Kwa sasa, sultani na vibaraka wake wanatumia njia mbadala kutekeleza kile ambacho walishindwa kufanya baada ya mapinduzi kwa sababu ya muungano. Masikini wa Mungu wengi wa wanaohangaika na kupigia chapu muungano wa mkataba au kujitenga kwa Zanzibar hawaelewi wanatumiwa na vibaraka wa mkoloni ili kuirudisha Zanzibar kwa Sultani. Kuna watu wanapewa mapesa kibao toka uarabuni ili kuvuruga muungano kwa kisingizio kuwa U-Zanzibari wao uko hatarini kufutika. Wadai taifa lao.
Hivyo, hakuna hata mmoja kwenye CCM ana ubavu wa kuzungumzia serikali moja kwa kuwa:
- Zanzibar wameshakuwa NCHI (According to their constitution)
- Ni UZENBE wa CCM na Serikali yao umefikisha hali kuwa hivyo
- Kuukubali ukweli maana yake ni kumuambia Kikwete na wenzake ni wadhaifu
- Kubwa zaidi ni kuwa kwa upepo ulivyo hivi sasa, kuwaambia WaZenji serikali moja ni sawa na kuuvunja Muungano. Hawatakubali.
Kaka Mween,
Kama nimekuelewa vizuri, Concern yako imeegemea katika mambo mawili:
1. Kuihofia hatima ya Zanzibar - na kama ndivyo hatima hiyo ya Zanzibar kama itakuwa na madhara basi athari zake zitaikumba Bara. Ndicho kinachoifanya CCM na wengine wenye mtazamo wa kuunga mkono muungano kuendelea na msimamo huo?
2. Lakini je, udhaifu wa CCM na uongozi wake (akiwemo Kikwete) na aibu ya kukubali kwamba waliruhusu mambo kufikia hapo pa Zanzibarb kujiwekea Katiba yake huru ndio lichukuliwe kama kigezo cha kung'ang'ania mambo ambayo madhatra yake yanaweza kuwa makubwa na hatari zaidi?