Siri nzito ya 'muccob's" hii hapa.

Siri nzito ya 'muccob's" hii hapa.

Nelson Kileo

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Posts
3,054
Reaction score
3,263
HABARI WANA JAMVI.


TUMEKUA TUKISIKIA WADAU MBALIMBALI WAKISEMA KUA AJIRA NYINGI HUPEWA WATU WANAOTOKA KWENYE CHUO CHA USHIRIKA KILICHOPO MOSHI 'MOSHI UNIVERSITY COLLEGE OF COOPERATIVE AND BUSINESS STUDIES' YAANI MUCCOB'S,AMBACHO NI CHUO KISHIRIKI CHA 'SUA' YAANI 'SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE'[AMBACHO CHUO HICHO 'MUCCOBS' HIVI SASA KIPO KWENYE MCHAKATO WA KUA CHUO KIKUU KAMILI YAANI KISIWE TENA CONSTITUENT COLLEGE OF SUA] .WATU WANADAI KUA AJIRA NYINGI HUPENDELEWA WADAU WALIOMALIZA KUTOKA CHUO HICHO NA ZAIDI KWENYE TAASISI ZA BIASHARA PIA ZA MAENDELEO YA KIJAMII KAMA NGO'S,WENGI WANASEMA HII INATOKANA NA HISTORIA YA WAFANYAKAZI WENGI KWENYE TAASISI MBALIMBALI KUA NA UMAKINI NA WELEDI WAKIWA KAZINI . (GOOD REPUTATION).MIMI BINAFSI NIMEKUTANA NA WATU WENGI SANA WAKIDAI KUA CHUO HICHO KINATOA WAHITIMU WAZURI NA WALIOIVA.KUNA HABARI PIA ISEMAYO, KAZI ZILIZOTANGAZWA NA TRA WENGI WATATOKA USHIRIKA.( HUMU JF PIA IMEWEKWA).


NIMECHUNGUZA NI KWANINI CHUO HICHI KINAJIZOLEA SIFA HIZO, NA NIMEGUNDUA KUA 'GOOD REPUTATION' INATOKANA NA SABABU ZIFUATAZO;

1. WELEDI WA WALIMU {LECTURERS}
KATIKA TAFITI ZANGU, NIMEGUDUA KUA WALIMU WANAOFUNDISHA KWENYE CHUO HICHO WENGI WAO WAKIWA NI MAPROFESA NA MADAKTARI, WANA SIFA ZIFUATAZO, I).WAMEBOBEA KWNEYE KAZI HIYO YA UFUNDISHAJI (EXPERIENCE) II).NI WENYE WELEDI (DESCPLINE).NA III).WAMEJITOA KWENYE KAZI HIYO.NIMEGUNDUA HILO KUTOKANA IV).VITU WANAVYOVIFUNDISHA VINGI NI VITU AMBAVYO WENGI WAO WANAKUTANA NAVYO NA KUVIFANYAKAZI KATIAKA MAISHA YAO YA KILA SIKU IKIWA WENGI WAO HUTUMIKA KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIUCHUMI NA SERIKALI, PIA KATIKA KUTENGENEZA SERA NA SHERIA MBALIMBALI JUU YA MASWALA YA USHIRIKA,VIWANDA NA BIASHARA,NA HIVYO KUA NA HIVYO KUWAWIA RAHISI NA HALISI ZAIDI KWA KILE WANACHOKIFUNDISHANA.NA PIA TAFITI WANAZOZIFANYA {RESEARCH] ZIMEKUA ZIKISAIDIA KATIKA KUTATUA MASWALA MBALIMBALI KATIKA UCHUMI.ZAIDI NIMESHUHUDIA JINSI WALIMU WANAVYOHUDHURIA VIPINDI BILA KUKOSA TENA KWA MUDA MUAFAKA ,NAMNA YA UFUNDISHAJI,NA PIA UHUSIANO MZURI ULIOPO KATI YA WALIMU NA WANAFUNZI.

2. PROGRAM ZINAZOTOLEWA.{(UBUNIFU}
INGAWA KUNA PROGRAM ZILIZO ZOELEKA KUTOLEWA KWENYE VYUO VINGINE KAMA, PROCUREMENT,ACCOUNT AND FINANCE PAMOJA NA HUMAN RESOURCE MANAGEMENT , ILA PALE ZINATOLEWA KWA NAMNA YA KITOFAUTI KABISA. HUTOFAUTIANA NA VYUO VINGINE KUTOKANA NA IDADI YA COURSE ZILIZOPO KWENYE PROGRAM HUSIKA, PAMOJA NA MATERIAL YANAYOTUMIKA HUA YAPO KWENYE MUDA SAHIHI,

