Sio vizuri kuudhi wengine

Samcezar

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
13,096
Reaction score
22,826
Habari wanajamvi natumai mpo vizuri.

Kuna hali katika mwili na maisha ya binadamu huitwa hasira. Hii hali nilinaweza sababishwa na sababu za ndani kwa ndani (internal causes) kama vile homoni kuamrisha akili, haiba ya mtu mfano wenye vidada(brats),kisirani,hali ya kiafya ya mtu, historia ya maisha ya muhusika n.k.

Ila pia kuna visababishi vya nje (external causes) kama vile kudhurumiwa,kudanganywa, kucheleweshewa ahadi,kunyimwa haki,kupuuzwa, kudharauliwa,kubezwa,kushtukizwa na jambo usilolitaka, n.k ambavyo leo ndio naanzishia mjadala.
Hasira sio jambo zuri hata kidogo na si hali au tabia ya kuvumilika.

Mimi binafsi ninapomuudhi mtu huwa nakosa amani pia hadi hapo nitakapohakikisha yule mtu kanisamehe na amerejea katika hali ya kawaida.Hasira hufanya heshima ipotee, hasira humharibia mtu siku, hasira hupunguza ufanisi wa mtu, hasira huzaa chuki, hasira huzaa visasi, hasira hutoa amani,hasira sio nzuri kwakweli.

Kwanini umuudhi mtu na ukijua wazi kuwa unafanya vibaya ukifanya hivyo kwanini unamdanganya mpenzi wako na unajua wazi akijua atakasirika kwanini unachukua mwanamke mwingine na wajua wazi mkeo atakasirika,kwanini dokta unanichoma sindano mtoto wa miezi minne au mitano au sita kisa tu sijui kusema na wajua wazi siipendi maana inauma.

Kwanini unafanya mawasiliano ya siri na wavulana huku ukijua wazi mpenzi wako anakujali na akijua haumpi attention anayohitaji unawapa hao wavulana atakasirika kwanini unathamini furaha yako tu kwa gharama ya furaha ya mwenzako na ukijua wazi wewe unapofurahi yeye atakasirika.

Kwanini unavaa chupi ya mwenzako hadi anajua na kukasirika kwanini unakunywa juice au soda ya mwenzako bila ruhusa yake ukijua wazi kuwa utamuudhi kwanini unachukua pesa ya mumeo unakwenda kufanyia mambo yasiyo ya familia yenu bila ridhaa yake na wajua atakasirika akijua.

Kwanini unatumia urembo wako kuhadaa wanaume zaidi ya m'moja ukijua wazi kuwa watakapojuana watakasirikakwanini unatembea na mume/mke wa mtu na wajua kuwa ni jambo linalochochea hasira kwanini hivi ni kwanini kwanini ukipata pesa haukumbuki kulipa lile deni kama ulivyoahidi na unajua wazi hiyo itampa hasira mtu anayekudai.

Kwanini unafanya jambo baya kwa mwenzako halafu hata baada ya kujua kosa lako unakaa kimya ukijua wazi hii itampa hasira kwanini jamani unamuudhi hata MUNGU anayekupenda kwanini unafanya maudhi, kwanini usiende kuishi huko Jangwani maana hiyo tabia yako si nzuri kuishi nayo na binadamu wenzako.

Kwanini usikae mbali na uahirishe zoezi la kuudhi kwanini usiache huo utoto unafanya ili umrudishie amani mwenzakoroho mbaya si nzuri huwa inaharibu haijengi kuudhi wengine ni tabia ya watu wenye roho mbaya.

Sio vizuri kuudhi wengine acha maudhi
 
Bange za Mwananyamala Kisiwani hizo......
 
Ni afya dunia ikiwa na vurugu na fujo za kila aina.
 
Unajua mheshimiwa wanasaikolojia wanasema mtu ambae ni true to him/her self ni yule mwenye uwezo wa kukasirika wazi wazi kwa jambo linalomuudhi na kutoomba msamaha kwa mtu yoyote pindi anapokasirika..lakini ukiwa mtu wa kuficha sana hisia zako za kikasirika na kuomba omba msamaha bila mpango unakua hujipendi na ur not true to urself..unakuwa unajali hisia za wengine kuliko zako(unakuwa fake)....so kuchukia na pia kusema ukweli na watu wakakasirika sio kitu kibaya ni kujitambua na kuwa "true to ur self"
 
This must have been translated from Indonesian.
 
Japo maelezo mengi tena yasiyo na ulazima wowote ila nimekuelewa vizuri kabisa.....
Asanta kwa ujumbe mzuri
 
Kweli lakini.

Ujue sio vizuri mwenzako anataka kuweka wewe unamwambia "naumwa" wakati wala huumwi, haipendezi ujue.

Unamsababishia hasira anatoka nje kama mvutaji wa sigara anavuta sigara, kama mnywaji pombe anaenda kunywa pombe, kama wa kupenda utulivu anaenda sehemu anatulia huku akiwa amejawa na mawazo tele, mara anatokea mlimbwende anamuuliza "kaka kulikoni?" kulikoni mara inakuwa kulikoni mwisho anaamua kumliwaza, sasa kosa hapo la nani?

Ujue uchoyo sio mzuri, hata kama kidogo kula na wenzako, tusinyimane e...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…