samnas
Member
- Oct 11, 2015
- 35
- 1
Hakuchoka kumuomba mungu msamaha na amjaalie aweze kupata mtoto, japo kwake ilikua ni ndoto ya alinacha. Ochu furaha yake aliokua nayo ilianza kufifia, hata wafanyabiashara wenzake hawakuelewa nini kilimsibu mwenzao, hata walipomuuliza hakuweza kuwajibu zaidi ya kuwaambia yupo kawaida. Hali hiyo iliendelea katika familia hio kwa muda mrefu bila kujua nini wafanye, hakuna aliyejua kati yao wapi alikuepo hashir na wala hawakua na uhakika kama ni kweli kichanga hiko kiliweza kuendelea kuishi, kwao hashir alikua ni pengo kubwa au jicho ambalo likitoka huacha kilema cha maisha, walipoteza jicho lao kwa dharau kabisa bila kufikiria nini kingetokea maisha ya baadae. Majuto ni mjukuu waswahili husema, ndicho kilichowakuta wanandoa hao baada ya kulitambua kosa lao.
Nani angeliwasaidia juu ya tatizo lao? Ni kweli zuwena asingekua tayari kumsikia mumewe ochu akitaka kuongeza mke wa pili kisa kilema cha kutopata mtoto alichokua nacho, alilitambua hilo ochu na hakutaka kumkera mkewe kipenzi zuwena, hivyo na huzuni aliyokua nayo iliyoambatana na tamaa ya kupata mrithi wake aliweza kujizuia na kuendelea na kazi zake za kila siku huku wakipeana moyo ipo siku watampata mtoto wao.
''Mume wangu, huyu mfanyakazi kapatwa na matatizo kwao, hivyo ameniomba likizo ya muda mrefu arudi kwao kigoma'' zuwena alimwambia ochu
''Eh!! Balaa gani tena limemkumba jamani?''
''Mama yake kapatwa na maradhi ya kiharusi ghafla...''
''Aisee, maradhi mengine haya...mh...mpe pole sana,, basi sawa itabidi tutafute mfanyakaz mwengine kipindi hiki kifupi au wasemaje??''
''Hilo tutaliongelea mume wangu, kwanza tumalizane na hili la Sada''
''Mh basi sawa''
Ilipita miezi mitatu bila ya kupata mfanyakazi nyumbani kwa ochu, zuwena alikua akifanya kazi zote za nyumbani hapo, alimlalamikia sana ochu amtaftie mfanyakazi lakini ochu nae kazi alizokua nazo ilikua ngumu kumtafuta mfanyakazi. Jumapili mnamo majira ya saa 8 mchana Hashir alimuaga bibi yake bi.zai na kumwambia anaenda kutafuta kazi ili wapate chochote cha kula,, aliyachoka maisha ya dhiki na kutamani apate kazi yoyote ili aweze kumlisha bibi yake, mtu pekee aliyebaki kama kiongozi wake maishani, tangu alipo mpoteza babu yake hakuweza kuendelea na masomo, alimaliza darasa la saba kwa kusaidiwa kulipiwa na baba wake jasmin. Hashir alielekezwa na rafiki yake chidy aliyekua akiishi nyumba ya tatu mkono wa kulia baada ya nyumba ya mzee ochu huko Temeke hospitali. Alipopata taarifa hizo ndipo Hashir Alielekea moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Ochu, alikutana na zuwena mke wa Ochu na kumwambia lengo lililompeleka pale. Zuwena hakuweza kumkatalia kufanya kazi nyumbani hapo sababu ya kutafuta mfanyakazi kwa muda mrefu bila mafanikio.
Haikua rahisi kwa wawili hao kutambuana, ni miaka mingi tangu wapoteane, hivyo hawakutambuana, hashir alifurahi kupata kazi za ndani kwa zuwena, na alianza kazi rasmi wiki iliyofuata.
★★★★★★
Miezi miwili baada ya kifo cha mzee kauchume, matokeo ya darasa la saba yalitoka na Hashir aliweza kufaulu kwa ufaulu wa juu sana kuliko mtu yeyote shuleni hapo akifuatiwa na chidy, jasmin nae hakua nyuma, alichukua nafasi ya 9 hakutaka mchezo. Kwa ugumu wa misha aliyokua nayo hashir hakuweza kuendelea na masomo baada ya kukosa mdhamini na muhimili wa ada za sekondari pamoja na sare za shule. Alipenda sana kukaa karibu na bibi yake kwa sababu hakuwa na mtu muhimu mwengine dunian baada ya huyo na aliyekwisha kufariki. Ndoto zake za kuwapata wazazi wake ziliyeyuka ghafla na kujikuta akianza kutafuta maisha ili waweze kuishi na bibi yake, aliyachoka maisha ya kuomba omba, alimwambia rafiki yake chidy kuhusu suala hilo naye hakua nyuma kumsaidia. Alimuelekeza ilipo nyumba inayotafuta mfanya kazi wa ndani naye hakusita kwenda.
..
..
Je wahisi hashir angelitambua kua amepata kazi kwa wazazi wake wawili angelifanya nini? Na wangejihisi vipi wazazi wake baada ya kulitambua hilo.
Usikose kufatilia riwaya hii ya kusisimua sehemu ya #7