Sipati jibu kwanini walimu tunafanyiwa hivi?

Msigazi Mkulu

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
4,110
3,269
HIVI WALIMU TUMELOGWA NA NANI?

Hivi ni kweli kwamba hatujui hata kufikiri kwa kina na kuangalia mambo kwa mtazamo mpana zaidi au tumeridhika na hali?
Hapana jamani Naomba Tujaribu kuelimishana wenyewe kwa wenyewe japo kidogo kidogo kidogo huenda tukamjua mchawi wetu.
Mimi mwenyewe ni CCM lakini baada ya kuona mfumo ni mbaya niliamua kuachana na Uchama kadi nikaiweka ndani sasa naimba Mabadiliko.

Badala ya kukaa na kujiuliza ni kwa nini Nurse aliyeishia Form Four akuzidi maisha wewe Graduate umekaa tu na kuridhika.
Hatuwazi kwa nini Askari analipwa laki 4 na ushee na kila tarehe 15 anapewa karibu 170000 huku hakatwi kodi ya PAYE
(PAYE AS YOU EARN)
Ambayo ni laki na ushee wewe Mwalimu wa degree unaimba tu CCM OYEE

Kumbuka Askari huyo alifeli form IV wewe ukafaulu ukaenda Form V na VI ukafaulu ukakopeshwa na HESLB mamilioni ukasoma degree
Leo umesain mkataba unalipwa laki 63000 kama total salary huku take home ikiwa
(..................)
Nisiseme manake inatia hasira.

Nadhani huwa hatupigi hesabu nyepesi kwamba askari aliyeishia form ni kama anakuzidi mbali mno tena yeye ana marupurupu na nyumba huwa lazima apewe alipiwe maji na umeme huku wewe mwalimu huna Marupurupu na umepanga kachumba kamoja kadogo kama choo kila siku unapigwa vumbi la chaki mwishowe uugue TB ufe ukikohoa damu.

Sisemi sisi walimu ni wajinga hapana nahisi labda tunajichukulia sisi ni wadhaifu tu jambo ambalo sio sahihi kabisa.
Tujitahidi kuwa wadadisi kidogo na kuwaza juu ya maisha yetu hatujaumbwa kuwa masikini bhaaana!.

Siku 1 nilisema darasani kwamba ukiamua kuwa Mwalimu ni kujichagua kuwa masikini na kuishi maisha duni labda uwe fisadi wa kuiba mali za shule au ufanye ubadirifu jambo linalowafanya watu wenye kupenda maisha mazuri na utajiri kuikimbia fani hii.
Na ndio maana walimu wengi wenye degree katika kizazi hiki cha sasaivi ni watoto wa familia za kimasikini au watoto wa wakulima waliohofia wasingesoma ualimu chuo kikuu basi huenda wangepewa mikopo midogo au kutopewa kabisa hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao hizo kielimu.
(Yaani walisoma ualimu ili wapate mikopo)

Niliwahi kukaa na kujiuliza hivi ningekuwa Mwanafunzi kuna mwalimu wa shule ya kata angeweza kunishawishi nisome nifike chuo ili niwe na maisha mazuri wakati yeye kasoma hadi huko lakini anaishi chumba mithili ya stoo?
Napolifikiria jambo hili nawaonea huruma walimu wenzangu.
Yaani ukiwa mwalimu huwezi kuwaza mambo makubwa?
Huwezi kuwa na ndoto za kuwaza ubilionea!
Hii hapana jamani tujiangalie tena na tukatae ualimu sio wito hii ni kazi kama kazi nyingine.
(Ni ajira yetu kwa nini watuhadae eti ni wito)

Binafsi Siwezi kukubaliana na hali hii ndio maa na nilipoenda kuripoti kituo cha kazi sikukaa maana nisingeweza maisha yale,
Maisha ya ajabu ajabu ilimradi kusogeza siku.
Kuishi kwa madeni January mpaka December.
Yaani unadaiwa na Bodi ya mikopo, unadaiwa na BANK, unadaiwa na Saccos, unadaiwa Rafiki yaki, unadaiwa Sokoni na dukani pia😳
Mimi hii hali ilinishinda nikakimbia.
🏃🏽🏃🏽🏃🏽🏃🏽🏃🏽

Mimi nina ndoto za kuwa na Gari zuri kuliko lile la marehem baba yangu,
Nataka nije kujenga nyumba nzuri,
Watoto wangu waje wasome shule nzuri kuliko nilizosoma mimi,
Nimepanda ndege nilipomaliza form VI nataka mwanangu apande tu kama bus.
(Haya maisha kwa walimu wengi wa serikali ni ndoto za Alinacha)

Tena nawaomba sana tusiishie kusema tu sijui kidumu Chama huku usiku watoto wetu wanalala kitanda kimoja wa kike na wa kiume.
Tunabaki kuponda sijui CHADEMA wachagga mara CUF waislamu au ACT ni CCM B pasipo kuwa tumejua ni nini tunaongea kwa nini walimu tunakuwa wapotoshaji badala ya waelimishaji?

Mimi huwa nashangaa walimu hawajui wao ndio watumishi masikini kuliko Wote lakini hawataki kubadilika sijui aliyetuloga keshakufa!😩

Walimu wengi Tuna maisha ya ajabu mno lakini hatujijui,
Maisha gani kuandikwa kwenye madaftari ya madeni madukani kwa watu aaah😳
Yaani mshahara huu hautoshi kukuwezesha kuishi mpaka ukute mshahara mwingine?😳
Kwa hali hii ualimu siutaki ng'o.

Kama nitakuwa mwalimu Niwe wa private schools.
Nilipwe vizuri niishi vizuri, nile vizuri na nivae vizuri, nipate huduma za kijamii nzuri
Sio kuwa ka hawa walimu wa serikali hususanu wa shule za kata wenye maisha ya kutisha.
Kumbe ndio maana rafiki yangu mmoja ni mwalimu lakini kaamua kuwa Bodaboda.
Sijajua tu madhara ya upepo ule wa Bodaboda changanya na vumbi la chaki yatamjia kwa style gani miaka miwili ijayo.

Ebu jiangalie wewe hapo ni kijana mdogo una degree lakini sidhani hata kama umewahi kula fillet fish huenda hata huzijui na wakati kilo 1 ni 7500 tu
Sidhani kama unajua hata Sandwich labda unajua pizza na Bagga tu ambazo huenda umekula ukubwani.
Hivi umewahi kula prons?
Umewahi kula hata beef sausage kweli au ndio wale wale niliosikia hata mayonnaise mlijulia vyuo kikuu?
Hebu jiulize utaishi kwa kunywa chai na kiporo mpaka lini?
Ni nani alikwambia kiporo ni kitafunwa?
Chai yenyewe ya rangi sukari ya kurushia kukata ladha ya maji na majani lakini unaimba CCM OYEE una wazimu au?😱

Ngoja nikwambie kwa elimu yetu hii ya degree walau kwenye chai zetu tunapaswa mfano ukiwa na kijimkate basi pembeni kuna nutello, kuna blue band au wengine wana drinking chocolate, nido, peanut butter au asali kama ndio hobby yako na wala sio kiporo cha ugali dagaa mwishowe ujitapikie ukiwa unaendesha baiskeli kuwahi kipindi cha kwanza.

Bado Sijajua ni kwa nini walimu wenzangu mnapenda hata wanenu waje kuwa washamba wa vitu vya kawaida kama ninyi.
Hivi Unakubalije mtu std 7 mwanae anakula witter bits sidhani hata kama unazijua,
(Ni chakula cha ngano special kwa watoto kinajenga mwili vizuri sana huchangwanywa kwenye maziwa na ni kizuri sans kwa afya ya mtoto)
Yaani unachukulia poa tu mtu wa std 7 mwanae Anakunywa maziwa ya Red Gold wewe wako hata Lactogen haijui sasa ulienda shule kusoma ili uje kuaibika au kustirika?
Maana haiwezekani mtoto wa mwalimu lakini afya ya kuunga unga akipigwa na homa kidogo tu unashauri apimwe na UKIMWI ili aanze kumeza ARV's mapema kwa jinsi mwili ulivyo dhaifu kumbe hana cha UKIMWI wala malaria ni UTI tu kwa kunywa na kutokula mlo kamili.
(Balance diet).

Mimi nasema hapana nataka mwanangu awe mjanja sio aende kwa jirani anyweshwe strawberry lipps aambiwe sio pombe
Au aone wenzake wakimumunya BILLAR CHEWING CANDS aanze kushangaa Big G gani zinayeyuka zenyewe.

Kiukweli walimu wanaoisapoti CCM huwa wananibore lakini hawajui tu ndio maana nimejikuta nayasema yote haya

Narudia; Bado sijajua ni kwa nini Mtu kama mwalimu hatamani maisha ya kuingia Supermarket kuhemea hata honey popcorns tu ampe mwanae then aende zake nyumbani?
Tena kuna walimu Tangu wameajiriwa hawajawahi kuingia hata supermarket wakiona hata min market wanaona ni maduka ya matajiri peke yao jamani maisha gani haya!!😭😭

Hivi leo hii kwa mfano Mwanafunzi akikuuliza airport pakoje unaweza hata kumjibu kweli!
Hujawahi hata kupanda ndege unafundisha air transportation unajua hata ni muda gani watu wanafunga mikanda wewe?
Unajua kwamba kwenye ndege kila abiria ana mpira wa emergency oxygen akiona pumzi inamuishia anauvaa au ndio umejulia kwenye hii makala?
Hivi unafundisha tourism umewahi kwenda Mapango ya Amboni?
Unaijua Ngorongoro crater kwa kuiona kwenye picha alafu unawafundisha wanafunzi ambao wamewahi kuiona kwa macho hahaha!
Zanzibar kwenyewe hupajui unaishia kupasoma kwenye vitabu na Kufundisha sijui siku unamfundisha Mzanzibar utageuka Mwanafunzi au listener?

Nauliza: Huvi Kwani nyie Walimu hamtaki Maisha Mazuri kama ya watu wa CCM?
Ina maana hamtaki mkitoka huko madongo kuinama mkakeni Secondary mnakuja huku mjini kutusalimia ndugu zenu tuwapokelee Airport sio Stand za Mabasi?.

Ina maana Walimu mnafundisha lakini hamuelimiki?
Sasa mbona mnasahau hata Sifa za Graduates?

Naona inakuwa ndefu mno lakini nimalizie kwa kusema:
"ili useme umesoma your education must reflect evidently in societal life in which you associate"
 
  • Thanks
Reactions: V2d
Nimejaribu kuingia kwenye ubongo"Imagination" wa mwanzisha mada.

Nimewaza jinsi gani unavyoumia,mapito unayopitia n.k

Kwa kweli katika taaluma ambazo zinatakiwa zipewe kipaumbele hapa nchini basi ni Ualimu.Ndio taaluma pekee inayozalisha taaluma nyingine zote zilizopo duniani.Yatupasa tuwape heshima walimu.

Serikali mbona haitambui umuhimu wa hii fani. Mishahara duni,mazingira ya kazi mabovu,nyumba za walimu hakuna n.k Kwa kweli inasikitisha.
 
yani me hiyo ccm inavyoniboa sijui hata niwafanye kitu gani
 
Walimu wanaoishabikia ccm sielewi wanafikiri vipi!kuna tatizo mahali sio bure!
 
yaan nmeishia katikati nmecheka sana serikali hii unaiibia muda tuu mi nliendaga masomoni nkiwa mwaka wa pili nkaahirisha mwaka, nkapiga kazi private mwaka ndipo nkarudi chuo tena nlimtaarifu mwajiri kwa barua tu nlipiga hela mbaya
 
Serikali ibadilishe kwa recruitment system ya kwenda vyuo vya ualimu
Now ile cream ya taifa ndio iende ikasomee ualimu na sio watu waliokosa pa kwenda au wanaofanya ualimu kama daraja la kupitia ili wafikie ndoto zao
 
Back
Top Bottom