kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,127
- 24,429
Hakuna kitu kinanikera kama kuombwaombwa misaada yaani sasa hivi kila simu nayopokea kutoka kwa ndugu na jamaa ni za kunililia shida tu
Sijui watu huwa wananionaje mimi?Hapa nawazungumzia ndugu hawa wa ukoo mmoja na sio hawa nilozaliwa nao
Utapigiwa simu utaombwa hela na kila misaada hata kama ukijaribu kumuelewesha kuwa kuna mambo unapitia au hauna fedha kwa wakati huo au hela umepeleka kwenye miradi fulani ndo kwanza hawakuelewi
Mimi sijui watu huwa wanaonionaje wakuu, kila mtu nikikutana nae ni wa kunililia shida tu,
Cha ajabu huwa nina mengi sana na mambo yangu huwa napambana natatua mwenyewe bila kuomba msaada wao wanashindaje kutatua shida zao wenyewe?Kuombaomba ni ujinga labda iwe imekua too much na tatzo limekuzidi ngumu mtu ni nzima ana miguu na mikono haumwi wala nini yupo fiti anaombaomba kweli?
Wakuu mimi ni mtu wa tofauti kidogo mimi ni ngumu sana kumuomba mtu kitu yaani hata nyumbani wife tukipungukiwa na nini bora tukose tu kwa wakati huo hadi hela ipatikane sio kuomba...Kwenye maisha yangu sina utamaduni wa kuombaomba kabisa.
Niwaambie tu ukweli mimi huwa nawasaidia walowahi kunisaidia tu au watu baki wengine wenye uhitaji, Nimesoma darasa la kwanza hadi Chuo kikuu kuna kipindi nilikula msoto nyie acheni tu dadeki nilikonda nikawa kama uzi sio mjomba, sio shangazi, sio binam wala sio baba mkubwa alonisaidia walikua wananitazama tu kama uchafu leo nimepata simu ndo zinalia.
Mimi wazazi wangu na ndugu zangu na wote walowahi kunisaidia maishani nipo loyal kwao vibaya mno, huwa najitoa kwao kwa hali na mali, huwa naamini kuwa napaswa kula na wale walionisaidia tu, yaani kama kipindi cha nyuma nilikua nateseka nakuomba msaada au unapaswa unisaidie na uwezo ulikua nao lakini ukanipuuza usitegemee kukusaidia hata unakufa, nitakuacha ufe kwakweli.
Kiukweli naonekana nina kiburi, roho mbaya na majivuno kisa sitoagi hata senti kwa mtu, lakini mimi huwa nasema kabisa kuwa kama hukuwahi kunisaidia usitegemee msaada wowote kutoka kwangu...
Kwakweli nachukia kuombwa hela ile mbaya, mimi akiniomba hela mke wangu, wazazi wangu, mchepuko,watoto wangu, ndugu zangu na marafiki na jamaa ambao kwa shida na raha tunasaidianaga inatosha
Bora nimsaidie mtu baki kuliko kumsaidia ndugu nilozaliwe naye au wa ukoo au jamaa ambaye kipindi cha msoto hakunisaidia chochote zaidi ya kunicheka
Kwenye maisha yangu nimechekwa sana,nimebezwa sana nilishakatishwa tamaa sana wengine hadi nimezaliwa nao lakini nilisimama kiume na kufika hapa nilipofika
Waache waseme sana kwamba mimi nina roho mbaya au naringa ila wallah hawataona hata senti moja kutoka kwangu yaani ni kusema kuwa watasubiri sana nilivyokua nadharauliwa naonekana takataka na siwezi chochote halafu leo huyo mtu ananiomba hela haki nakumbuka nilipotoka huwa napata hasira sana nikikumbuka misoto niliyopitia machozi hunitoka kwahiyo hela yangu sio ya kuchezea kabisa na bado nitaendelea kuwatimulia vumbi tu.
Kila mtu abebe msalaba wake mwenyewe.