UBUNIFU
;
UBUNIFU MKUBWA UMEJIONYESHA KWENYE KUTENGENEZA PROGRAM ZA MASOMO ZINAZOENDANA NA MABADILIKO YA KIUCHUMI DUNIANI,UBUNIFU HUO UMEONEKANA KWENYE PROGRAM ZIFUATAZO;

a)'MICRO-FINANCE AND ENTERPRISE DEVELOPMENT'{DEGREE LEVEL}
PROGRAMU HII INAHUSIKA NA MAMBO YA TAASISI NDOGONDOGO ZA KIFEDHA PAMOJA NA UJASIRIAMALI.KAMA ILIVYO SASA , JAMII INAJIKWAMUA KWNYE UMASIKINI KUPITIA TAASISI HIZI NDOGONDGO ZA KIFEDHA(SACCOS) KWA KUJIPATIA MIKOPO YENYE UNAFUU, DUNIA PIA IMEJIKITA KWNYE UJASIRIAMALI NA KUONA NDIO NAMNA PEKEE YA KUDIDMIZA UMASIKINI.PROGRAM HIYO HAIKUISHIA TU HAPO BALI INA WIGO MPANA KATI YA COURSE TAKRIBANI 52 ILIYOJIBEBEA NDANI YAKE KUNA COURSE ZA MAMBO YA BANK,FINANCE,BUSSINES LAW NA NYINGINE NYINGI , COURSE AMABAZO ZINAMPA FURSA MHITIMU KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALI MBALI KATIKA JAMII INAYOMZUNGUKA.PROGRAM HII HUMFANYA MHITIMU KUA WA KISASA NA KUENDANA NA MABADILIKO YA DUNIA KATIKA SWALA ZIMA LA KUJIKWAMUA KIUCHUMI NA KUONDOKANA NA UMASIKINI.

PROGRAM TAJWA HAPO JUU KWA SASA NI KAMA 'LULU' NA NI GUMZO MIDOMONI MWA WATU NA TAASISI MBALIMBALI.

b) 'COMMUNITY ECONOMIC DEVELOPMENT"{DEGREE LEVEL}


SEHEMU MBALIMBALI PROGRAM HII IMEKUA INAJULIKANA KAMA 'COMMUNITY DEVELOPMENT' LAKINI KWA UMAKINI NA UFANISI WA HALI YA JUU,WANAZUONI WA MUCCOBS WALIGUNDUA KUA MABADILIKO NA MAENDELEO YA JAMII YANAENDA SAMBAMBA NA MABADILIKO YA KIUCHUMI, HIVYO BASI WAKAONA KUNA HAJA NA UMUHIMU WA KUWEPO KWA PROGRAM HII ILIKUONYESHA NI KWA JINSI GANI UKUWAJI WA UCHUMI UNALETA MABADILIKO CHANYA KATIKA UKUAJI NA MAENDELEO YA KIJAMII . PROGRAM HII INATOA MAFUNZO JUU YA MAHUSIANO YALIPO KATI YA JAMII PAMOJA NA UCHUMI.

PROGRAM TAJWA HAPO JUU ZOTE CHIMBUKO LAKE NI CHUONI HAPO.



3.TIME TABLE.
RATIBA NYINGI ZA MASOMO NILIZO ZIONA CHUONI PALE ,ZIPO TOFAUTI KABISA NA RATIBA NILIZIZIONA KWNYE VYUO VINGINE. IKIWA NI PAMOJA IDADI YA MASOMO YANAYOFUNDISHWA KWA SIKU PAMOJA NA MUDA WA KILA SOMO KUFUNDISHWA. MASOMO MENGI CHUONI HAPO HUFUNDISHWA KWA MUDA USIOPUNGUA MASAA MAWILI NA RATIBA ZOTE HUANZA KUANZA 8:00am NA KUMALIZIKA 7;30pm. PIA WAMEZINGATIA UWEPO WA KUTOSHA WA SEMINER HOURS. HII INAMPA MWANAFUNZI FURSA YA KUJUA MAMBO MENGI.PIA WALIMU WAMEKUA MAKINI KATIKA KUZINGATIA MUDA,MUDA KIPINDI KINAPASWA KUANZA HUNAANZA NA MDA KINAPASWA KUISHA HUISHA KWA MUDA MUAFAKA. KWA HILI HATA WW UTAWEZA KULISHUHUDIA, CHA KUFANYA FIKA ENEO HILO NA UONE MDA WANAINGIA NA MUDA WANATOKA CHUO NA JINSI WALIMU NA WANAFUNZI WANAVYOPISHANA KUKIMBIA KWNYE VIPINDI.

4.UTUNGWAJI NA USIMAMIZI WA MITIHANI PAMOJA NA WASTANI WA UFAULU..

