BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,082
Tume haitatoa taarifa za fedha za EPA kwa sasa
2008-03-09 16:46:28
Na Radio One Habari
Timu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza upotevu wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje-EPA-ya Benki Kuu ya Tanzania imesema kwa sasa haitatoa taarifa ambazo zinaweza kuathiri kazi ya uchunguzi inayoendelea.
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bwana Johson Mwanyika imesema tume itaendelea kutoa taarifa ambazo inaamini hazitaathiri uchunguzi unaoendelea.
Timu hiyo ambayo wajumbe wengine ni Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha, TAKUKURU, imesema pamoja na fedha zinazorudishwa ni vyema ikaeleweka kuwa kazi ya uchunguzi haijafika mwisho.
Taarifa hiyo ambayo imepewa kipindi cha miezi sita kukamilisha kazi yake huu ni mwezi wa pili tangu ianze kazi yake na kwa sasa imejikita katika kufanya uchunguzi wa kitaalamu na wa kina.
Kumekuja na hoja kutaka watuhumiwa wanaorejesha fedha watajwe majina yao.
SOURCE: Radio One