Sio rahisi

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,193
^^
Naikumbuka siku niliyompigia simu Mama,
Nikamwambia Mama nataka kuoa,
Niliweza kuisikia sauti yake upande wa pili wa simu,
Akitabasamu,
Kisha akaniuliza swali ambalo nililijibu kwa fahari,
Alisema mwanangu,
'Umetumia muda kumjua vizuri'
Nikasema Mama,
'Yeye ni bora kuliko wote'
...
Lakini leo inaniuma
Kurudi kwa Mama
Kwenda kumwambia
Nimeamua kumuacha
Mama,chaguo nililofanya,limekuwa tofauti na matarajio yangu,
Mama akasema
SIO RAHISI KUELEWA MWANANGU,
LAKINI NATUMAINI UTAWEZA NA UTAKUWA MWENYE FURAHA TENA
..
Nakumbuka kanisani
Mchungaji aliposoma maandiko,
Ulionekana mzuri kabisa na mtakatifu,
Sikujua nyuma ya uzuri wako huo,
Kuna rangi zitakazoua maisha yangu ya baadae
..
Nakumbuka tulivounganishwa mikono na mhubiri,
Mhubiri alisoma maandiko,
Akiweka maneno kinywani mwako,
Labda maneno aliyotamka mhubiri,
Hayakuwa ndani yako,
Sasa naelewa wanachomanisha wasemao,
Mwanamke mzuri sana ni pumziko la wanaume wengine,
Ee Mungu naumia
Chaguo nililofanya,
Halikunizalia matunda sawa na nilivofikiri,
Mama anasema,
SIO RAHISI KUELEWA MWANANGU
LAKINI NINATUMAINI UTAWEZA
NA UTAKUWA NA FURAHA TENA.
^^
From LUCKY DUBE
Song IT'S NOT EASY
DEDICATION KWA WOTE AMBAO WAMECHAGUA ISIVYO NA WANAOTEGEMEA KUCHAGUA.
My own translation
^^
 
Hebu nitafutie ya chaguo sahihi........
 
Naipendaga hii nyimbo,namkumbuka my old school friend...

ila ulivyotafsiri sijui nimeonaje
 
Kosea njia utaelekezwa, lakini ukikosea kuchagua mke wa kuoa machungu itakuwa sehemu ya maisha yako yote.
 
Naipendaga hii nyimbo,namkumbuka my old school friend...

ila ulivyotafsiri sijui nimeonaje

^^
Pole kwa kukumbusha mbali,,mmm kuna mahali nimekosea tafsiri au mlikuwa mnausikia bila kuelewa maana yake?
^^
 
pole sana ila kaza buti na kuomba cku ziishe haraka ili upumzike mbinguni kwa furaha.
 
Kitu hiki kimenikumbusha rafiki wangu wa chuo ,alikuwa anaupenda akanifanya na mimi niupende sanaaaaaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…