WASTANI WA UFAULU NI KUANZIA WASTANI WA ..... NA KUENDELEA. MGAWANYIKO UKIWA KAMA IFUATAVYO

ASSIAMENT + QUIZ+PRESENTATION+CLASS TEST {COURSE WORK} 40%
FINAL EXAM 60%



TOTAL 100%


KWA MGAWANYIKO HUO HAUMPI NAFASI MWANAFUNZI KUBEBWA NA COURSE WORK' NA KWA MAANA HIYO ATABAKI KUA NA KIBARUA KIKUBWA CHA KUFANYA VIZURI KWENYE ALAMA 60% ZA MTIHANI WA MWISHO NA LAZIMA ITAMGHARIMU KUSOMA KWA BIDII KUFIKISHA KIWANGO CHA UFAULU.
UTUNGWAJI WA MITIHANI NI WA KIWANGO CHA JUU ,USIMAMIZI WAKATI WA MITIHANI NDIO HATARI KABISAA/USIMAMIZI NI WA KIWANGO CHA JUU.


5. ADABU WALIYONAYO WANAFUNZI.

UKITOFAUTISHA NA VYUO VINGINE TENA UKIZINGATIA IDADI KUBWA YA WANAFUNZI WENGI WA VYUO NI VIJINA, VYUO VINGI WANAFUNZI WAMEKUA WAKIKOSA HESHIMA KWA KUJIINGIZA KWENYE STAREHE MBALIMBALI NA KUWAFANYA WASAHAU KILICHOWAPELEKA,ILA KWENYE CHUO HICHI , WENGI WAO WANAJIHESHIMU NA KUJUA NI NN HASA KILICHOWAPELEKA.WAHUDHURIAJI WAZURI KWENYE VIPINDI NA PIA WANAKUA NA JITIHADA KATI KUSOMA,WAKIZINGATIA ZAIDI KUSOMA KWENYE MAKUNDI.WENGI HUJIONA KAMA WAMETUA MZIGO MZITO PALE IFIKAPO MWISHO WA SEMISTER.
NILIJARIBU KUJIULIZA NI KWANINI WANAFUNZI HAWA WAPO HIVI,NA NILJIULIZA YAFUATAYO,

1.SABABU ZA KIMKOA, MJI WA MOSHI NI MJI TULIVU , MJI WA KIBIASHARA, NA WATU WENGI WAPO BIZY KUTAFUTA HELA KULIKO KUFANYA STAREHE. NI MJI AMBAO HAUNA STAREHE KAMA MJI WA DAR-ES-SALAAM.

2. LABDA ,NI JINSI RATIBA INAVYOWABANA NA KUWAFANYA WASHINDWE KUJIINGIZA KATIKA MASWALA YASIYO NAA MAADILI.

NA MENGINE MENGI AMBAYO NILIJIULIZA ,ILA NILIISHIA KUJUA TUU ..PALE NDIPO ADABU INAFUATA MKONDO WAKE NA TENA ZAIDI UKIWA UNAFANANISHA NA VYUO VINGINE .


HIZO NI KATI TU YA SABABU CHACHE NILIZOWEZA KUZIONA BAADADA YA KUFANYA TAFITI NDOGO KWENYE CHUO CHA 'MUCCOBS' ,NAJUA ZITAKUWEPO SABABU NYINGINE KAMA VILE , MAZINGIRA MAZURI, MANEJIMENTI NZURI NA NYINGINE NYINGI TU ZINAZOKIFANYA CHUO CHA USHIRKA MOSHI KUA ASALI KICHWANI,MIDOMONI NA KWENYE TASISI MBALIMBALI.
HIVYO BASI MSIBAKI KUUMIZA VICHWA NA KUSEMA 'WHY MUCCoB'S' HIZO NDIZO SABABU , VYUO VINGINE YAPASA KUIGA .

BIG UP {MUCCoB'S}
 
Acha kupiga promo wanaoenda hapo ni wale waliofel yani div 3 na kuendelea.Uliye anzisha huu uzi unataka marumbano ya vyuo wakati hayana tija kwa Tz wakati wasomi wengi na rasilimali zinaibiwa na Wazungu Je kuna haja ya kuwa na wasomi?
 
Huyu nataka kubishana tuu lakini hicho chuo cha kawaida sana
 
MUCCoB'S gooooooooooooooo goooo!
Kingine mitihani yote husimamiwa na Board ya NBAA inakuwa yenye kiwango ambacho ukichomoa basi unakuwa umewiva vya kutosha! na Pass mark pale ni 50 hamna utani!

Sina maana ya kuvibeza vyuo vingine ila palipo na ukweli pasemwe tu na kama mnabisha ingieni kwenye hizo taasisi muone Muccobs walivyo wengi na Wako vizuri!
 
MUCCoB'S gooooooooooooooo goooo!
Kingine mitihani yote husimamiwa na Board ya NBAA inakuwa yenye kiwango ambacho ukichomoa basi unakuwa umewiva vya kutosha! na Pass mark pale ni 50 hamna utani!

