Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,415
- 22,026
Nimesoma kwamba katika ufunguzi wa BRT Raisi aliwauliza viongozi wa BRT kuwa ni faida gani imepatikana tangu kuanza kwa mradi wa BRT. Raisi alitoa agizo kwamba kufikia jioni wawe wamempa taarifa BRT imetoa faida kiasi gani.
Kimsingi, haiwezekani mradi wa BRT uwe umepata faida hadi sasa tangu uanzishwe. HAIWEZEKANI. Sababu ni kwamba mradi huo ulianza 2010, ujenzi kukamilika 2015, na kama sikosei ulianza rasmi mwaka jana. Kwa hiyo kwa raisi kuuliza BRT umepata faida kiasi gani hadi sasa, haileti maana na linakuwa ni swali gumu lisiloeleweka kwa mtu yeyote mwenye ufahamu hata kidogo wa biashara, na huenda lisilojibika katika kipindi alichotoa Raisi.
Mradi wa BRT utaanza kupata faida pale ambapo utavuka "Break Even Point (BEP), ambapo labda ni miaka mitano ijayo. Raisi anapaswa kufahamu BRT kupata faida maana yake urudishe fedha yote ya uwekezaji (capital cost) huku unazingatia kitu kinaitwa discounting rate.
Je, Raisi Magufuli alimaanisha anataka kujua kitu kinaitwa "daily gross revenue over operational costs?" Kama ni hivyo, kuikokotoa hiyo sio suala la masaa, hasa ukichukulia kwamba itabidi kwanza uchukue mapato, kisha uingize gharama zote za siku, kutia ndani kiwango cha siku cha uchakavu mabasi, mafuta, matairi, barabara, vituo, malipo ya wafanyakazi, majengo ya ofisi na hata ufikirie kiwango cha urejeshaji wa mtaji (capital servicing).
Kwa ujumla basi, swali alilouliza Raisi wetu na amri kwamba apewe faida siku hiyo halikuwa sahihi kabisa, na ninawaonea huruma waziri na uongozi wa BRT - sijui hata mlienda kumwambia kitu gani. Mie ningesema Mheshimiwa Raisi sina jibu, eidha fafanua una maana gani unaposema faida gani imepatikana, au nitumbue tu maana siwezi kukudanganya!