Siogopi kufa: Filikunjombe!

Siogopi kufa: Filikunjombe!

Movement

Member
Joined
Mar 24, 2012
Posts
58
Reaction score
15
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, ameapa kuwa yuko tayari kufa kwa ajili ya kutetea Watanzania wanyonge na kwamba haogopi vitisho uchwara vinavyotolewa na baadhi ya watu.

Alisema kamwe hawezi kukaa kimya akitazama namna Watanzania wanavyoporwa haki zao na viongozi wachache wenye uroho wa madaraka.

“Hatuwezi kufumbia macho wizi huu unaoliangamiza taifa kwa hofu kuwa ni chama changu. Ubunge wangu ni kwa manufaa ya Wana Ludewa na Watanzania wote, hivyo, wanaonishambulia wao ndio maadui wa CCM na Watanzania,” alisema mbunge huyo.

Alipuuza madai kuwa hatua yake ya kuungana na wapinzani katika suala la kutia saini kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ni hatua za kukihama chama chake.
 
Sema tena sijasikia....huogopi kufanywa nini????????????

Ungekuwa jirani na Pinda angekuchapa kofi la kukosa uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility).
 
Ifike wakati sasa watanzania tuache uoga, vinginevyo na wakoloni watarudi na kutubebesha pembe za ndovu na kutufunga minyororo kaaaama walivyofanywa babu zetu eti kwa kuogopa kufa, Kwani nani ataishi milele?
 
Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, ameapa kuwa yuko tayari kufa kwa ajili ya kutetea Watanzania wanyonge na kwamba haogopi vitisho uchwara vinavyotolewa na baadhi ya watu. Alisema kamwe hawezi kukaa kimya akitazama namna Watanzania wanavyoporwa haki zao na viongozi wachache wenye uroho wa madaraka.
“Hatuwezi kufumbia macho wizi huu unaoliangamiza taifa kwa hofu kuwa ni chama changu. Ubunge wangu ni kwa manufaa ya Wana Ludewa na Watanzania wote, hivyo, wanaonishambulia wao ndio maadui wa CCM na Watanzania,” alisema mbunge huyo.
Alipuuza madai kuwa hatua yake ya kuungana na wapinzani katika suala la kutia saini kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ni hatua za kukihama chama chake.
“Huo ni ujinga. Sina wazo la kukihama chama changu, nakipenda na nitaendelea kuwa mwanachama tu, labda wanifukuze,” alisema.

Tanzania daima
 
Huyu Filikunjombe naye siyo msafi kihivyo. Alipewa rushwa na TCRA ili kuisafisha kutokana na hesabu zake zilizokuwa zimejaa ufisadi. Anyamaze kimya kabisaaa
 
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, ameapa kuwa yuko tayari kufa kwa ajili ya kutetea Watanzania wanyonge na kwamba haogopi vitisho uchwara vinavyotolewa na baadhi ya watu.

Alisema kamwe hawezi kukaa kimya akitazama namna Watanzania wanavyoporwa haki zao na viongozi wachache wenye uroho wa madaraka.

"Hatuwezi kufumbia macho wizi huu unaoliangamiza taifa kwa hofu kuwa ni chama changu. Ubunge wangu ni kwa manufaa ya Wana Ludewa na Watanzania wote, hivyo, wanaonishambulia wao ndio maadui wa CCM na Watanzania," alisema mbunge huyo.

Alipuuza madai kuwa hatua yake ya kuungana na wapinzani katika suala la kutia saini kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ni hatua za kukihama chama chake.

Big up kamanda Filikunjombe kama unenayo yanatoka rohoni!!
 
Hata DAUDI BALALI alisema haogopi kufa lakini amekufa, vivyo hivyo HORICE KOLIMBA
 
Hongera sana kwa kuwa na msimamo, mkipatikana kumi tu wa namna hiyo mwaweza kuifikisha nchi pazuri........NCHI KWANZA CHAMA BAADAYEEEEEEEEE
 
Sema tena sijasikia....huogopi kufanywa nini????????????

Ungekuwa jirani na Pinda angekuchapa kofi la kukosa uwajibikaji wa pamoja (collective responsible).

Collective responsibility?

Ni heri kufa unapambana kuliko kuishi umepiga magoti! - No retreat no surrender, together we stand!.
 
Huyu Filikunjombe naye siyo msafi kihivyo. Alipewa rushwa na TCRA ili kuisafisha kutokana na hesabu zake zilizokuwa zimejaa ufisadi. Anyamaze kimya kabisaaa

Akina Anna Kilango, Ole sendeka wako wapi tuliwasifu sana JF baadaye tunaanza kuwatukana.

Twende taratibu kumwaga sifa nyingi mbele hatukujui
 
Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Vitisho vya wajinga, walafi na wachoyo haviwezi kuinyamazisha. Endelea na kazi yako ya uwakilishi.
 
Kifo ni haki yako pekee ambayo huwezi kudhurumiwa usiwajali hao comrade hawawezi kukutisha juu ya haki yako kwani nao pia hawataishi milele,wakati umefika sasa tupa kila kitu chao ubaki na Mungu pili watanzania tu
 
kwa hali ilivyo sasa hakuna mtanzania atakaye endelea kuogopa ujinga wa kutishiwa kuuwawa..
Kwani tiyari watu wameshauwawa kimwili..
 
huyu jamaa anafikiria 2015, usishangae 2014 akahamia cdm akagombania ubunge 2015 kwa ticket ya cdm, wabunge wengi ni ma hypocrites. Its always about them them and them and never their people..sasa huyu badala ya kutueleza nini atafanya kuhakikisha viongozi wanawajibishwa kila siku anasema yuko tayari kufa, well kufa atakufa tu siku moja hata asipokua tayari, acheni siasa za ajabu ajabu, watanzania wameamka sasa hivi mambo ya kuibiwa mchana kweupe na maneno yenu sasa hivi hamuambulii kitu
 
Wabunge wote wa CCM wanakiri kuona madudu yanayofanywa na serikali yao lakini wafanyeje? NJAA!
 
Back
Top Bottom