ushauri wangu kwa kunjombe endapo rais atalivunja bunge aseme anawapatia vijana uwaziri na wewe ukaingia kichwa kichwa watakumwakyembe nawe uote mabaka mabaka na uvae gloves kama rooney awapo uwanjani na pama kama la micheal jackson kataa kabisa naona move hiyo wazee ccm wanataka wawangamize vijana wao wanaowaona viherehere shauri zako ukiingiwa na tamaakwa hali ilivyo sasa hakuna mtanzania atakaye endelea kuogopa ujinga wa kutishiwa kuuwawa..
Kwani tiyari watu wameshauwawa kimwili..
Sema tena sijasikia....huogopi kufanywa nini????????????
Ungekuwa jirani na Pinda angekuchapa kofi la kukosa uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility).
OSOKONIHicho chama unachokipenda si ndio hicho kinacholea ufisadi? sio ndio hicho kinachukia wapambanaji wa ufisadi kama wewe, mwakyembe sitta lembeli nk? ukiendelea kubaki huko huna uhuru wa kutosha na pia hao sio wema kama hata wanakutishia kukuua kwa nini uendelee kushiriki nao? umesahau yaliyompata Kolimba? Tafuta chama kingine uhamie maadamu unafahamika kwa uchapa kazi na kutetea maslahi ya umma uchaguzi ukirudiwa utashinda tu!!!!
Mkuu, nani alikwambia Balali alikufa? Kumbe siku hizi kuhamishwa nchi pia kunaitwa kufa??Hata DAUDI BALALI alisema haogopi kufa lakini amekufa, vivyo hivyo HORICE KOLIMBA
tunakuppongeza sana kamanda wetu kwa uamuzi wako wa busara kwani hakuna wa kumuogopa zaidi ya mungu baba yetu wa mbinguni kama ni kifo kila nafsi itaonja mauti tuko nyuma yako tunakuombea usikate tamaa watanzania wote tupo nyuma yenu.sema ukweli daima na utakuwa huru daima
Hata DAUDI BALALI alisema haogopi kufa lakini amekufa, vivyo hivyo HORICE KOLIMBA
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, ameapa kuwa yuko tayari kufa kwa ajili ya kutetea Watanzania wanyonge na kwamba haogopi vitisho uchwara vinavyotolewa na baadhi ya watu.
Alisema kamwe hawezi kukaa kimya akitazama namna Watanzania wanavyoporwa haki zao na viongozi wachache wenye uroho wa madaraka.
Hatuwezi kufumbia macho wizi huu unaoliangamiza taifa kwa hofu kuwa ni chama changu. Ubunge wangu ni kwa manufaa ya Wana Ludewa na Watanzania wote, hivyo, wanaonishambulia wao ndio maadui wa CCM na Watanzania, alisema mbunge huyo.
Alipuuza madai kuwa hatua yake ya kuungana na wapinzani katika suala la kutia saini kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ni hatua za kukihama chama chake.
Hata DAUDI BALALI alisema haogopi kufa lakini amekufa, vivyo hivyo HORICE KOLIMBA
Hata DAUDI BALALI alisema haogopi kufa lakini amekufa, vivyo hivyo HORICE KOLIMBA
Sema tena sijasikia....huogopi kufanywa nini???????????? Ungekuwa jirani na Pinda angekuchapa kofi la kukosa uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility).