Sipo comfortable na salamu za kiswahili

Sipo comfortable na salamu za kiswahili

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
23,713
Reaction score
57,229
sio kesi lakini ni mtizamo wangu tu kuwa salamu zetu huwa zipo kinafki sana.unakuta yes mnafahamiana kabisa na kila mtu anajua jinsi maisha yanavotukimbiza resi,ubize ila kwenye salamu tu mmekutana naye labda mtaani au njian mtu atataka musalimiane dakika kumi,maneno mengi afu ni yale yale
Mfano wa story tumekutana
Mtu:habari ndege
Mimi:safi sana
Mtu:upo?
Mimi:yeah nipo
Mtu:huonekani
Sasa huwa najiuliza huwa tumekaririshwa hadi salamu mtu anakuambia huonekani as if kwamba imeandikwa mtakuwa pamoja saa zote.na wakati anajua kabisa maisha tupo mazingira tofauti
Mfano wa story nyingine
Mtu:shwari
Mimi:ni shwari
Mtu:kama kawaida?
Sasa najiuliza hio kawaida si ndo maana tunaendelea kuishi
Mtu:nambie
Sasa nikwambie kitu gani wakati tunayoyaona ndo haya haya
NINGEWEZA KUTOA MIFANO MINGINE YA SALAMU AMBAZO ZINABOA ILA POINT YANGU YA MUHIMU JAPO SIO YA MSINGI NI KUWA SALAMU ZA KISWAHILI NI KAMA VILE TUNAKARIRISHWA MANENO YA KUSEMA.MPANGILIO WA MAZUNGUMZO HASA TUKIANZA NA SALAMU TUPO SLOW SANA..ME MTU AKIANZA KUZINGUA KWENYE SALAMU TU NASHINDWA KUVUMILIA KUJIAMIN KUONGEA NAYE NAMUONA KAMA AMEKAA KINAFKI NAFKI.namkubali mtu ambaye tukisaliamana tuna flow naturally SASA UNAKUTA MTU HANA CHS KUKWAMBIA LAKINI ILI MUONGEE ATATAKA MSALIMIANE MUDA MREFU
NB:maisha ni zaid ya salamu,hivyo hali kama hizo haziNikwazi sana lakini ndo hivyo huwez kumkataza mtu kufikiri.ndo nimefikiri hivyo kwamba kama huna habari mpya kumwambia mtu msalimie kifupi tu
Mambo vip
Poa
Basi afu pita hivi..sio uanze kumchora mtu akujibu misalamu yako
 
Ni kawaida iyo mbona ingawa kuna watu tena hawa ndo wengi ni wambeya sana,unakutana na mtu maswali anayouliza unatamani umjibu shit,, utasika,,"Uko wapi siku hizi,,una ishu gani,,unafanya kazi wapi,,aisee umekonda sana unaumwa?.,naona sa hivi umependeza una hela ntakuja kukopa bana,,,hivi pale ushahama?,, ulishaolewa au bado?? Una watoto wa ngapi?? Maswali hayo yote mi kiukweli siwezi kumuuliza mtu halafu mi Nina bahati mbaya ya kuulizwa,,,

Watu wanakera sana..
Hawajui baadhi ya maswali unaweza mjeruhi mtu,,
 
We itikia tu, kwani ukijibu kama kawaida kuna tatizo?/
 
Mbona na wewe mleta hoja umeandika maneno mengi yasiyo ya lazima wakati ungeweza kuandika kwa kifupi tu na kueleweka ili kuokoa muda wako na wa wengine?
 
zingatia muktadha,
uswahili peleka kwa waswahili.
 
Waambie hao mkuu...!!! maana nikisema mm watasema "huyu Shombe kashaanza"
 
Mimi: niaje
Yeye: full vipi
Mimi: bomba, uko poa
Yeye: niko poa
Mimi: kabisa
Yeye: kabisa yani
Mimi: kitambo sana man
Yeye: mbona nipo aisee
Mimi: nchi hii hii?
Yeye: yap sana tu
Mimi: basi poa mi ndio napatikana hapa
Yeye: usihofu boss nitapita jioni
Mimi: mia mia mzee
Yeye: sana bab mida
Mimi: hasta la vista
 
Back
Top Bottom