Chigwiyemisi
JF-Expert Member
- Jun 22, 2011
- 531
- 230
Wanajamvi heshima kwenu.
Nimetumia muda mefu sana kufanya utafiti ni kwa nini CCM wanang'ang'ania serikali mbili lakini mpaka hivi leo sijapata sababu yoyote ya msingi.
Nimekuwa nikiamini kuwa serikali tatu ni suluhisho la kero za muungano hata kabla ya mchakato wa Katiba kuanza.Tume ya Warioba ikaleta sababu za msingi kabisa za kuwa na serikali tatu na ikapendekeza hivyo katika rasimu. Wanaounga mkono serikali tatu wote wana hoja. Lakini wanaong'ang'ania serikali mbili (CCM) hawana hoja yoyote zaidi ya propaganda.
Sasa wadau naomba kujua kuna siri gani ya wao kung'ang'ania serikali mbili kinyume na maoni ya wananchi? Naomba mwenye kujua chochote anisaidie kwani hakuna hata mmoja anayejenga hoja zenye mashiko kuhusu serikali mbili. Hata rais mwenyewe aliishia kutishia tu lakini hakuna hoja yenye mashiko niliyoiona toka kwake. Naamini kuna siri imejificha au maslahi fulani. Je ni siri gani au maslahi gani?

- Wamefikia hatua ya kuwanunua hata watu tunaowaheshimu sana kwenye jamii kuunga mkono hoja yao.
- Wamegeuza TBC kuwa chombo cha propaganda na kuwasema wote wanaopendekeza serikali tatu kuwa wanataka kuvunja muungano (propaganda ya kijinga kabisa).
- Wamewatisha wabunge wao kwa kuwalazimisha kupiga kura ya wazi ili kuona wanaoenda kinyume na msimamo wao.
- Wamemdhihaki na kumnyanyasa Jaji Warioba na tume yake.