Sio lengo la ACT Tanzania kupambana na CHADEMA

Sio lengo la ACT Tanzania kupambana na CHADEMA

Hansen Nasli

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2012
Posts
883
Reaction score
340
Sio lengo la Chama cha ACT-Tanzania kuibomoa CHADEMA chama ambacho sote tumeshiriki kwa nguvu zetu zote kukijenga.

Ni shabaha ya ACT-Tanzania kuimarisha mfumo wa vyama vingi kwa kufanya siasa Mpya za masuala dhidi ya siasa za 'personal attacks', kufanya siasa za maendeleo ya wananchi dhidi ya maendeleo binafsi ya wanasiasa, kufanya siasa za demokrasia ya rasilimali dhidi ya uporaji wa utajiri wa nchi kwa faida ya wachache.

ACT-Tanzania inataka kurejesha Tanzania ya wakulima na wafanyakazi ambao wanaona fahari kuwa Watanzania kwa kurejesha misingi ya uadilifu, uwajibikaji, Utu na Uzalendo
 
Toka mwanzo hata hamjakisajili, mlikuwa mnasema kitapambana na CDM! Leo mnakuja nw ngonjera zingine baada ya kupambana na nguvu ya umma. Mbona hamsemi mtaing'oa CCM madarakani 2015?
 
Waweledi wanaelewa Act Inafanya nn ila wale wanaoendeshwa kwa upepo watabaki wanaweweseka kadri upepo unavovuma,Act Tanzania chagua la wakweli na wawazi
 
act ni msingi wa uweledi katika siasa za tanzania

chadema ni chama chenye mpango wa 'allah' ambacho hupambana na vyama vyenye laana kama act na mwishowe hushinda na kuimarika zaidi.
-mwisho wa act ni kilio kikuu cha kusaga meno.
 
Sio lengo la Chama cha ACT-Tanzania kuibomoa CHADEMA chama ambacho sote tumeshiriki kwa nguvu zetu zote kukijenga. Ni shabaha ya ACT-Tanzania kuimarisha mfumo wa vyama vingi kwa kufanya siasa Mpya za masuala dhidi ya siasa za 'personal attacks', kufanya siasa za maendeleo ya wananchi dhidi ya maendeleo binafsi ya wanasiasa, kufanya siasa za demokrasia ya rasilimali dhidi ya uporaji wa utajiri wa nchi kwa faida ya wachache. ACT-Tanzania inataka kurejesha Tanzania ya wakulima na wafanyakazi ambao wanaona fahari kuwa Watanzania kwa kurejesha misingi ya uadilifu, uwajibikaji, Utu na Uzalendo

Wanafiki utawajua kwa maneno na matendo yao. ACT ni mkakati wa CCM kupambana na CDM. Ndo maana siku zote tangu kuanzishwa kwake vita yake imekuwa ni dhidi ya CDM tu, sijawahi sikia hata siku moja mki-ichallenge CCM. Na kadri siku zinavyozidi kusonga ndo rangi yenu halisi inavyozidi kuonekana na wa-Tanzania ndo tunazidi kuwafahamu.
 
Kasisiko,wamarwa na mambo ni walipa fadhila kwa zzito ambao hawatakuja kusahau dhambi mbaya ya usaliti walioufanyia umma wa watanzania.
 
Unafiki kama huu ndio unaowafanya mtimuliwe CHADEMA.ACT walijitanganzia mapema kabisa kuwa ni mbadala wa CHADEMA.Mulifikili CHADEMA mtaibomoa kirahisi kama mdori ulitengenezwa kwa udongo.Mambo yameanza kuwadodea mmeanza kuleta ngonjera zenu kuwa ACT haiko kwa ajili ya kuibomoa CHADEMA mtakuwaje mbadala wa CHADEMA kabla ya kuibomoa kwanza ili mpate nafasi hiyo?.
 
Sio lengo la Chama cha ACT-Tanzania kuibomoa CHADEMA chama ambacho sote tumeshiriki kwa nguvu zetu zote kukijenga. Ni shabaha ya ACT-Tanzania kuimarisha mfumo wa vyama vingi kwa kufanya siasa Mpya za masuala dhidi ya siasa za 'personal attacks', kufanya siasa za maendeleo ya wananchi dhidi ya maendeleo binafsi ya wanasiasa, kufanya siasa za demokrasia ya rasilimali dhidi ya uporaji wa utajiri wa nchi kwa faida ya wachache. ACT-Tanzania inataka kurejesha Tanzania ya wakulima na wafanyakazi ambao wanaona fahari kuwa Watanzania kwa kurejesha misingi ya uadilifu, uwajibikaji, Utu na Uzalendo

Usaliti ni dhambi mbaya sana inayoweza kusababisha maafa.ACT wanaimarishaje upinzani wakati wako kwenye safu moja na CCM kuuwa upinzani?Asilimia kubwa ya wapinzani kama siyo wote wako UKAWA kutetea masilahi ya wananchi.Lakini hakuna hata siku moja ambayo ACT imewahi kutoa tamko la kuwaunga wenzao mkono ili kuonyesha kuwa wako pamoja na wapinzani.Ukiangalia mitandaoni na mitaani ACT ni chama kinachoongoza kwa kuwa na mashabiki wengi wa CCM halafu wanajifanya kuwa ni chama cha upinzani labda kwa maana ya chama cha upinzani kwa kuvipinga vyama vya upinzani.
 