Sina maana ya kuvibeza vyuo vingine ila palipo na ukweli pasemwe tu na kama mnabisha ingieni kwenye hizo taasisi muone Muccobs walivyo wengi na Wako vizuri!

Acha promo mkuu kwanz mm cji ng'o kusoma hapo napiga CBE hapa
 
hahhahhaahaha wewe unaota mchana wewe hicho chuo kinajilikana hapo tu na kilometa chache kutoka hapo hahhhahhah wanafunzi wanaotoka hapo tunakutana nao huku job cv mbovuuuu
 
acha kupiga promo wanaoenda hapo ni wale waliofel yani div 3 na kuendelea.uliye anzisha huu uzi unataka marumbano ya vyuo wakati hayana tija kwa tz wakati wasomi wengi na rasilimali zinaibiwa na wazungu je kuna haja ya kuwa na wasomi?
comment kilichopo ,na sio uongelee vitu nje ya maada .. Mara ucomment hoja hii mara utoke nje ya mada ..
Nenda kacomment hizo za rasilimali ziko nyingi jf . Na sio lazima ucomment kila ukionacho.
Hakuna anayetaka mabishano ya vyuo kama usemavyo bali ni ukweli ulio wazi..
Weka tafiti yako juu ya tuhuma hizo kuwa waendao ni failures.. Otherwise ukiongeacho tunakiita propaganda
 
hahhahhaahaha wewe unaota mchana wewe hicho chuo kinajilikana hapo tu na kilometa chache kutoka hapo hahhhahhah wanafunzi wanaotoka hapo tunakutana nao huku job cv mbovuuuu

utakataa lakini ulweli utabaki pale pale ..
 
na ndio kinaongoza kwa ngono na tabia mbovu za kujiuza kwa wengi wa wanawake pale MALINDI,PUB ALBETO NA LALIGA,,hilo nalo usisahau mkuu
 
na ndio kinaongoza kwa ngono na tabia mbovu za kujiuza kwa wengi wa wanawake pale malindi,pub albeto na laliga,,hilo nalo usisahau mkuu

mnunuzi na muuzaji hukutana pamoja .. Na kama ulishanunua ngono moshi aliyekuuzia akakuambia ni mwanafunzi wa pale kakudanganya ili umuone wa thamani other wise hakuna ukweli .
 
Nakubaliana nawe mkuu,muccobs aka muccobize elimu yake ngumu kama harvard watu wanasoma utafikiri wanafunzi wa sekondar,pia nidham lazima iwepo tu kwa njia yoyote! Hapana chezea C.C.P kabisa wakizingua tu jamaa wanashuka kufanyia field pale
 
Nijuavyo mie muccobs ni chuo cha mchangani.alafu wewe lazima utakua ni ombeni ibrahim likolwa.

hayo majina ya watu unataja huku ya kazi gani .. changia hoja kaa pembeni .. umeshasema ni cha mchangani basi acha wamchangani wachezi.
 
Marketing officer.
Promo nyingi.
Piga msuli ilukimaliza ingia kitaa, komaa na maarifa uliyopata achana na Mbwembwe za Chuo ulichotokea
 
Marketing officer.
Promo nyingi.
Piga msuli ilukimaliza ingia kitaa, komaa na maarifa uliyopata achana na Mbwembwe za Chuo ulichotokea

nilitoa hoja ya utafiti niliopata .. na sijaona kama nimemgusa mtu direct .. sasa inageuka vip kua kero kwa mtu binafsi direcf
 
MUCCoB'S gooooooooooooooo goooo!
Kingine mitihani yote husimamiwa na Board ya NBAA inakuwa yenye kiwango ambacho ukichomoa basi unakuwa umewiva vya kutosha! na Pass mark pale ni 50 hamna utani!

Sina maana ya kuvibeza vyuo vingine ila palipo na ukweli pasemwe tu na kama mnabisha ingieni kwenye hizo taasisi muone Muccobs walivyo wengi na Wako vizuri!

Hata Mzumbe ni 50 acha sifa za kijinga wewe chuo chenyewe wanaosoma 70% hawana boom sababu ya div III na IV 20% div II na 10% div I.
 
Nakumbuka niliomaliza nao form 6 walioenda muccobs wenye div II hawafiki 10 hakuna mwenye div I aliyeenda pale na wenye div III na IV ni zaidi ya 80 both Degree na IV Diploma. Najua mtani mind ila muccobs si tu kwanilio maliza nao mwaka huo hata miaka mingine na ninao wajua wote Waliosoma Muccobs ni waliopata III na hata shule hawakuwa vizuri darasani. Hutaki acha sitaki matusi hapa ila thats the truth tho unauma.
 
Back
Top Bottom