Sipo comfortable na salamu za kiswahili

Sipo comfortable na salamu za kiswahili

Mimi: niaje
Yeye: full vipi
Mimi: bomba, uko poa
Yeye: niko poa
Mimi: kabisa
Yeye: kabisa yani
Mimi: kitambo sana man
Yeye: mbona nipo aisee
Mimi: nchi hii hii?
Yeye: yap sana tu
Mimi: basi poa mi ndio napatikana hapa
Yeye: usihofu boss nitapita jioni
Mimi: mia mia mzee
Yeye: sana bab mida
Mimi: hasta la vista
 
kuna shida...? au unaringa sasa hutaki salamu zetu....?
 
m: najee man?
y: a guda guda
m: ishu n gan mzee?
y: fulu mfulele
m: haina nouma bas km vp mishale
y: miaaaaaaa
 
Jina lenyewe Ndege unambwembwe hizo, je ungeitwa Europlane John si hata salamu ungezitaka kwa kilatino?
 
Sina tatizo na salamu za Waswahili wenzangu, nisalimie kadri uwezavyo naona poa tuu....
 
Kuna wale akikumaliza wewe anahamia kwa watoto wakati hata hajazoeana kihivyo
Yeye: Wanao.!
 
Salamu yoyote, iwe ndefu ama fupi, itapendeza kwa wahusika kama/iwapo nyote mambo yenu yatakuwa mazuri...!!
 
Mimi ata sioni shida iko wapi
Maneno yote hayo hata dakika haifiki unachapa mwendo.

Pia inategemea na aina ya mtu uliekutana nae kuna mwingine mmepoteana mda mrefu nilazima mtaongea kiasi nahapo ndipo maswali Kama umeoa/olewa yanakuwepo.unawatoto au huna

Na kuna watu wao wanapenda tu salamu ni lazima afuate huo mtiririko wote ndio aridhike.
 
sio kesi lakini ni mtizamo wangu tu kuwa salamu zetu huwa zipo kinafki sana.unakuta yes mnafahamiana kabisa na kila mtu anajua jinsi maisha yanavotukimbiza resi,ubize ila kwenye salamu tu mmekutana naye labda mtaani au njian mtu atataka musalimiane dakika kumi,maneno mengi afu ni yale yale
Mfano wa story tumekutana
Mtu:habari ndege
Mimi:safi sana
Mtu:upo?
Mimi:yeah nipo
Mtu:huonekani
Sasa huwa najiuliza huwa tumekaririshwa hadi salamu mtu anakuambia huonekani as if kwamba imeandikwa mtakuwa pamoja saa zote.na wakati anajua kabisa maisha tupo mazingira tofauti
Mfano wa story nyingine
Mtu:shwari
Mimi:ni shwari
Mtu:kama kawaida?
Sasa najiuliza hio kawaida si ndo maana tunaendelea kuishi
Mtu:nambie
Sasa nikwambie kitu gani wakati tunayoyaona ndo haya haya
NINGEWEZA KUTOA MIFANO MINGINE YA SALAMU AMBAZO ZINABOA ILA POINT YANGU YA MUHIMU JAPO SIO YA MSINGI NI KUWA SALAMU ZA KISWAHILI NI KAMA VILE TUNAKARIRISHWA MANENO YA KUSEMA.MPANGILIO WA MAZUNGUMZO HASA TUKIANZA NA SALAMU TUPO SLOW SANA..ME MTU AKIANZA KUZINGUA KWENYE SALAMU TU NASHINDWA KUVUMILIA KUJIAMIN KUONGEA NAYE NAMUONA KAMA AMEKAA KINAFKI NAFKI.namkubali mtu ambaye tukisaliamana tuna flow naturally SASA UNAKUTA MTU HANA CHS KUKWAMBIA LAKINI ILI MUONGEE ATATAKA MSALIMIANE MUDA MREFU
NB:maisha ni zaid ya salamu,hivyo hali kama hizo haziNikwazi sana lakini ndo hivyo huwez kumkataza mtu kufikiri.ndo nimefikiri hivyo kwamba kama huna habari mpya kumwambia mtu msalimie kifupi tu
Mambo vip
Poa
Basi afu pita hivi..sio uanze kumchora mtu akujibu misalamu yako
Hakuna hata salamu moja ya kiswahili hapo,hayo ni maneno ya kihuni mitaani,salamu za kiswahili huzijui? Wengine humu nao wanachangia kwa kukurupuka tu!!! Kama ndiyo mnasalia hivyo basi tambueni kuwa nyie ni‘WAHUNI’!!!!!!!!
 
Wasap

Long time no see

Tel me

Hizi ni salamu za kawaida tuuuu
 
Back
Top Bottom