitisha kikao cha NEC kuwathibitisha wajumbe wapya wa Sekretarieti. Anateua wale wale ili apate muda wa kutafakari na kuwa na safu ambayo anaamini itamsaidia. Ndio maana kamteua Kinana kuwa Katibu Mkuu na kuirejesha Sekretarieti nzima. Hapa JPM kacheza kama Pele.

Pia Mzee Tupatupa ukumbuke kuwa jana ilikuwa ni siku ya furaha kwa CCM. Iliandaliwa tafrija ili makada tukasherehekee na kufurahia. Nikuulize Mzee Tupatupa, uliwahi kuhudhuria sherehe ya harusi ambapo umeshiriki Kitchen Party na Sendoff Then mke anamkataa mume siku ya hasuri? Nini kinatokea?

Unafikiri nini kingewatokea wale waliompa kura za Ndiyo Magufuli then wakatumbuliwa pale pale? Wangejisikiaje? Je unafikiri Dodoma pangekalika? Nini wangewaza kwenye vifua vyao?

Kiongozi mzuri ni yule anayechagua wakati wa kupiga na mahala pa kupiga. Binafsi naamini kuwa Nape Nnauye, Dr Asha Rose Migiro, Rajab Luhwavi na Zakhia Meghji hawatakuwa kwenye Sekretarieti ya JPM ambayo ataiteua siku chache zijazo. Naam huo ni mtazamo wangu nawe Mzee Tupatupa unaweza kuja na vigezo vyako kunipinga.

Nape ni Waziri katika serikali ya JPM. Rais ameshaweka wazi kuwa hataona mtu anayemteua serikalini anakuwa na wadhifa mwingine chamani. Dr Asha Rose naye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Marekani. Naye anaangukia kule kule. Rajab Luhwavi alikuwa anashiriki kwenye mikakati ovu ya kujisimika kileleni. Naye hana nafasi. Kumbuka jana alisema kuwa kuna watu walikuwa wanawinda nafasi ya Katibu Mkuu na akasema kuwa imekula kwao? Wewe ulimuelewaje? Zakhia Meghji hana nafasi kabisaa kwa vile hakuna lolote alilofanya tangu ateuliwe kwenye nafasi hiyo.

Siamini kama kuna wazee wapo ndani ya CCM wanashindwa kuchanganua mambo na kutokuwa na hoja za kujenga wawapo kwenye hadhira kama Mzee Tupatupa. Tunao wazee kama akina Yusuph Makamba ambao kila wakisimama kuongea, jukwaa linasisimka. Wazee wa design ya Mzee Tupatupa tunao kule UKAWA
 
Jana amesema kuwa yeye si mgeni ndani ya chama, na kuwa amekuwa chamani kwa miaka zaidi ya 40, sasa unadhani anataka kukijua chama kwa namna gani zaidi?
Yupo sahihi kabisa si mgeni ccm,lakini kwa wadhifa tuliomtwika ,walau awe na kinana kwa miezi michache ijayo
Kwani na kule ikulu si alianza na Ombeni Sefue?ni nyie hao hao mlipiga kelele aondoe mabaki ya Jakaya
 
Mwenyekiti safari hii lazima alainike, awe mpole.
CCM ni kubwa sana kwake, hawezi kupambana na wenye chama, na ni rahisi kumuhujumu na kumuangusha yeye na chama chake.
Its not over yet.
Una maana CCM nimkubwa kuliko Serikali? Nakubaliana na wewe katika point moja tu kuwa kwa vile Magufuli kateuliwa na Chama, ni dhahiri kwamba chama kitakuwa kikubwa. Ila kwa vile yeye ndiye Mwenyekiti wa chama, sidhani kama kuna mkubwa chamani zaidi yake
 
Kawatupia kamba ndefu wajimalize wenyewe mmoja baada ya mwingine. Kawapa hadidu rejea ya anachotaka kukifanya kwenye chama ili kukiimarisha; kiondokane na ulegelege wa enzi za JK, ili kiweze kuisimamia serikali madhubuti. Kazi kwao kuonyesha wanaweza vinginevyo imekula kwao mithili ya Sefue, Kitwanga na Anne Kilango!! Only time will tell.
 
Back
Top Bottom