Mleta mada hebu twambie ni watu wangapi wamehamia ACT kutoka CCM tangia msajili chama chenu.

Tiba
 
ACT naona mmejipanga sana. Ila naona makada wa CDM ndo wanaipaisha ACT. Sioni sababu ya watu kulalamika. Nakumbuka CDM imepaishwa na CCM yenyewe kwa gharama ndogo sana.

Hiki nakiona ACT.
 
Wapo wengi sana na wanaendelea kuingia na sio ccm au chadema tu vyama vingi sana na huu ni mwanzo tu
 
Hansen Nasli,
ACT-Tanzania inataka kurejesha Tanzania ya wakulima na wafanyakazi ambao wanaona fahari kuwa Watanzania kwa kurejesha misingi ya uadilifu, uwajibikaji, Utu na Uzalendo​
Mkuu haya maneno ya kweli au mnachapia tu? Maana nimewahi kusema humu JF miaka kama 5 au 6 ilopita kwamba mwanasiasa yeyote ama chama chochote kitakacho weka maslahi ya WAKULIMA na WAFANYAKAZI mbele ya malengo yake, basi mtu huyo ama chama hicho kitakuja kuwa chaguo la Wananchi..

Je, kweli ACT mnataka kurejesha Tanzania ya Wakulima na Wafanyakazi? na kivipi yaani..
 
Ukitazama kwa jicho la kiutafiti zaidi utagundua act ni chama chenye mwelekeo wa kuubomoa upinzani, ndo maana kimesajiliwa harakaharaka! Watanzania watakumbuka ccj iliishia wapi? Kisa ni kuwa ccj ilikuwa ina dhamira ya kuibomoa ccm!
 
Wapo wengi sana na wanaendelea kuingia na sio ccm au chadema tu vyama vingi sana na huu ni mwanzo tu


Bwan Nasli, kinachoonekana ni kwamb ACT inapata caverage kubwa sana kutoka kwa gazeti la uhuru na gazeti la jambo leo ambayo yanamilikiwa na ccm? Huoni kama hapa kuna namna? Sijaona magazeti haya mawili yakitoa positive caverage kwa vyama vingine vya upinzani!

Halafu hata wachangiaji wengi wanaowaunga mkono hapa jamii forums ni akina Msalani na kundi lake la vjana wa lumumba. Hawa ccm wana mapenzi gani na ACT kama chama cha upinzani? Au Act sio chama cha siasa au siyo wapinzani wa ccm?
 
Hawajitambui hawa Mkuu...Wameonja joto ya jiwe sasa wameanza kubadili kauli zao. Vongozi wa chama hiki bado wanafichwa sana, hili ni la kushangaza sana.

Toka mwanzo hata hamjakisajili, mlikuwa mnasema kitapambana na CDM! Leo mnakuja nw ngonjera zingine baada ya kupambana na nguvu ya umma. Mbona hamsemi mtaing'oa CCM madarakani 2015?
 
Hansen Nasli,
Mkuu haya maneno ya kweli au mnachapia tu? Maana nimewahi kusema humu JF miaka kama 5 au 6 ilopita kwamba mwanasiasa yeyote ama chama chochote kitakacho weka maslahi ya WAKULIMA na WAFANYAKAZI mbele ya malengo yake, basi mtu huyo ama chama hicho kitakuja kuwa chaguo la Wananchi..

Je, kweli ACT mnataka kurejesha Tanzania ya Wakulima na Wafanyakazi? na kivipi yaani..

Tukikuambia wafuasi wa ACT wanaoendesha maisha kwa msaada wa CCM huamini. Pata elimu hii sasa ACT ni nyumba ndogo ya CCM!
 
Waweledi wanaelewa Act Inafanya nn ila wale wanaoendeshwa kwa upepo watabaki wanaweweseka kadri upepo unavovuma,Act Tanzania chagua la wakweli na wawazi

Act ni msingi Wa uweledi katika Siasa za Tanzania

ACT naona mmejipanga sana. Ila naona makada wa CDM ndo wanaipaisha ACT. Sioni sababu ya watu kulalamika. Nakumbuka CDM imepaishwa na CCM yenyewe kwa gharama ndogo sana.

Hiki nakiona ACT.

ACT ni nyumba ndogo ya CCM!
 
Back
Top Bottom